Haki ya kumiliki mali katika uislamu

Haki ya kumiliki mali katika uislamu

Haki ya kumiliki mali



Kumiliki mali ni suala la kimaumbile na limeshikamana na silka ya kujihami (self presevation).Katika historia ya binaadamu suala la kumiliki mali limekuwa likiandamana na itikadi au falsafa inayotawala mahali.


Kwa mfano katika baadhi ya jamii za kitwaghuti umilikaji wa mali uko chini ya familia au huwa chini ya 'watu wote' (mali ya umma) au huwa chini ya mtu au watu binafsi. Katika Uislamu kila kitu kipo chini ya miliki ya Mwenyezi Mungu:


'Sema Ee Mola uliyemiliki Ufalme wote! Humpa ufalme umtakaye na humuondolea ufalme umtakaye na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye, kheri imo mikononi mwako. Bila shaka wewe ni Mwenye Uwezo juu ya kila kitu '. (3:26).



Hivyo ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mmilikaji wa hakika wa vitu vyote. Binaadamu anamiliki mali kwa dhamana tu siyo kwa hakika na kwa sababu hiyo ataulizwa jinsi alivyotumia. Katika Qur-an Allah (s.w) ameruhusu watu binafsi au kwa vikundi kumiliki mali pale aliposema:


'Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaom bee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe); na Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye.' (9:103)


Hivyo Uislamu unakubali na kuheshimu haki ya mtu au watu binafsi kumiliki mali.



Mipaka ya Umilikaji mali
(i)Mali hiyo iwe imechumwa kwa njia ya halali. Uislamu unaitambua haki ya kumiliki mali na haki ya kuilinda mali hiyo, lakini mali yenyewe iwe ya halali.



(ii)Mtu anaweza kuiuza au kuitumia mali yake apendavyo maadamu ana akili timamu. Iwapo hana akili timamu, itabidi apatikane mdhamini wa kuingalia mali hiyo kwa niaba na manufaa yake na manufaa ya jamii.



(iii)Maadamu mtu anayo mali basi anao pia wajibu wa kutekeleza majukumu yanayohusiana na mali aliyo nayo.



(iv)Uislamu unakataza ubakhili na israfu (ubadhirifu) katika matumizi. Mwenyezi Mungu anasema:


Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingoni mwako, wala usikunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika. (17:29).


Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila sala; na kuleni (vizuri) na kunyw eni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika Yeye hawapendi wapitao kiasi. (7:3 1).


Ubadhilifu ni kufanya mojawapo ya mambo matatu
Kwanza,
kununua kitu usichokihitaji. Au kununua kitu unachokihitaji lakini kwa kiasi kingi kuliko unavyoweza kutumia. Kwa mfano kutengeneza chapati tano ilihali uwezo wako ni wa kula chapati mbili tu, halafu zile tatu ukazitupa jalalani.


Pili ni ubadhilifu kununua kitu chochote kile cha haramu, hata ikiwa kwa thamani ndogo namna gani. Kwa mfano hata kama masanduku laki moja ya bia yanauzwa kwa shilingi hamsini ukiitoa shilingi hamsini hiyo kununua pombe hiyo unaandikiwa madhambi ya ubadhilifu.


Tatu kutoa sadaka kwa ajili ya kujionesha kwa watu, badala ya kuandikiwa thawabu unaandikiwa madhambi ya israfu.



(v) Uislamu unakataza rasilimali zilizo katika jamii kuachwa bila kutumiwa Mtume (s.a.w) amesema mtu akiendeleza ardhi ana haki ya kuimiliki. Lakini akiiwacha kwa miaka mitatu bila kuitumia mtu mwingine ana haki ya kuiendeleza na kuimiliki.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 124


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

KUAMINI SIKU YA MALIPO
Soma Zaidi...

Kisa cha Israa na Miraji na kufaradhishwa swala tano
Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B. Soma Zaidi...

Matendo ('amal) hulipwa kutokana na nia (makusudio)
Soma Zaidi...

Imam Muslim na Sahihul Mslim
Soma Zaidi...

SHUGHULI ZA KILA SIKU
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...

'Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye'
Soma Zaidi...

Namna ya kutambuwa kibla na umuhimu wa kuelekea kibla wakati wa kuswali
4. Soma Zaidi...

1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
1. Soma Zaidi...

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...