Vita vya Badri.
Vita vya Badri.
- Vilikuwa ndio vita vya kwanza vya jihad vilivyopiganwa siku ya Ijumaa mwezi 17 Ramadhani, mwaka wa 2 A.H (624 A.D) katika bonde la Badri.
- Chanzo cha vita ni kuwa mtume (s.a.w) alikusudia kuuzuia msafara wa Maquraish wa Makkah uliotokea Syria (Sham) uliosheheni bidhaa zenye thamani ya dinar 50,000 kwa ajili ya maandalizi ya kuupiga vita Uislamu na Waislamu.
- Mtume (s.a.w) alikuwa na askari 313, ngamia 70 na farasi 2 tu na Makafiri wa Kiquraish wakiwa askari 1000 waliojizatiti kivita, ngamia 700 na farasi 300.
- Waislamu walipata ushindi kwa waliuawa Maqurish 70 wengi wao wakiwa vigogo wa Makkah na waislamu 14 tu waliuawa.
Rejea Qur’an (3:123-124), (8:9-11), (54:45), (8:65), (8:17) na (8:48).
Mafunzo kutokana na Vita vya Badri.
1.Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.
Rejea Qur’an (3:123-124), (8:42-45).
2.Tunajifunza pia namna ya kuwafanyia mateka wa kivita ikiwa ni pamoja na;
- Kuwapatia haki na huduma zote msingi za kimaisha, kibinaadamu na kiutu.
- Kuwalea na kuwafanyia wema na uadilifu kama wanafamilia wengine.
- Kwa mateka wanaoweza kuleta madhara kwa waislamu na Uislamu, ni bora
kuuawa badala ya kuachwa huru kwa kujikomboa.
Rejea Qur’an (8:67-69).
3.Mwenyezi Mungu (s.w) aliwaadhibu makafiri na kuwanusuru waislamu katika vita vya Badri na hawakuadhibu walipokuwa Makkah kwa sababu walikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) na pia walipewa muda wa kutubia.
Rejea Qur’an (8:32-34) na (8:19).
4.Tunajifunza pia, inafaa nguvu ya kivita kutumika ikibidi katika kuzuia na kuondoa uovu, udhalimu, uonevu na choko choko za maadui.
Rejea Qur’an (8:60) na (60:8-9).
5.Tunajifunza pia, Uislamu bila ya juhudi za kweli kufanyika na kumwagika damu na kujitoa muhanga ipasavyo, hautasimama katika jamii.
6.Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma.
Soma Zaidi...Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B.
Soma Zaidi...Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam.
Soma Zaidi...KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
Soma Zaidi...