Siri ya wageni wale

Siri ya wageni wale

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Siri ya wageni wale

SIRI YA WAGENI WALE INAFICHUKA
Tambua ewe kijana changu, mimi na baba yako tulikutana zamani sana. Tulikuwa ni marafiki sana tukiwa katika umri wa miaka 7 mapka 18. baba yako alikuwa ni mchamungu toka alipokuwa mdogo. Alipata malezi mema sana. Na mimi nilivutiwa nikawa nirafiki yangu sana. Tulikuwa tukifanya ibada pamoja na karibia mambo yetu yote. Wakati nilipohama Misri kuja Yemeni niliweka ahadi na baba yako kuwa nikipata mtoto wa kike ataolewa na mtoto wake na akiwa wa kiume atauoa wako, na tulimuomba Mungu atutofaitishie watoto wetu, yaani akiwa wangu wakike wake wa kiume ama wake wa kike wangu awe wa kiume.



Miaka mingi ilipita hata tukasahau ahadi zetu. Mimi nilichelewa kupata mtoto na hata yeye. Hata hivi miaka yapata 17 iliyopita nikajiwa na wageni wa ajabu, kisha akataja kisha kama kile kilichomtokea baba. Kisha akaenelea kusema. Wageni wale walikuwa si watu wa kawaida. Ni wajumbe waliotumwa kuja kutukumbusha ahadi zetu na kutupatia habari njema za kaupa watoto. Siku ya mwisho walipoondoka wageni wale walinieleza kuwa mtoto wako atao;ewa na mtoto wa rafiki yako kaam ahadi. Atakuja mwenyewe, na utamjuaje wakaniachia pete hii iliyokufikia. Walinieleza kuwa pete hii ikifika mikononi mwako katu haitaondoka.



Wakanieleza kuwa sifa zako utakuwa ni muuza viatu. Hivyo binti yangu anayemsaidia kazi mke wangu nilimuagiza aje kwako kuuliza viatu kama walivyonieleza wageni wale sifa za viatu. Nikamueleza kama utamuona mtu aliyebadilika utambue huyo ni mtu ninaye mtafuta. Mwambie aje kwangu. Sasa nilikuwa na ugomvi na matajiri wenzangu waliotaka kumuoa binti yangu, niliwakatalia sana, na ndipo wakapanga njama ya mumuua.



Bila ya kutambua wakamuua yule mfanyakazi wangu wakidhani ndiye binti yangu. Baada ya tukio lile kutokea na pete kupotea bikajua kuwa pete imesafika kwa mwenyewe, maana wageni wale walinieleza katu ete isingeweza kuibiwa, ila itamfikia mwenyewe. Baada ya kumaliza kuzungumza akaniambia kuwa nisiendelee tena kuwatafuta wageni wale katu sitawaona. Akamuita binti wake nije nimuone.



Akaja binti mmoja akafunua sura yake. Nilihisi kama nimepigwa shoti kwenye mwili wangu. Ghafla joto likapanda, nilistaajabu kabisha kuona kuwa kumbe duniani kuana mabinti warembo kiasi kile. Nilijisemea kuwa wale waliotaka kumuoa hawakukosea katu. Kwa kweli binti alikuwa ni mzuri sana. Kisha mzee akasema “mwanangu nitakuozesha binti yangu bure ila kwa sharti kuwa uwe ni kama mwanangu”



Nilikubali na ndipo nikaozeshwa. Nilimuoa mke wangu nikiwa sina mkono mmoja. Bada ya harusi niliishi na mke wangu kwa muda wa miaka 5. kumbe kulikuwa na watu wananifanyia uaduni. Na ndipo wakanifanyia uchawi nikapata jini hili lililokuwa likinisumbua. Tulipata sifa zako ndipo tukaja Baghadad kupata matibabu. Ha hii ndio hadithi ya kukatwa mkono wangu.



Baada ya tabibu kusimulia hadithi hii akamuelekea Sulatani na kumuuliza “Je! Sultani hadithi hii haiwezi kuwa nzito kama kifo cha mtoa burudani?” mfalme akajibu angalau ila bado. Kama haitahadithiwa hadithi nyingine iatakayoshinda hii, wote mtapoteza vichwa vyenu. Basi hapo Mshona nguo akaja mbele na kusema “ Mtukufu nitasimulia kisa kilichomtokea huyu marehemu jana,kitakuwa ni cha kushangaza zaidi kuliko hadithi za wenzangu waliotangulia kusimulia. Akaanza kusimulia kama ifuatavyo:-



Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 806

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Hadithi iliyosimuliwa na tabibu
Hadithi iliyosimuliwa na tabibu

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Familia mpya baada ya harusi
Familia mpya baada ya harusi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...
Utajiri wa baba na kifo chake
Utajiri wa baba na kifo chake

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Hadithi ya tabibu
Hadithi ya tabibu

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA TABIBU: Tambua ewe Sultani mwadilifu kuwa mimi nimezaliwa katika familia ya wachamungu waabuduji wanaofata mila za kiyahudi.

Soma Zaidi...
Ndani ya jumba la aladini
Ndani ya jumba la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

Soma Zaidi...
Ndoa ya siri
Ndoa ya siri

NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi.

Soma Zaidi...
Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Kifo cha mtoa burudani wa sultani

Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan

Soma Zaidi...