SAFARI YA SITA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SITA YA SINBAD.

SAFARI YA SITA YA SINBAD

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

SAFARI YA SITA YA SINBAD.

Walipokusanyika watu wote akaanza kusimulia kuhusu safari yake ya sita. Nilipookoka na safari ya tano sikutamani tena kusafiri kwa njia ile. Hali hii haikudumu kwa muda mpaka nilipoamua kufanya safari ya mwisho kwani nilikuwa uymri umeshakwenda sana. Nikaamini kuwa faida nitakayoipata safari hii sitafanya safari nyingine yeyote ya majini. Basi nilianza kujiandaa kwa ajili ya safari hii. Hata hivyo maandalizi yalichukuwa muda kwani umri ulikuwa umeshakuwa mkubwa. Baada ya maandalizi safari ikaanza.

Safari hii ilikuwa mbaya sana, maana hata hatukuweza kupata siku mzima iliyo salama. Mara tuu baada ya kuanza safari kwa muda wa masaa kama nane kwa makadirio upepo uliharibika na kuwa mkali sana. Jahazi lilikuwa likipelekwa tusukokujuwa kwa muda wa siku tano. Siku ya sita upepo ulitulia katika sehemu ambayo hata hatuijui kabisa. Nahodha baada ya kuangalia zaidi eneo hili alilitukusanya karibu na akatuambia kuwa hapa tulipo tupo katika mkondo hatari sana baharini na hakuna jahazi lililokuja mkondo huu na kupona. Ghafla maji yaendayo kwa kasi yakatuchukuwa na kutupeleka kwenye ufukwe wa kisiwa tusichokijua. Tulipofika pale nahodha akatuambia tuchuke sisi na mizigo yetu kisha akagawa chakula tulicho nacho sawa kwa sawa kwa kila mtu. Kisha akatuambia kuwa hapa tulipo hakuna upepo unaotoka kuelekea kokote. Maji yote yanavutwa kuelekea hapa. Na eneo hili kama mnavyoona lina mlima huu ambapo hata ukipanda sauti haitafika popote wala kusikiwa na mtu.

Kisha akatuambia kuwa hakuna yeyote atakuja kutuakoaa hapa hivyo maisha ya mtu kuishi yatategemea kuisha kwa chakula chake. Wakati anazungumza maneno yale mimi nilikuwa nawaza yalonikuta kule kwenye mapango. Basi hali ikawa hivyo kwa hakika hakuna pa kutokea. Nilizunguka kuangalia eneo li;le nikagunguwa kuwa kuna mto ambao umetokea mlimani kisha ukakunja bila ya kuingua baharini ukarudi upande wa bondeni kudogo pembeni mwa ufukwe na ukapotelea kwenye pango ililo jembaba.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1129

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME.

Soma Zaidi...
Ndoa ya Sinbad na binti mfalme

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI.

Soma Zaidi...
SAFARI YA NNE YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA NNE YA SINBAD Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara.

Soma Zaidi...
Hadithi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Ndani ya pango la makaburi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA KWANZA MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA KWANZA MTOTO WA MFALME kwanza utambue mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa.

Soma Zaidi...
Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya samaki wa Rangi nne

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Kisiwa cha uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...