Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali
Khabari za kutekwa Basra zilimchukua kwa mshangao mkubwa Khalifa Ali ambaye alikuwa aende Syria kumrudi Muawiya lakini alilazimika kwenda Basra kwanza kutuliza hali ya kule.
Alipofika Dhi-Qar’a mahali karibu na Basra-alituma ujumbe kwa Aisha, Talha na Zubeir wafanye mazungumzo ya amani. Nafasi ilipatikana mazungumzo yakafanywa na wakawa karibu kukubaliana baada ya Ali kuahidi kuwa atawaadhibu wauwaji wa Uthman Dola itakapokuwa na amani. Lakini mpango wa amani haukuwa na maslahi kwa lile kundi la Ibn Sabaa ambalo lilifanya sehemu ya jeshi la Ali.
Walinong’onezana kuwa Ali anataka kufikia makubaliano ya amani na ameahidi kuwaadhibu waliomuua Uthman. Kundi hili lilikuwa ndilo lililomuua Khalifa Uthman halikupendezwa na mpango huu, wakaunda hila iliyochochea kutokea vita. Mbinu mbili walizitumia. Kwanza walipeleka umbea Basra kuwa Ali akiingia Basra atawafanya watumwa wakazi wote na atawaua vijana wote. Kwa sababu hii watu wa Basra lazima wapigane.66 Ibn Sabaa na wachochezi wake usiku usiku walivamia jeshi la mama Aisha ambaye aliarifiwa na kwa namna hii vita vikaanza. Vita hivi vinajulikana kwa jina la Vita vya ngamia.
Vita vilikuwa vikali kwa vile ukubwa wa jeshi ulilingana. Baada ya mapigano makali na kuuawa Waislamu wapatao elfu kumi, Talha aliuwawa na , Zubair aliacha kupigana na akawa anaelekea Madina ndipo akauliwa njiani. Wakati wote wa vita mama Aisha alikuwa katika sehemu ya uwanja wa vita akiwa amepanda ngamia. Kuwepo kwake kulifanya mapigano yaendelee kwa kasi kubwa, bila kukoma, ndipo Ali alipoamuru ngamia wake akatwe miguu ya nyuma. Ngamia aliangukia miguu yake ya mbele na kwa heshima zote akatolewa mama Aisha ndani ya kikalio cha ngamia na vita vikaisha. Mama Aisha akasindikizwa Madinah na kaka yake Muhammad bin Abubakar.
Baada ya vita, Ali alizungumza na Waislamu katika msikiti wa Basra na Waislamu wakampa mkono wa utii. Alipoondoka alimuacha Abdallah bin Abbas kuwa Gavana wa Basra.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 709
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Madrasa kiganjani
Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...
Mbinu Alizozitumia Nabii Shu’ayb(a.s) Katika Kufikisha Ujumbe Wake
Soma Zaidi...
Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine katika dola ya kiislamu
Soma Zaidi...
Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s. Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...
Wapinzani wa Ujumbe wa Hud(a.s)
Waliomuamini Mtume Hud(a. Soma Zaidi...
Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?
Mwenyezi Mungu si kiumbe. Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Adam(a.s)
(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s. Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa
Kuanzishwa kwa Polisi. Soma Zaidi...
Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Historia ya vita vya Muta
hii ni historia ya vita vya Muta. Katika makala hii utajifunza sababu ya vita hivi na yaliyojiri katika uwanja wa vita. Soma Zaidi...
Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake
Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a. Soma Zaidi...