Navigation Menu



image

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE

FAMILIA YA MTUME (S.

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE


FAMILIA YA MTUME (S.A.W)
Mtume ametokana katika ukoo wa Ibn Hashimu. Na ukoo huu umeitwa kwa jina hili kutokana na kurithi jina hili kutoka kwa mzee wao Hashim Ibn Abd Manaf. Hapa tutaona kwa ufupi.

1. Hashim:
Huyu alikuwa ni katika wazee wanaoheshimika sana katika kabila la kikuraishi Maka enzi hizo. Pia ndie ambaye alikuwa na jukumu la kuwapa chakula na maji mahujaji wote. Mzee huyu alitambulika pia kwa kuwa tajiri na mtu mkweli na muwazi. Pia alijulikana kuwa ndiye mzee wa kwanza kuwalisha mahujaji mkate uliochanganywa na mhuzi.

Jina lake halisi ni Amr na ameitwa Hashim kutokana na kitendo chake cha kutengeneza mikate kwa mahujaji. Pia ndie ambaye alianzisha safari mbili za makuraishi wakatika wa kipupwe na kiangazi jerea Quran suat Quraysh. Pia imeripotiwa kuwa aliwahi kwenda Syria kama mfanya biashara. Alipokuwa Madina alimuoa Salma mtoto wa Amr kutoka kabila la Bani ‘Adi bin An-Najjar. Alikaa pamoja na mkewake Madina kwa muda kisha akaelekea tena Syria wakati ho alimwacha mkewe akiwa ana ujauzito.

Mzee Hashim alikfariki 497 B.K nchini Palestina katika mji uitwao Ghazza. Bada ya kifo cha mzee huyu mke wake alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa ‘Abdul-Muttalib na lilijulikana kwa jina la utani kama Shaiba. Alipewa jina hili kwa sababu alizaliwa akiwa na nywele nyeupa yaani mvi kwenye kichwa chake. Mke wake alimchukuwa Mtoto ‘Abdul-Muttalib na kumpeleka kwenye nyumba ya baba yake Madina. Kuzaliwa kwa kijana ‘Abdu-Muttalib hakukujulikana na yeyote katika familia ya Hashim.

Hashim alikufa akiwa na watoto wanne; Asad, Abu Saifi, Nadla na ‘Abdul-Muttalib. Pia alikuwa na watoto wakike watano ambao ni; Ash-Shifa, Khalida, Da’ifa, Ruqyah na Jannah.

2. Abdul-Muttalib:
Baada ya kifo cha Hashim, kazi ya kulisha mahujaji alipewa ndugu yake Al-Muttalib bin ‘Abd Munaf ambaye alifahamika kwa kuwa na sifa ya ukarim, uwazi na ukweli. Sasa wakati ambao ‘Abdul-Muttalib alipofikia umri wa ujana mzee Al-Muttalib alizipata habari juu ya kuwepo kwa mtoto wa kaka yake Hashimu huko Madina. Hivyo akafunga safari ili akamchukuwe mtoto wa ndugu yake. Basi pindi alipomuona tu machozi yalimtoka na kudondoka kupitia kwenye mashavu yake. Alimkumbatia na kumpandisha kwenye ngamia wake. Lakini kijana alikataa kwenda madina mpaka apate ruhusa kutoka kwa mama yake.

Basi mzee Al-Mutalib akaenda kwa mama yake kijana na kuomba aruhusiwe aondoke nae kuelekea Makkah. Lakini mama nae akakataa kumruhusu kijana wake kuondoka. Lakini mzee Al-Muttalib akatumia maneno ya ushawishi kwa kumwambia kuwa “mtoto wako anakwenda Makka kushika madaraka ya baba yake pia kwa ajili ya kuitumikia Al-kaba (nyumba tukufu ya Allah). Kwa maneno haya mama alikubali kumruhusu mwanae.

Zee al-Muttalib alipofika Makka na kijana wake watu wakadhani kuwa yule ni mtumwa wake, lakini akawaambia kuwa “huyu ni mwanangu, ni mtoto wa kaka yangu Hashim” Kijana Abdul-Muttalib akapelekwa nyumbani kwa baba yake mzee Al-Muttalib, na aliishi pale mpaka mzee Al-Muttalib alipofariki katika sehemu iitwayo Bardman huko Yemen, basi hapo madaraka yote alipewa Abdul-Muttalib. Alifahamika kwa utawala wake ulio mzuri na upendo kwa watu wa Makkah. Alikuwa ndiye kiongozi katika mambo ya kusimamia Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba.

1. Wakati mzee Al-Muttalib alipofariki, Nawfal alichukuwa madaraka kimaguvu kutoka kwa Abdul-Muttalib. Hivyo Abdul-Muttalib akaomba msaada kwa maquraish wakakataa kumsaidia, akaamuwa aombe msaada kwa mjomba wake Abu Sa‘d bin ‘Adi kutoka katika kabila la Bani A-Najjar ambaye alikubali kumsaidia hivyo akaja maka akiwa na wanajeshi wapanda farasi 80. Alipofika akaenda kwa Nawfal na akawashuhudishia wazee wa kiqurayshi kuwa kama Nawfal hatarudisha madaraka kwa mpwa wake basi atamkata kwa upanga. Baada ya hapo akaenda nyumbani kwa mpwa wake na akakaa hapo kwa muda wa siu tatu. Alifanya ibada ya Umrah kisha akarudi Madinah.

Baadae Nawfal akaingia makubaliano ya kusaidiana kati ya ukoo wake na ukoo wa Bani ‘Abd Shams bin ‘Abd Munaf, makubaliano ya kusaidiana dhidi ya kuwapinga bani Hashim (yaani ukoo wa Abdul-Muttalib). Wakati kabila la Khuzaa lilipoona ukoo wa Bani An-Najjar wanawasaidia bani Hashim nao wakaingia makubaliano na ukoo wa Bani Hashim dhidi ya kumpinga Nawfal na Kundi lake. Kaika wakati wa utawala wa mzee Abdul-Muttalib alishuhudia matukio makuu mawili ambayo ni kuchimbwa kisima cha zamzam pamoja na kuangamizwa kwa jeshi la tembo.

Kwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Basi akachimba na ndipo akakuta chini ya kisima vitu ambavyo vilifukiwa pamoja na kisima. Walofukia vitu hivi ni watu kutoka kabila la Jurhum. Hawa pindi walipolazimika kuondoka Maka walikifukia kisima cha zamzam na kufukia baadhi ya vitu vya thamani kama mapanga, nguo za vita, na dhahabu. Baada ya hapo mlango wa alka’aba ukatengenezwa kwa hii dhahabu waloipata. Na unyweshwaji wa maji ya zamzam kwa mahujaji ukarudi upya.

Basi kisima cha zamzam kilipoanza kutoa maji, watu kutoka kabila la quraysh walitaka kufanya makubaliano juu ya maji yale lakini Abdul Al-Muttalib alikataa kwa kudai kuwa Allah amempa mamlaka yeye tu. Basi wakakubaliana wakamuulize kuhani kutoka ukoo wa Bani Sa’ad juu ya swala hili. Basi Allah akawaonesha alama za ukweli juu ya madai ya Abdul Al-Muttalib. Baada ya hapo mzee Abdul Al-Muttalib kwa shukran yake kwa Allah akaapa kumtoa kafara mtoto wake kwa Mwenyezi Mungu.

Tukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka’aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)

Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.

Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San’a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.

Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.

Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo.

Mzee Abdul Al-Muttalib alikuwa na watoto wa kiume kumi ambao ni Al-Harith, Az-Zubair, Abu Talib, ‘Abdullah, Hamzah, Abu Lahab, Ghidaq, Maqwam, Safar na Al-‘Abbas. Pia alikuwa na watoto wa kike sita ambao ni Umm Al-Hakim, Barrah, ‘Atikah, Safiya, Arwa NA Umaima.

3. Abdallah: huyu ndiye baba wa Mtume Muhammad (s.a.w). mama yake aliitwa Fatimah mtoto wa ‘Amr bin ‘A’idh bin Imran bin Makhzum bin Yaqdha bin Murra. Abdallah alikuwa ndiye mtoto mtanashati zaidi kuliko watoto wote wa mzee Abdul-Muttalib alikuwa mcheshi zaidi na alipendwa zaidi kuliko watoto wote wa Mzee Abdul-Al-Muttalib.na huyu ndiye mtoto ambaye mishale ya kafara ya ahadi aloiweka mzee Abdul al-Muttalib ilimuangukia.

Pindi watoto wake mzee Abdul al-Muttalib walipofikia balehe aliwaita na kuwaambia kiapo cha siri alichokiweka juu wa kutoa kafara ya mtoto wake kwa mungu wao Hubal. Basi majina ya watoto yakaandikwa kwenye mishale ya kuangalizia utabiri na jina la Abdallah ndilo likatokelezea kuwa ndie aliyechagulia kutolewa kafara. Kwa kuwa huyu ndiye Mtoto anayependwa zaidi na mzee Abdul al-Muttalib hivyo akashauriwa kubadilisha na ngamia. Baada ya kuangalizi ni ngamia wangapi wanafaa ngamia miamoja ndio wakaonekana wanafaha badala ya kuchinjwa kwa Abdallah. Mtume (s.a.w) alikuwa akisema “mimi ni mtoto wa wachinjwa wawili” yaani ismail mtoto wa Mtume Ibrahimu na Abdallah mtoto wa Abdul al-Muttalib.

Addallah alifariki baada ya mke wake kupata uja uzito kwa muda wa miezi miwili. Wanazuoni wa historia wanatueleza kuwa alifariki akiwa na umri wa miaka 18 na hakuacha chochote katika urithi. Abdallah alifariki Madina alipokuwa anarudi kutoka kwenye safari za kibiashara kutokea Sham baada ya kupatwa na ugonjwa wa ghafla na alizikwa Madina upande wa ujombani kwake.


                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1517


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA MAISHA YA UTOTONI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)
MAISHA YA UTOTONI YA MTUME S. Soma Zaidi...

Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)
8. Soma Zaidi...

Matukio mbalimbali katika historia ya uislamu kabla na baada ya Mtume (s.a.w) na makhalifa wake wanne
1. Soma Zaidi...

Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo
Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kumlingania Uislamu Baba Yake
Baada ya NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...

Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam
Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Soma Zaidi...

Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU
Soma Zaidi...

Imam Muslim na Sahihul Mslim
Soma Zaidi...

tarekh 10
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa mahakama na mahakama ya Kadhi wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Katika Mji wa Taif
Baada tu ya Mtume(s. Soma Zaidi...