Malipo ya wema ni wema

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

MALIPO YA WEMA NI WEMA

Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Hapa Zubeida akawa anajiulia kuwa ni nani huyu anakuja? Aua ni yule mchumba wake? Maswali haya hayakupata amjibu. Baada ya muda kupita akatokea binti mmoja mreembi kama mwezi uliokamilika umbo lake. Binti yule akamsogelea Zubeidah na kupiga goti mbele yake na kuukamata mkono wa Zubeidah na kuubusu kisha akamwambia “ NI YAPI MALIPO YA WEMA? KWA HAKIKA NI WEMA TU”.

 

Lilikuwa ni swali ambalo halihitaji majibu kutoka kwa Zubeidah. Kwa malipo ya wema ni wema, Zubeida akamuuliza “ni nani wewe ni ni nani mimi na nimefuka vipi hapa?. Yule mrembo akaanza kutoa kisa chake. Kuwa yenye ni mtoto wa mkuu mfalme wa majini ambaye alionana naye hapo mwanzo. Alipokiuwa matembezima jana akiwa amejibadili katika umbo la nge alipokuwa nakimbizwa na adui wake aliyekuwa katika umbo la kunguru alimsaidia kwa kumuuwa adui wake kunguru. Hivyo yule nge alikuwa ni huyu mtoto wa mfalme. Kwa ufupo ni kuwa Zubeidah amemuokoa mtoto wa mfalme katika kizingiti za kifo kuuliwa na adui wake na huu ni wema mabao analipwa.

 

Basi yule mrembo akamwambia Zubeida kuwa ndugu zako walipokutumbukiza baharini nilikuwepo kwenye jahazi lenu kwa nia ya kuku;inda mpaka ufikapo kwenu. Hivyo nilikuokoa kwenuye ajali ile na sikuweza kumuokoa mchumba wako, kwa hilo naomba unisamehe sana. Hata hivyo baba yangu anaweza kukupa chochote utakacho kiseme utapata, na hata ukitaka utaishi hapa na mimi. Ila kuhusu ndugu zako kwa hakika sitaweza kuwasamehe katu. Nitawapa adhabu kubwa sana nai ningewauwa ila kwa kuhofia chozi lako siwezi kufanya hivyo.

 

Basi Zubeidah akaitwa na mfalem wa majini yule na kuulizwa nini ameamua kati ya yale aloelezwa na binti mafalme. Zubeidah akachagua kurudishwa nyumbani kwao na hakuhitajia chochote. Basi binti mafalme akampa unywele wake na kumwambia ukiwa na shida na mimi choma nywele hii kwa hakika nitakuja hapo kwa haraka zaidi. Basi kufumba na kufumbua Zubeidah akajikuta yupo nyumbani kwake na mlangoni wamekaa mbwa wawili na kuangalia pembeni akakuta bahasha ambayo imewekwa mlangoni. Kufungua bahasha ile akakuta ndani kuna barua iloandikawa “Kutoka kwa Binti Mfalme wa majini ya majini na Nchi kavu kwenda kwa Zubeidah mwana wa tajiri mpotea njia mwenye kusalitiwa. Ama baada ya salamu napenda kukutaarifu kuwa hao mbwa unaowaona mlangoni kwako ni ndugu zako na hiyo ndio adhabu niloichagua. Watabaki hivyo kwa muda wa miaka 10 na utakuwa ukiwapiga fimbo za mijeledi 300 kwa kila mmoja na kila siku. Na kama hautafanya hivyo watakufa siku inayofata. Ama kuhusu mali zako zote nimeziokowa na zipo stoo. Hata hivyo baba yangu amekujengea nyumba karibu jirani na mji wa Mfalme mwadilifu Harun Rashidi mfalme wa Baghdah. Huko uende na ukakae na ndugu zako hao. Usisahau kufanya nilichokwambia Zubeidah.”

 

Hivyo Zubeidah akachukuwa mali zake na kuhamia katika nyumba ile aloambiwa mjini Baghdad na ndugu zake. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mbwa wakawa wanatoa machozi mengi sana na hata mfalme akawa anatoa machozi. Hivyo hii ndi sababu ya mimi kuwaadhibu mbwa hawa kila siku yalikuwa ni maneno ya Zubeidah. Mfalme baada ya kusikiliza hadithi hii akamgeukia Amina aliyekuwa na alama na makovu kwenye mwili wake na mumwambia aeleze hadithi yake, nae akaanza kama ifuatavyo;-

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1457

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Hadithi ya kisiwa cha mawe yanayolia

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Kutokana nyani mpaka kuwa chongo

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Binti wa ndotoni

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
KISIWA CHA UOKOZE CHA PILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nilikwenda mpaka nikakuta misitu minene na nisijuwe pa kuenda.

Soma Zaidi...
Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Kisa Cha mfugaji na mkewe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
SAFARI YA PILI YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA PILI YA SINBAD Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi.

Soma Zaidi...
KUELEKEA BONDE LA UOKOZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUELEKEA BONDE LA UOKOZI Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha hadithi ya Chongo

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...