nini maana ya Unafiki na sifa za unafiki katika quran na sunnah

Mnafiki ni yule anayeukubali'Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha.

nini maana ya Unafiki na sifa za unafiki katika quran na sunnah

  1. Kuepuka Unafiki 

Mnafiki ni yule anayeukubali Uislamu mdomoni (kwa kauli tu) lakini moyoni mwake na katika matendo yake anaukanusha. Wanafiki wanaainishwa vema katika aya zifuatayo:-

“Na katika watu wako wasemao: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Wanataka kumdanganya Allah na wale w alioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao, nao hawatambui.” (2:8-9)

Wanafiki pamoja na kuonyesha imani ya uwongo, ni maadui wakubwa wa Allah (s.w) na Mtume wake. Hushirikiana na Makafiri na Washirikina katika kuupiga vita Uislamu. Wao ni maadui wabaya zaidi kuliko makafiri na washirikina kwa sababu wao hutoa siri za ndani za Waislamu na kuwapelekea maadui wa Uislamu ili wapate kuuhilikisha Uislamu. Hivyo Allah (s.w) amewaahidi wanafiki kuwa watapata adhabu kali kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:



Bila shaka wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto. Hutamkuta kwa ajili yao msaidizi’. (4:145)

Hakuna alama au nembo maalum zinazoonekana katika sura au viwili wili vya wanafiki, bali wanafiki wanatambulika kwa matendo



yao au mienendo yao. Mwenendo wa kinafiki au sifa za wanafiki zimebainishwa kwa uwazi katika Qur-an na Hadith Sahihi. Katika Qur’an Allah (s.w) amewaelelezea wanafiki katika aya zifuatazo:

(2:8-20), (3:167-168), (4:60-63), (4 :138-145), (9:43-68), (33:12-20), (57:13), (59:11-1 7), (63:1-8).



aya hizi tunajifunza kuwa wanafiki wamesifika kwa sifa

Maneno ya wanafiki siku zote ni kinyume na matendo yao.

Wanafiki hujaribu kumdanganya Allah pamoja na Waislamu wakidhani kuwa yaliyo vifuani mwao h ayaju likan i.



    Sifa za wanafiki:

  1. Siku zote wanafiki hufanya ufisadi huku wakidai kuwa wanatenda wema (wanatengeneza).
  2. Huwaona waumini wa kweli kuwa ni wajinga kwa kufuatakwao Uislamu inavyotakikana.
  3. Huwacheza shere Waislamu.
  4. Wanafiki huyapendazaidi maisha ya dunia kuliko ya
  5. Hawapendi kuhukumiwa na sheria ya Allah (s.w).
  6. Hutumia viapo kama kifuniko cha maovu yao.
  7. Huwafanya makafiri na washirikina kuwa ndio marafiki zao wa ndani badala ya Allah na Mtume wake na waislamu.
  8. Hujaribu kushika njia ya katikati baina ya Uislamu na Ukafiri, hivyo huyumbayumba baina ya Uislamu na Ukafiri.
  9. Huenda kuswali kwa uvivu.
  10. Hawamkumbuki Allah(s.w) ila kwa kidogo
  11. Huwafitinisha Waislamu.
  12. Huchukia Waislamu wanapofikwa na kheri na hufurahi wanapofikwa na msiba.
  13. Hawako tayari kutoa mali zao katika njia ya Allah na wakitoa chochote hutoa kwa ria.
  14. Mara nyingi huzifanyia shere aya za Qur-an.
  15. Huamrisha maovu na kukataza mema.
  16. Ni wenye kutapatapa wakati wa matatizo na humdhania vibaya Allah na Mtume wake.
  17. Husema uongo na hawatekelezi ahadi.
  18. Hujitahidi kuwavunja moyo Waislamu wa kweli ili wabakie katika ukafiri sawa na wao.
  19. Hufanya hiyana katika mambo ya kheri na huchagua mambo mepesi mepesi yenye kuwafurahisha.
  20. Wanawaogopa na hukaa upande mmoja na maadui wa Uislamu na Waislamu.
  21. Hupenda kusifiwa kwa kazi nzuri zilizofanywa na wengine.
  22. Huchochea fitna baina ya Waislamu, n.k.


Hizi ndizo sifa za wanafiki kama zilivyobainishwa katika Qur-an. Kwa muhtasari, Mtume (s.a.w) anatufahamisha sifa za wanafiki kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatazo:

Mtume (s.a.w) amesema: Mambo manne akiwanayo mtu humfanya awe mnafiki wa wazi hata kama anaswali, anafunga na anadai kuwa ni Muumini,. Anayesema uw ongo kila anapoongea, anayevunja ahadi kila anapo ahidi, anayehini amana kila anapoaminiwa, na anayechupa mipaka kila unapotokea ugomvi. (Bukhari)

Muislamu wa kweli hana budi kujiepusha na unafiki kwa kujinasua na tabia za wanafiki.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 400

Post zifazofanana:-

Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake Soma Zaidi...

WAJUE FANGASI, AINA ZAKE, DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Soma Zaidi...

nina maambukizi ya zinaha maumivu wakati wa kukojoa na usaha
Mimi nilifanya ngono isiyo salama Tar 14/07 mwaka huu, nilikutana tu na mwanamke ambae sikuwa hata na background yake yoyote hivyo baada ya siku tatu nilijikuta nina maambukizi ya zinaha (maumivu wakati wa kukojoa na usaha), hivyo nilienda hospital na kup Soma Zaidi...

Kujiepusha na Shirk
Shirki ni kitendo chochote cha kukipa kiumbe nafasi ya Allah (s. Soma Zaidi...

FORM FOUR NECTA ENGLISH, (FORM FOUR ENGLISH NECTA PAST PAPERS)
Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

FAIDA ZA MATUNDA MBALIMBALI
1. Soma Zaidi...

jamii somo la 34
Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...

Mitihani aliyopewa Nabii Ibrahimu kutoka kwa Allah
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...