Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula tango
Tango (coccumber).
Tango ni katika mimea jamii ya matikiti na maboga. Tango ni katika matunda ambayo unatakiwa uyale sana kwenye maisha yako. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 95 ya tango ni maji. Tango lina vitamin K, B vitamins, copper, potassium, vitamin C, na madini ya manganese.
Tango lina anti-inflammatory flavonol ambayo huitwa fisetin. Hii husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo. Hii husaidia katika kutunza kumbukumbu na kuimarisha afya ya mfumo wa fahamu pamoja na neva.
Tafiti zinaonesha kuwa tango lina polyphenols ambazo huitwa lignans (pinoresinol, lariciresinol, and secoisolariciresinol), husaidia katika kuzuia kupata aina mbalimbali za saratani (cancer) kama saratani ya kizazi kwa wanaume na wanawake.
Tango pia lina antioxidant flavonoids, kamavile quercetin, apigenin, luteolin, na kaempferol, ambazo husaidia katika kupambana na maradhi kama saratani na maradhi mengineyo.
Tango hupunguza joto tumboni, pia huondoa bajteria wanaoleta harufu mbaya mdomoni. Tafiti zinathibitisha kuwa tango husaidia katika kuondoa misongo ya mawazo na hii ni kutokana na uwepo wa vitamin B1, vitamin B5, and vitamin B7 (biotin) kwenye tango.
Tango huimarisha afya ya moyo na kupumguza shinikuizo la damu. Tanago husaidia mfumo wa kumeng’enya chakula ufanye kazi kwa ufanisi. Tango husaidia katika kuthibiti uzito wa mwili
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tikiti
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mapema, kwa sababu ya kuwepo kwa saratani ya matiti, kuna dalili ambazo zikijitokeza zinapaswa kutolewa taarifa mara moja bila kuchelewa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukutajia sababau kuu 10 ambazo zinaonyesha umuhimu wa kula matunda kiafya. kwa nini kiafya unashauriwa ule matunda na mboga mara kwa mara?
Soma Zaidi...