Navigation Menu



Hadithi ya Mshona nguo

Hadithi ya Mshona nguo

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MSHONA NGUO (FUNDI SHERAHANI)


Jana tulikuwepo kwenye sherehe moja ya wafanyabiashra. Mmoja kati ya wafanyabiashara alikuwa na sherehe yake, nayo ni nadhiri aliyoiweka pindi mambo yakiwa safi atalisha watu bure kwa masaa machache ya siku. Katika sherehe hiyo ilipofanyika chakula kizuri kiliandaliwa. Niliwaza hata kuchukuwa chakula niende nikampatia mkewangu naye apate kuonja vitamu, vilivyoandaliwa na mfanyabiashara.


Sikuwa na mtoto hivyo chakula kidogo kingemtosha mke wangu kipenzi kutuliza hamu yake. Kama ilivyo ni kawaida hatukupewa viti vya kukalia bali mazulia mazurimazuri yaliyopambwa vyema yalitandikwa. Waungwana na watumwa tukajiweka vyema na kuandaa matumbo yetu kwa kinacholetwa. Mazulia yalitandikwa kwa mpango wa duara na katikati ndipo kulikuwa na meza kuu.


Zulia lililopo kati lilikuwa ni bora, zuri na lenye thamani kubwa. Kimoyoni nilijisemea โ€œkweli itifaki imezingatiwaโ€. zulia hilo la meza kuu liliandikwa maneno ya kiarabu yaliyonyooka vyema kama mapambo ya mauwa. Rangi ya manjano ilikolea mithili ya dhahabu ya Moroko. Lilipata kubonyea zulia hili midhili ya godoro, hata nikastaajabu uzito ulioje wa zulia hili. Nilitamani niengeliona wakati linatandikwa. Ila nikajiridhisha badala ya kuliona lipo kwenye vipande vilivyoungwa vyema.


Muda haukukawia sana mnawishaji akapita na kutoa maelekezo kuwa wawiliwawili ndio mpango wa kula. Nilikuwa na mwenzangu ambaye alikuwa akijishughulisha na shughuli za unyoaji yaani kinyozi. Alikuwa amevaa vyema na mavazi yamemkaa sawiya. Muda wote hakuwacha kutabasamu utadhani amebebeshwa gunia la furaha. Nilitamani sana kuwa kama yeye hasa ilipoona uso wake ulio mkunjufu usio na mikunyo kama anayekula ndimu.


Nilitamani niwenaye karibu, nipate kujuwa ni manukato gani anatumia, lakini sikufanya hivyo. Wakati haya yote yakiendelea nikathubutu kuchungulia kwa ndani kwa furaha niliona sahani zinaletwa. Sahani za vyakula ziliongozana na waheshimiwa waliopaswa kukaa kwenye zulia la wageni maalumu. Katia msafara huo ilionyesha kweli ni msafara wa wafanya bishara. Kwa mavazi, walipendeza vyema. Wakina ni vijana watatu na mzee wa makamo mwenye ndevu nyeupe na nyeusi..


Walipofika mlangoni wakasimama kuangalia hadhara, wakati huo wanaongea na mwenyeji wa shughuli. Wakiwa wao wanazungumza huku tayari vyakula vilianzwa kugawiwa. Sinia kubwa liliwekwa mbele yetu. Ndani ya sinia hili kulikuwa na vyakula pamoja na vinywaji. Nyama za kuoka na kupikwa vyema, vyakula vipendwavyo pamoja na michuzi mizito. Mikate iliyopikwa vyema na mchuzi wa kutowea. Juisi ya matunda yaliyochujwa vyema, uzitowake utadhani ni asali mbichi iliyokaa siku 10 ndani ya mtungi. Kwa ukarimu walio nao maji ya kuywa yalikuwa ni maji kutoka Miji mitakatifu.


Wale wageni badala ya kuzungumza kidogo wakaanza kuelekea kwenye kikalio chao. Sasa kijana mmoja kati ya wale wageni akakunja sura kwa ghafla, kanakwamba amechanganyikiwa badala ya kuona kitu cha ajabu sana. Haya yote yalitokea badala ya yeye kuangalia upande ambao mimi na wenzangu tuliuwa tumekaa. Watu walipatwa na shauku ya kutaka kujuwa nini kimemtokea mbele za watu pale. Yule kijana ikaonekana anataka kuondoka kwenye shughuli ile. Mwenyeji alionekana kumsihi sana asiondoke lakini wapi.


Kumbe sikuwa mimi tu bali tulikuwa wengi ambao tulikuwa tukifatilia kwa ukaribu tukio lile. Watu walio karibu wakatika kujuwa hasa kwa nini mgeni wetu anataka kuondoka. Hapo mwenyeji wa shuguli akamuomba aeleze kitu ambacho hakukifurahia. Kijana yule akasema kuwa hapa nimeoa mtu ambaye niliapa katika maisha yangi kuwa sitakaa naye sehemu moja, mji mmoja wala nchi mmoja. Kisha akamuonyesha yule kinyozi. Watu wakataka kujuwa hasa ni kitu gani kilitokea kati yao. Kijana akasema kuwa huyo kinyozi ndio sababu ya yeye maisha yake kuwa vululu, kuvunjiaka mguu na mabaya makubwa mengi yalimpata kwa sabbu ya kinyozi. Kisha kijana akaanza kusimulia hasa kilichotokea kati yao:-

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 675


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰2 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU
Soma Zaidi...

Historia ya pango, aladini na kitabu
Soma Zaidi...

ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KITABU CHA PILI HADITHI ZA ALIF LELA U LELA UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA. Soma Zaidi...

HADITHI YA KILEMA WA VIUNGO
HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME
Soma Zaidi...

SIRI YA KIFO INAFICHUKA
Soma Zaidi...

Aladini katika pango la utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Kwanini vidole gumba vilikatwa
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa y Soma Zaidi...