Simulizii hii ni nzuri na ni mojawapo ya hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili......
SIKU YA SITA YA WAGENI
Siku ya sita walianza mapema kama siku ya nne kisha wakamueleza baba awapeleke msituni. Baba aliwapeleka msituni maeneo yenye tembo. Baba alikuwa na lengo lake, akiamini kuwa kama watauwa tembo atapewa kichwa hivyo atauza meno na kupata pesa nyingi sana. Lakini wale mabwana walisha tambua hili, mmoja wao akasema “wala usitende wema kwa kutarajia malipo kwa mema wako, bali taka malipo kwa Mwenyezi Mungu”. nafsi yangu ilinisuta sana ila sikujali sana nilitambua kuwa ni kawaida yao. Haya ni maneno aliyojisemea baba.
Basi baba akawapeleka kwenye msitu wenye tembo. Wale mabwana walikuwa wanatumia mikuki, michale na mmoja wao alikuwa na bunduki iliyotengenezwa India. Niliitambua kutokana na hati ya maandish yaliyoandikwa. Basi baba akawapeleka kwenye msitu wenye tembo na akawapeleka sehemu ambapo tembo huwa wanapenda kunywa maji. Wale watu wakakaa sawa kwa kujiandaa kuwinda, ngafla kundi la tembo likaja. Baba akaanza kufurahia moyoni akidhani sasa utajiri unafata. Kitu cha ajabu mmojawao akapiga bunduki juu ili kuwatisha tembo.
Wale tembo wakakimbia na kubakiwa vinyama vijidogo. Baba akapata hasira moyoni lakini mmoja wa wale watu akasema “wala usikodolee macho kitu kilichopo kwa mwenzio”. muda si mrefu mamba wakaanza kuja mmoja kati ya wale watu akachukuwa mkuki na kumnyatia mamba na akapiga kwa nguvu. Mamba alitapatapa sana lakini wakafanikiwa kumvua. Nilianza kuhoji maswali mengi hata nikadhani wanataka kula mamba. Haya ni maneno ambayo baba alikuwa akiwaza.
Wakamtoa mamba na kumuandaa vyema na kuotoa sumu yake na kuifukia. Walipomaliza wakamkata kichwa na kumpatia baba. Yule mzee sana akasema “mamba huyu amezoea kula kambare wakubwa wanaojificha kwenye matope. Kihifadhi kichwa hiki mpaka siku ya miadi”. baba anasema niliwaacha kulekule baada ya kuniambia kuwa njia wanaijuwa hivyo watarudi wenyewe. Baba hakujuwa yule mamba wamemfanya nini alipokuja kichwa chake akakiweka tena sehemu nzuri. Wageni wetu tuliwasubiri hata ikafika usiku wa manane bila kutokea.
Baba akaamuwa aende kuwafatilia huenda wamepotea. Aliwakuta palepale alipowaacha, na walipomuona walimshukuru sana na kumuombea dua kwa ukarimu wake na kwa kujali kwake wageni. Wageni wakamweleze kuwa watalala pale asubuhi ndio wataonana. Basi baba akarudi na ilipofika subuhi wageni wakamwita baba uwani kwetu na kumwambia ahakikishe milango amefunga na hakuna mtu atakayesikiliza mazungumzo yao.
Baba ananieleza kuwa wakamwambia alete vichwa vile vitatu na kuviweka mbele yao. Wakakipasua kichwa cha kambale na kukuta alimeza dini la dhahamu kubwa. Kumbe madini yalikuwa yakihuka kwenye yale maporomoko ya maji na kwa kuwa makambale wanajitafutia chakula kwenye matope kwa bahati mbaya kambale yule alimeza dini nile na likamkwama kwenye kichwa chake. Baba akaambiwa auze dini lile na ndio zawadi yeke.
Walachukuwa kichwa cha kunguru na kukipasua wakatoa mkufu wa dhahabu. Wakamwambia auze mkufu ule baada ya mwaka mmoja. Maana mkufu ule ulikuwa ni mali ya msafiri mmoja ambaye alishawahi kusaidia na baba. Na mkufu ule aliusahau sehemu ambayo alilala siku moja baada ya kuondoka nyumbani. Kunguru yule aliubeba mkufu ule na ukamkwama kwenye koo lake. Wakamwambia kama baada ya mwaka hajatokea mwenyewe uza na utumie thamani yake.
Wakachukuwa kichwa cha mamba na kukipasua wakakuta kuna matope mengi sana.katika matope yale kulikuwa na madini ya dhahabu kadhaa. Wakamkabidhi tena baba na kumwambia hii ndio zawadi yako kwetu. Kishha wageni wakakusanya kila kilichochao na kuendelea na safari yao. Hatukupatapo kujuwa hata majina yao, wapi wametoka na wapi wanakwenda. Baada ya muda wa mwaka baba aliuza mali zile na hapo ndipo utajiri wetu ulipoanzia.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:13:47 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 133
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
kitabu cha Simulizi
👉4
Madrasa kiganjani
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
Kitabu cha Afya
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 1: Hadithi ya chongo watatu, watoto wa mfalme na wanawake wa Baghdad.
Skmulizii hii pia imetoka kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 15: Hadithi ya safari ya Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 17: Siri ya wageni yafichuka
Muendelezo........ Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 13: Wageni wa Baraka kujongea
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 23: Kaka wa pili wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 10 Part 5: Safari ya kwenda nyumbani
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 11: Ndani mwa junba la Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 17: Hadithi ya Malipo ya wema ni wema
Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 20: Kinyozi maishani mwangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...