Navigation Menu



image

Hizi ndizo aina tatu za Hija

Hizi ndizo aina tatu za Hija

Aina za Hija



Kuna aina tatu za Hija ambazo kila mwenye kuhiji ana uhuru wa kuchagua mojawapo kulingana na uwezo wake wa kukidhi masharti ya kila aina. Aina hizi ni
(i) Ifraad,
(ii) Qiran na
(iii) Tamattu kama zinavyoelezewa katika hadith ifuatayo:



Amesimulia Aysha (r.a): “Tulitoka na Mtume wa Allah (s.a.w) (kwenda Makka) katika Hija ya Mtume ya kuaga. Miongoni mwetu tulivaa Ihram kw a n ia y a kufany a `Umra tu (al-Tama ttu) w engine kw a Hija n a `Umra pamoja (al-Qiran) na kw a w engine kw a Hija tu (al-Ifraad). Mtume w a Allah (s.a.w) alivaa Ihram kwa nia ya Hija tu. Kwa hiyo kwa yule aliye vaa Ihram kwa Hija tu au kwa Hija na `Umra pamoja, hakutoka katika Ihram mpaka siku ya kuchinja (kutoa muhanga yaani siku ya mwezi 10 Dhul-Hija). (Bukhari).



(i)Ifraad: Ni aina ya Hija ambapo, “Hajj” anavaa Ihram kwa nia ya kufanya Hija tu bila ya “Umra” na ataanza kuitikia mwito wa Allah (s.a.w ) kwa:(Labbaika lhajji ) yaani “Nimeitika kwa Hija.” Hajj hatavua Ihram yake mpaka amalize matendo yote ya Hija yanayomlazimu kuwa katika Ihram. Haji huruhusiwa kuvua Ihram na kutoka kwenye masharti yake baada ya kutupa mawe kwenye mnara na kunyoa au kupunguza nywele siku ya mwezi 10 Dhul-Hija. Kwa yule aliyechagua aina hii ya Hija halazimiki kuchinja siku ya mwezi 10 Dhul-Hija.



(ii)Qiran: Ni aina ya Hija ambapo Haji huvaa Ihram kwa nia ya kufanya Hija na ‘Umra pamoja na katika talbiya ataanza kutikia mwito wa Allah kwa: (labbaika lhaji wa Umra) - yaani “Nimeitika kwa Hija na ‘Umra’.Hajj katika aina hii ya Hija hatavua Ihram mpaka baada ya kuchinja na kufanya Tawaful-Ifadha (tawafu ya nguzo) siku ya mwezi 10 Dhul-Hija.



Aina hii ya Hija inafanywa na wale wanaokuja Makka na wanyama. Katika Hija yake ya kuaga, baada ya kumaliza ibada ya ‘Umra, Mtume (s.a.w) aliwaamrisha watu wote wavue Ihra m ila kw a w ale w a liokuja n a w any ama.


(iii) Tamattu: Katika aina hii ya Hija, Haji anapofika katika Miiqaat yake huvaa Ihram kwa nia ya kufanya ‘Umra tu na ataitikia mwito wa (Labbaika liumra) - yaani “Naitikia kwa ‘Umra’. Baada ya kumaliza ‘Umra atanyoa au kupunguza nywele na kuvua Ihram na kuwa huru na miiko yote ya Ihram. Atavaa tena Ihram kwa nia ya Hija mnamo mwezi 8 Dhul-Hija, na atabakia na Ihram mpaka amalize Hija ya mwezi 10 Dhul-Hija kama ilivyo katika aina nyingine za Hija. Haji analazimika kuchinja siku ya mwezi 10 Dhul-hija.



Katika aina hizi tatu za Hija, At-Tamattu ndio aina bora zaidi na yenye nafuu kubwa kwa wale wanaotoka mbali wasioweza kuja na wanyama, ama kwa wakazi wa Makka au majirani wa Makka ambao wana uwezo wa kwenda na wanyama, Hija iliyo bora kwao ni hii ya Al-Qiran. Lakini wenye kuhiji Hija ya Tamattu wanalazimika kununua mnyama na kumchinja siku ya mwezi 10 Dhul-Hija kama tunavyofahamishwa katika Qur’an:


“... Na mtakapokuwa kwenye salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya `Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliyesahilika (mbuzi au kondoo).Na asiyepata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba atakaporudi (kw ake); hizi ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na msikiti Mtakatifu wa Makka. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. ” (2:196).




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 576


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee
1. Soma Zaidi...

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Sifa za mchumba
Soma Zaidi...

Taratibu za kufunga ndoa na kumuinglia mke
Soma Zaidi...

Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa
Soma Zaidi...

nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji
2. Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA
Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMAN
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Muda wa kuhiji na mwenendo wa mwenye kuhiji
Soma Zaidi...