Kisa cha Malkia wa Sabaa.
Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen.
Kisa cha Malkia wa Sabaa.
Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Watafiti wa mambo ya historia na geografia wanasema Sabaa ilikuwa kiasi cha umbali wa maili hamsini kutoka mji wa Sanaa. Watu wa Sabaa walikuwa wakiabudu Jua na walimfanya mtawala wao kuwa ni mwanamke - malikia.
Pamoja na ushirikina wao, Allah(s.w) aliwaneemesha watu wa Sabaa kwa kila kitu walichohitajia katika maisha yao. Nabii Sulaiman aliwafahamu watu wa Sabaa kupitia kwa ndege Hud-Hudi kama aya zifuatazo zinavyobainisha:
"Na akawakagua ndege (na usimuone kidege Hud-Hud) akasema: "Imekuwaje mbona simuoni Hud-Hudi, au amekuwa miongoni mwa wasiokuwepo (hapa leo)". "Kwa yakini nitamuadhibu adhabu kali au nitamchinja au ataniletea hoja iliyo wazi (ya kumzuilia kuja hapa leo)." "Basi hakukaa sana mara (Hud-Hudi akafika) akasema (kumwambia Nabii Suleiman) Nemegundua usilogundua, na ninakujia hivi kutoka (nchi inayoitwa) Sabaa na (nakuletea) habari yenye yakini"."Hakika nimekuta mwanake anawatawalia; naye amepewa kila kitu na anacho kiti cha enzi kubwa"."Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia (ya kheri), kwa hivyo hawakuongoka" (27:20-24).
Baada ya taarifa hizo Nabii Sulaiman alituma ujumbe kumnasihi malkia aingie katika Uislamu. Awali malkia baada ya kushauriana na mawaziri wake aliona apoteze lengo la Sulaiman kwa kumpa zawadi. Lakini lengo la Mitume ni kufikisha ujumbe wa Allah si kuchuma. Kwa hiyo Nabii Sulaiman alimrejeshea zawadi zake na akaendeleza harakati za kumvuta malkia katika haki mpaka akasilimu. Habari hizi zimebainishwa kwa urefu katika aya Qurβan(
27:27-44).
Jambo tunalotakiwa tulizingatie hapa ni ule msimamo thabiti wa Nabii Sulaiman katika kazi ya kuwalingania watu. Mara nyingi watawala hulewa tamaa ya kujilimbikizia madaraka na mali wakasahau wajibu wao mbele ya Muumba wao. Malkia wa Sabaa alidhani kwa kutumia mali angemtoa Nabii Sulaiman kwenye lengo lake. Lakini haikuwa hivyo.
Hali hiyo si kwa viongozi tu na wakuu wa nchi, bali hata sisi tulio katika harakati za Da'awah tuwe makini tusitolewe kwenye lengo kwa hongo ya mali au wadhifa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitau cha Fiqh π2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π3 web hosting π4 kitabu cha Simulizi π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara.
Soma Zaidi...Historia ya bi Khadija na familia yake na chanzo cha utajiri wake.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake.
Soma Zaidi...Kusingiziwa Nabii Sulaiman Uchawi
Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu.
Soma Zaidi...Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo
Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.
Soma Zaidi...