picha

Wanyama ambao hutolewa zaka

(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngo’ombe, mbuzi na kondoo.

Wanyama ambao hutolewa zaka

(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula
Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngo’ombe, mbuzi na kondoo. Farasi na Punda hawatolewi Zakat. Hadith zifuatazo zinatufahamisha juu ya Zakat ya wanyama:
Ali bin Abii Talib (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Hapana Zakat kutoka kwa Farasi na Punda...” (Tirmidh, Abu Daud)



Sayydina Ali (r. a) vile vile am eeleza: “Nina eleza kutoka kw a Mtum e (s.a.w) aliyesema: “Lete moja ya nne ya ushuru, ikimaanisha kuwa kuna Dirham moja kwa kila Dirham arubaini na mtu haijuzu kwake Zakat mpaka awe na Dirham mia mbili (200). Kwa hiyo zinapokuwa Dirham 200 kuna Dirham tano za Zakat kinachozidi kitatolewa kulingana na hisabu hiyo (ya 1/40). Na kwa mbuzi kuna mbuzi mmoja katika kila arobaini mpaka ifikie idadi ya mbuzi 120, kama wakizidi kwa mmoja mpaka 200


watatolewa mbuzi majike wawili wa mwaka mmoja. Kama wakiwa zaidi ya hapo mpaka kufikia 300 mbuzi 3 wa mwaka mmoja; kama hakuna zaidi ya mbuzi 39 haina Zakat juu yake kutokana na mbuzi hao. Na kuhusu ng’ombe, kwa kila ng’ombe ng’ombe 30 kuna ndama mmoja wa mwaka mmoja na katika kila ng’ombe 40, kuna ndama mmoja wa miaka miwili, na hapana Zakat inayojuzu kutokana na ng’ombe waliotiwa kwenye kazi” (Abu Daud).



Nisaab na kiasi cha kila aina ya mnyama



Wanyama waliotajwa watastahiki kutolewa Zakat baada yakuwa katika malisho na katika milki ya mfugaji kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kwa hiyo kila mwaka wafugaji wanatakiwa wahesabu mifugo yao iliyopindukia mwaka na kutoa Zakat kama ilivyoeleza hadithi iliyotajwa hapo juu. Wanyama watolewao Zakat wawe wazima na wachanga wasio na kilema chochote. Watolewe wanyama walio wazuri zaidi tukikumbuka msisitizo wa Qur-an:


Enyi mlioamini! Toeni katika vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyew e msingevipokea isipokuw a kw a kuviangalia. Basi jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi na Asifiwaye. (2:267).



Hivyo, japo majike katika ng’ombe na mbuzi hayaku sisitizwa katika Hadithi mbali mbali kama ilivyosisitizwa kwa upande wa ngamia, ni bora kutoa mbuzi jike au kondoo jike wa mwaka mmoja. Majike ni bora zaidi kuliko madume kwa kuwa yatazaa na kuongeza idadi ya mifugo. Kama katika kuthaminisha na fedha taslimu dume litakuwa na thamani zaidi kuliko jike na ikiwa mtoaji ametoa fedha taslimu badala ya wanyama, basi atoe thamani ya dume. Pia mifugo ya Zakat inaweza kuthamanishwa zitakapotolewa fedha taslim badala ya mifugo yenyewe. Lakini katika kufanya hivyo ni lazima liangaliwe lile litakalokuwa na maslahi bora kwa mpokeaji Zakat. Kama itakuwa ni bora kwa mpokeaji apokee mifugo badala ya kutoa thamani yake itakuwa sawa. Jambo muhimu linalosisitizwa hapa ni kwamba vinavyotolewa Zakat viwe vizuri vinavyopendeka kwa mtoaji na mpokeaji.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Views 1609

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

KUELEKEA BONDE LA UOKOZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUELEKEA BONDE LA UOKOZI Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi.

Soma Zaidi...
Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya mwenye kutabiriwa mtoto wa tajiri

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO.

Soma Zaidi...
Kisiwa cha uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...