KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)

Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika.

KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)

KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)

Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika. Na mradhi mengine kama malaria na homa ya bonde la ufa. Lakini kuna jambo linaumiza sana fikra za wasomaji. “kama mbu wanaweza kuambukiza maradhi hayo ya virusi, sasa ni kwa nini mbu hawezi kuambukiza HIV?”

 

Kwa hakika swali hili linasumbua fikra za watu wengi sana. Tafiti nyingi za kisayansi zimefanywa ili kuthibitisha majibu sahihi na kuwaridhisha waulizaji. Ukweli ni kuwa mbu katu hawezi kueneza HIV. Na huu ni ukweli ambao haupingiki katu, lakini sasa ni kivipi?. katika makala hii nitakueleza jibu la swali hili katika namna tatu:-

 

  1. Mdomo wa mbu una sehemu kuu 6, katika hizo 6 nne hutumika kutoboa ngozi ya mwili wa kiumbe anachotaka kunyonya damu. Na sehemu 2 zilizobakia ni kwa ajili ya kunyonya damu. Katika sehemu 2 hizo mojawapo ni kunyonya damu na nyingine ni kupeleka mate kutoka kwenye mwili wa mbu na kuelekea kwenye mwili wa kiumbe kinachonyonywa damu. Mate haya hutumika kwa kuifanya damu isigande.

 

Hivyo basi kitu ambacho kinatoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu ni mate ya mbu tu, na si damu, kwani damu haiwezi kutoka kutoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa. Tafiti zinaonesha kuwa mate kati hayawezi kuambukiza ukimwi, hata yawe ya mtu. Hivyo basi hata kama mate ya mbu yataingia kwa mbu kati hayawezi kuambukiza ukimwi kkama amebeba virusi.

 

  1. Virusi vya HIV vikifika mwilini mwa mbu vinaliwa na kupotea kabisa. Virusi vya HIV ili viendelee kuzaliana vinahitaji kupata T seli (T cell), lakini mbu hana seli aina hii. Hivyo virusi vinapofika kwa mbu, vinaliwa pamoja na damu na kupotea kabisa. Kwa sababu hii hakuna uwezekano wa virusi vya HIV kuingia kwenye mate ya mbu ambayo ndio huenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu. Hii inaonyesha kuwa katu HIV haiwezi kusambazwa kwa mbu.

 

  1. hata kama virusi vya HIV vitaweza kuingia kutoka kwa mbu kwenda kwa kiume kinachonyonywa damu (japo jambo hili haliwezekani) hakua uwezekano wa kuambukiza HIV. Tafititi zinaonyesha kuwa ili damu ama mate ya mbu yasambaze HIV inahitajika ang’ate si chini ya mara milioni 10. Jambo hili kisayansi haliwezekani. Pia kummeza mbu aliyebeba HIV HAIWEZEKANI KUSAMBAZA  HIV. Haka akipasukia kwenye jeraha la mtu katu damu yake haiwezi kuambukiza HIV.

 



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 2400

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI

Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho.

Soma Zaidi...
TAHADHARI KWENYE VYAKULA ILI KULINDA AFYA YAKO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
kitabu cha matunda

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
darasa la lishe

Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe

Soma Zaidi...
kitabu cha afya

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
CHUKUWA TAHADHARI KWENYE SHUGHULI ZAKO KULINDA AFYA YAKO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya

Basi tambua haya;- 21.

Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 03

Yajuwe mambo yanayoathiri afya ya miili yetu, jifunze mambo mengi kuhusu afya.

Soma Zaidi...
DARASA LA AFYA, AFYA YA UZAZI, MARADHI NA LISHE BORA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...