image

SAMAKI AINA YA SALMON

2.

SAMAKI AINA YA SALMON

2.SAMAKI AINA YA SALMON.

beroar Huyu ni samaki aliye maarufu sana diniani. Ukiachana mbali na kuwa na minofu pia mafuta ya samaki huyu ni mujarabu katika kulinda afya ya mwili dhidi ya maradhi pamoja na kusaidia ukuaji mzuri wa mwili na akili hususan kwa watoto wadogo.

Samaki huyu anapatikana sana kwenye mito iliyopo Amerca ya Kaskazini (North Amerca) samaki hawa maarufu wanapatikana kwa wingi sana. Miongoni mwa maajabu ya samaki hawa ni safari yao ndefu ya kutembea kutoka mto ni kwenye baharini na kurejea tena walipo toka baada ya kukaa muda mrefu wakiwa baharini.

Samaki huyu anasifa ya kuishi kwenye maji baridi na maji ya chumvi. Maisha ya samaki hawa yanaanzia pale samaki jike anapotaga mayai maeneo ya juu ya mto amapo kuna maji yabaridi (yasiyo na chumvi). Baada ya kutotolewa kwa samaki hawa wanakaa mtoni hapa kwa muda kadhaa.baada ya kwisha kuuwa kiasi cha kuweza kujitafutia chakula wenyewe na kuweza kujilinda hapa wanaanza safari yao ya maajabusana.

pic Salmon baada ya kukuwa na kukomaa anaanza kusogea karibu na bahari, na hapa mabadiliko huanza kutokea kwenye mwili wake ili kuweza kumfanya aishi kwenye maji ya chumvi. Baada ya kuweza kuendana na mazingira ya maji ya chumvi na hali ya hewa salmon wanaanza safari yao ya kuelekea baharini ambapo watakaa kwa muda mrefu sana.

Safari ya samaki hawa inaweza kuwa na urefu kuanzia kilomita 1600 mpaka kilomita 4000 inategemea aina ya samaki hawa. Inakadiriwa kuwa wakati wa safari yao samaki hawa huweza kutembea kwa umbali wa kilomita 6 mpaka 7 kwa siku. Baada ya kizazi hiki kuhamia baharini na kukaa kwa muda wa miaka kadhaa, samaki hawa wanapotaka kutaga na ili kuendeleza kizazi wanarudi kule walipozaliwa yaani mtoni. Na hapa safari ya kurudi iliyo na maajabu ndipo huanzia.

Itambulike kuwa samaki hawa wanatakiwa kurudi pale walipozaliwa na haijalishi ni muda gani toka waondoke lakini lazima watafika. Pia kwa kuwa maji ya mto yanaelekea baharini na samaki hawa wanarudi mtoni walipozaliwa basi safari yao itakuwa inapingana na maji ya mtu. Hivyo itawalazimu kukinzana na nguvu ya maji ya mtu na wakati mwingine wanapokutana kwenye maporimoko ya maji wanatakiwa waruke. Safari hii imejawa uvumilivu kwani kuna wanyama walao samaki huwa wanawasubiria maeneo haya yenye maporomoko pindi wanaporuka wawale. Samaki hawa wanaweza kuruka maporomoko yenye urefu unaokadiriwa kufikia mita 3. Pia Salmon anaweza kukutana na sehemu ya mto ambayo ina maji kidogo aya pamekauka, samaki huyu anaamuwa kuruka ili ayapate maji ama atasubiria mpaka maji yaingie aendelee na safari yake.

pic Wataalamu wanatueleza kuwa mnyama huyu aaweza kupajuwa mtoni alipo zaliwa kwa kutumia harufu ya maji. Inaelezwa kuwa samaki hawa wanaweza kutofautisha harufu za maji hata kwa kiwango kidogo sana. Samaki huyu pindi anapozaliwa kule mtoni harufu na maji ya eeo alipozaliwa anakuwa na kumbukumbu nayo bila ya kujali amekaa baharini kwa muda gani.

Salmon baada ya safari ndefu na iliyo ngumu anarudi mtoni ambapo amezaliwa. Salmon akiwa kwenye safari yake mwili wake hufanya babadiliko ambauo yatamfanya aweze kuishi kwenye maji ya baridi. Hii ni tofauti na samaki wengine ambao ukimtoa maji ya baridi papo kwa papo na ukamtia maji ya chumvi hufa. Salmon ana uwezo wa kuishi mazingira yote haya.

Baada ya kuwasili mtoni pale walipozaliwa samaki hawa wanataga mayai na kuyatotowa. Makinda yanapototolewa yanakuwa hayana uwezo wa kujilinda hivyo wanajificha kwenye mawe, baada ya wiki kupita hatimaye samaki hawa wanaweza kujitaftia chakula wenyewe safari hii huanza tena. Na haya ndio maisha ya samaki huyu salmon.

Nani kamfundisha samaki huyu kuweza kujuwa mazingira na maeneo alozaliwa, na kuweza kurudi bila ya kukosea. Kwa nini samaki huyu anatembea safari hii iliyo na ugumu na uvumilivu?. Salmon ni samaki ambaye anatupatia mafunzo mengi sana. Kwa mfano sikuzote kabiliana na changamoto kwani kukimbia zio njia sahihi ya kutatua tatua tatizo. Salmon anaenelea na safari yake bila ya kujali nguvu ya maji ya mto kuwa itamrudisha baharini, au maadua walao samaki ama maporomoko ambayo hataweza kuyaruka.


                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 475


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

MAAJABU YA MBU
7. Soma Zaidi...

Promo
Kama wewe ni Muandishi mzuri za hadithi au makala za kutoa elimu kwa watu na unataka kazi yako iwafikie watu wengi, au unataka kazi yako iweze kukuingizia kipato, Bongoclass ndio mtatuzi wako sasa. Soma Zaidi...

Promo
Kama wewe ni Muandishi mzuri za hadithi au makala za kutoa elimu kwa watu na unataka kazi yako iwafikie watu wengi, au unataka kazi yako iweze kukuingizia kipato, Bongoclass ndio mtatuzi wako sasa. Soma Zaidi...

Mbu (mosquito)
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mdudu mbu Soma Zaidi...

Tembo
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama tembo Soma Zaidi...

nataka niunganishe namba yangu kwa mtu mwingne ili kama kuna sms nimetumiwa ianzie kwa huyo mtu
Ikiwa nataka niunganishe namb yangu kwa mtu mwingne il kama kuna sms nime2miwa ianzie kwa huyo mtu nifanyeje? Soma Zaidi...

MAAJABU NA UWEZO WA CHEETAH
5. Soma Zaidi...

WELCOME TO OUR LIBRARY
Karibu sana Kwenye Maktaba Yetu Sasa umefika kwenye maktaba ya vitabu. Soma Zaidi...

MAKTABA YA VITABU
Soma Zaidi...

Buibui hupuruka ijapokuwa hana mbawa.
Nataka nikufundishe moja katika maajabu ya mdudu Buibui kwa lugha ya kimombo spider. Soma Zaidi...

FreeFind.com
Soma Zaidi...

More
Bila shaka umefurahishwa na huduma zetu, Je unataka huduma zaidi, Bofya kityfe cha Open hapo chini. Soma Zaidi...