Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri.
Zaka, kilugha ni kukua; kubariki na kuzidi kheri. Husemwa imekua konde yake, na husemwa imeongezeka mali yake, na husemwa umezidi uchamngu na kutenda kheri kwake, na husemwa kwa ku'tahirika (takasika): "Hakika amefanikiwa alieitakasa". (Ash-shamsu : 9).
Na hutumika kwa kusifu: "............ Basi msijisifu usafi. ............". (Annajm : 32).
Na Zaka, kisharia ni jina lililowekwa kwa kukusudiwa kiwango makhsusi cha mali chenye kutolewa kwa kadiri makhsusi na kupewa watu wa aina makhsusi kwa shuruti makhsusi. Zaka imepewa jina hili - kwa vile mali inayotolewa Zaka hukua na kubariki kwa du'a za wale wenye kupewa hio Zaka. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
……Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watao zidishiwa". (Ar-rum : 39).
Hukumu ya Zaka
Kuwajibika Zaka kumekuja kwa Qauli ya Mwenyezi Munguna Hadithi za Mtume s.a.w. na itifaqi ya wanazuoni.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: . "……na toeni Zaka; ………". (Al Baqara : 110).
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Chukua sadaka katika mali zao, ...........". (Tawba : 103).
Na amesema Mtume s.a.w.: . Maana ya Hadithi hii ni kama hivi:
"Umejengwa Uislam juu ya (Nguzo) tano". Miongoni mwa nguzo tano hizo za Uislam ni Zaka. Basi mwenye kukanya kulazimika kutoa Zaka huwa amekufuru, ila akiwa ni aliesilim karibuni hajapata kuufaham vyema Uislam, au amekulia mbali na elimu ya Kiislam. Mwenye kukataa kutoa Zaka, huchukuliwa (na Dola) Zaka yake kwa nguvu; hivi ndivyo alivyofanya Sayyidna Abu Bakar r.a. kwa wale waliokataa kutoa Zaka na akasema r.a.:
Maana ya maneno haya ya Sayyidna Abu Bakar r.a. ni kama hivi: "Wallahi, lau kama wangalinizuilia (wangalikataa kutowa) pingu za ngamia walikuwa wakizitekeleza (wakizitowa) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungus.a.w.; basi ningaliwapiga vita kwa ajili ya hizo".
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana.
Soma Zaidi...Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike?
Soma Zaidi...