Samaki aina ya salmon

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sifa za samaki aina ya salmon

.SAMAKI AINA YA SALMON.

 

beroarHuyu ni samaki aliye maarufu sana diniani. Ukiachana mbali na kuwa na minofu pia mafuta ya samaki huyu ni mujarabu katika kulinda afya ya mwili dhidi ya maradhi pamoja na kusaidia ukuaji mzuri wa mwili na akili hususan kwa watoto wadogo.

 

Samaki huyu anapatikana sana kwenye mito iliyopo Amerca ya Kaskazini (North Amerca) samaki hawa maarufu wanapatikana kwa wingi sana. Miongoni mwa maajabu ya samaki hawa ni safari yao ndefu ya kutembea kutoka mto ni kwenye baharini na kurejea tena walipo toka baada ya kukaa muda mrefu wakiwa baharini.

 

Samaki huyu anasifa ya kuishi kwenye maji baridi na maji ya chumvi. Maisha ya samaki hawa yanaanzia pale samaki jike anapotaga mayai maeneo ya juu ya mto amapo kuna maji yabaridi (yasiyo na chumvi). Baada ya kutotolewa kwa samaki hawa wanakaa mtoni hapa kwa muda kadhaa.baada ya kwisha kuuwa kiasi cha kuweza kujitafutia chakula wenyewe na kuweza kujilinda hapa wanaanza safari yao ya maajabusana.

 

picSalmon baada ya kukuwa na kukomaa anaanza kusogea karibu na bahari, na hapa mabadiliko huanza kutokea kwenye mwili wake ili kuweza kumfanya aishi kwenye maji ya chumvi. Baada ya kuweza kuendana na mazingira ya maji ya chumvi na hali ya hewa salmon wanaanza safari yao ya kuelekea baharini ambapo watakaa kwa muda mrefu sana.

 

Safari ya samaki hawa inaweza kuwa na urefu kuanzia kilomita 1600 mpaka kilomita 4000 inategemea aina ya samaki hawa. Inakadiriwa kuwa wakati wa safari yao samaki hawa huweza kutembea kwa umbali wa kilomita 6 mpaka 7 kwa siku. Baada ya kizazi hiki kuhamia baharini na kukaa kwa muda wa miaka kadhaa, samaki hawa wanapotaka kutaga na ili kuendeleza kizazi wanarudi kule walipozaliwa yaani mtoni. Na hapa safari ya kurudi iliyo na maajabu ndipo huanzia.

 

Itambulike kuwa samaki hawa wanatakiwa kurudi pale walipozaliwa na haijalishi ni muda gani toka waondoke lakini lazima watafika. Pia kwa kuwa maji ya mto yanaelekea baharini na samaki hawa wanarudi mtoni walipozaliwa basi safari yao itakuwa inapingana na maji ya mtu. Hivyo itawalazimu kukinzana na nguvu ya maji ya mtu na wakati mwingine wanapokutana kwenye maporimoko ya maji wanatakiwa waruke. Safari hii imejawa uvumilivu kwani kuna wanyama walao samaki huwa wanawasubiria maeneo haya yenye maporomoko pindi wanaporuka wawale. Samaki hawa wanaweza kuruka maporomoko yenye urefu unaokadiriwa kufikia mita 3. Pia Salmon anaweza kukutana na sehemu ya mto ambayo ina maji kidogo aya pamekauka, samaki huyu anaamuwa kuruka ili ayapate maji ama atasubiria mpaka maji yaingie aendelee na safari yake.

 

picWataalamu wanatueleza kuwa mnyama huyu aaweza kupajuwa mtoni alipo zaliwa kwa kutumia harufu ya maji. Inaelezwa kuwa samaki hawa wanaweza kutofautisha harufu za maji hata kwa kiwango kidogo sana. Samaki huyu pindi anapozaliwa kule mtoni harufu na maji ya eeo alipozaliwa anakuwa na kumbukumbu nayo bila ya kujali amekaa baharini kwa muda gani.

 

Salmon baada ya safari ndefu na iliyo ngumu anarudi mtoni ambapo amezaliwa. Salmon akiwa kwenye safari yake mwili wake hufanya babadiliko ambauo yatamfanya aweze kuishi kwenye maji ya baridi. Hii ni tofauti na samaki wengine ambao ukimtoa maji ya baridi papo kwa papo na ukamtia maji ya chumvi hufa. Salmon ana uwezo wa kuishi mazingira yote haya.

 

Baada ya kuwasili mtoni pale walipozaliwa samaki hawa wanataga mayai na kuyatotowa. Makinda yanapototolewa yanakuwa hayana uwezo wa kujilinda hivyo wanajificha kwenye mawe, baada ya wiki kupita hatimaye samaki hawa wanaweza kujitaftia chakula wenyewe safari hii huanza tena. Na haya ndio maisha ya samaki huyu salmon.

 

Nani kamfundisha samaki huyu kuweza kujuwa mazingira na maeneo alozaliwa, na kuweza kurudi bila ya kukosea. Kwa nini samaki huyu anatembea safari hii iliyo na ugumu na uvumilivu?. Salmon ni samaki ambaye anatupatia mafunzo mengi sana. Kwa mfano sikuzote kabiliana na changamoto kwani kukimbia zio njia sahihi ya kutatua tatua tatizo. Salmon anaenelea na safari yake bila ya kujali nguvu ya maji ya mto kuwa itamrudisha baharini, au maadua walao samaki ama maporomoko ambayo hataweza kuyaruka.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/11/Thursday - 12:29:21 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1102

Post zifazofanana:-

Madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji
Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua. Soma Zaidi...

Mbinu za kupunguza Kichefuchefu
Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu. Soma Zaidi...

Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Tabia za watu wenye damu ya group A au kundi A.
Posti hii inahusu zaidi tabia za watu wenye damu la kundi A na vyakula ambavyo wanapaswa kuvitumia, na pengine tutaona baadhi ya vyakula ambavyo havipaswi kutumiwa na watu wenye damu ya kundi A au group A Soma Zaidi...

THE DESTRUCTION OF THE ELEPHANT ARMY IN YEAR 570 AD.
This is the history of the attempt to destroy the city of Mecca and to destroy its people and destroy it in the history of the World. One leader, known as Abrah, organized a huge army to destroy Al-Qa'aba Soma Zaidi...

HADITHI YA SIRI YA UTAJIRI WA AJABU : sehemu ya 01
huu ni ufupisho wa kisa cha utajiri wa ajabu katika kijiji fulani huko zamani za kale. Soma Zaidi...

Dalili kwa mtu anayeharisha
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitia kinyesi chenye maji inawezekana kina damu au kisichokuwa na damu. Soma Zaidi...

Sababu za kutoka mimba yenye miezi Saba na nane
Posti hii inahusu zaidi sababu za mtoto kuzaliwa akiwa na miezi Saba na nane kwa kawaida mtoto wa hivi anakuwa hajafikisha mda wake kwa hiyo uzaliwa akiwa na miezi saba na nane, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali kama tutakavyoona Soma Zaidi...

Habari nilitaka kujua kuhusu ugonjwa wa fungusi kwenye uume
Je na wewe unasumbuliwa na fangasi wenye uume. Post hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...

Namna ya kutibu kuharisha kwa mtoto ukiwa nyumbani.
Post hii inahusu zaidi njia za kutibu kuharisha kwa watoto wakiwa nyumbani, kwa sababu mara nyingine mtoto anaweza kuharisha si kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ila ni uchafu tu kwa hiyo njia muhimu zinazofaa kutibu mtoto ni pamoja na yafuatayo. Soma Zaidi...

Vipimo vya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vipimo vya minyoo Soma Zaidi...

Saratani zinazowasumbua watoto.
Posti hii inahusu zaidi saratani zinazowashambulia watoto. Hizi ni aina mbalimbali za saratani ambazo upenda kuwasumbua watoto ambao ni chini ya umri wa miaka mitano na uleta madhara katika kipindi cha makuzi yao. Soma Zaidi...