Uchumi Katika Uislamu
Maana ya Uchumi
- Ni uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali, rasilimali na huduma mbalimbali katika jamii ili kujenga mahusiano kati ya binaadamu na Allah (s.w).
Sifa za Uchumi wa Kiislamu
1. Dhana ya mafanikio
Huzingatia hatima yake ambayo ni kupata radhi za Allah (s.w) pekee.
2. Dhana ya umilikaji mali
Mmiliki hakika wa pekee wa mali na rasilimali zote ni Allah (s.w).
3. Dhana ya bidhaa
Ni kitu kilicho safi, kizuri, twahara, halali, n.k.
4. Dhana ya matumizi
Haifai kufuja au kutumia mali au rasilimali kwa njia za haramu.
5. Mizani ya wakati katika kutumia
Ni kujiuliza, nini matokeo ya mali au rasilimali hiyo baada ya muda fulani?
Njia na Misingi ya Uchumi Halali Katika Uislamu
i. Pasiwe na udanganyifu wowote katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa au mali.
Rejea Qur’an (17:35), (26:181-183), (83:1-4)
ii. Pasiwe na viapo katika kuuza au kununua bidha, kwani ni miongoni mwa kuuza kwa ujanja-ujanja.
Abu Qatada ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Kuwa mwangalifu na viapo vingi katika uuzaji, kwa sababu japo
kunarahisisha uuzaji, kuna punguza baraka” (Muslim).
iii. Pawe na uhuru kamili kwa mnunuzi kuikataa au kuikubali bidhaa baada ya kuiangalia.
iv. Bidhaa yenyewe iwe halali na iwe imechumwa kwa misingi ya halali pia.
v. Kuwepo na maelewano kati ya muuzaji na mnunuzi bila masharti. Dosari yeyote ya bidhaa ijulikane kabla ya manunuzi kufanyika.
vi. Muuzaji awe na uhuru wa kuuza bidhaa yake kwa bei yenye maslahi kwake na isiwe ya kumnyonya mnunuzi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala.
Soma Zaidi...Maana ya TalakaTalaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili.
Soma Zaidi...Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh
Soma Zaidi...Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.
Soma Zaidi...