Sifa za wuamini zilizotajwa katika surat Al-ma'aarij


Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko. Inapomgusa shari huwa mwenye fadhaa. Na inapomgusa kheri huwa anaizuilia. Ila wanaosali; (hao hawana sifa mbaya). Ambao wanadumisha Sala zao. Na ambao katika mali zao iko sehemu maalumu. (70:19-24)


Kwa ajili ya aombaye na anayejizuilia kuomba (japo muhitaji). Na ambao wanasadiki siku ya Malipo. Na ambao wanaiogopa adhabu (itokayo) kwa Mola wao. Hakika adhabu ya Mola wao si ya kusalimika nayo mtu (mbaya). Na ambao wanahifadhi tupu zao. (70:25-2 9)


Isipokuwa kwa wake zao au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi. Lakini wanaotaka kinyume cha haya, basi hao ndio wanaoruka mipaka. Na ambao wanaangalia amana zao na ahadi zao . Na ambao ni imara katika ushahidi wao. Na ambao wanazihifadhi Swala zao Hao ndio watakaokuwa katika Mabustani wakihishimiwa. (70:30-35)



Mafunzo
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa:
Kwanza, binaadamu ameumbwa na udhaifu mwingi. Miongoni mwa udhaifu alionao ni kuwa anapofikwa na jambo lolote la shari hushikwa na huzuni kubwa na kukata tamaa; lakini akipata kheri kidogo, hujivuna na kuwa bahili.
Pili, mwanaadamu ataepukana na udhaifu mwingi alionao ambao humdunisha na kumshusha chini kuliko vilivyo chini, pale tu atakapokuwa Muumini wa kweli anayefanya vitendo vizuri ikiwa ni pamoja na:



(i)Kusimamisha swala kwa kuzihifadhi(kuteleleza vilivyo sharti na ngozo zake), kuziswali kwa unyenyekevu na kudumu nazo katika maisha yote.

(ii)Kutoa mali na kuwasaidia wanaadamu wenziwe wanaohitajia baada ya kupatwa na shida mbali mbali.

(iii)Kusadikisha au kuwa na yakini kuwa atarejea kwa Mola wake.

(iv)Kuogopa adhabu ya Allah(sw) kwa kujiepusha na yale yote yanayomghadhibisha Allah(sw) na kuomba mara kwa mara kuepushwa na moto (25:65 - 66)

(v)Kuhifadhi tupu kwa kujiepusha mbali na zinaa na vishawishi vyake vyote.

(vi)Kuchunga amana zote na amana kuu ikiwa ni ile ya Ukhalifa aliyotunukiwa na Allah (s.w) kama tu navyoku m bushwa kati ka aya ifuatayo:



"Kwa yakini tulitoa amana (ya Ukhalifa) kwa mbingu na ardhi na milima vikakataa kuichukua na vikaogopa, lakini mwanaadamu akaichukua.Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa (kwa kuhini amana aliyopewa na Mola wake) mjinga sana." (33:72)



(vii) Kuchunga ahadi zote anazotoa kwa watu na kwa Allah (s.w). Ahadi kuu aliyoitoa muumini kwa Allah (s.w) ni ile ya "shahada mbili" pale anapoahidi kuwa hatamshirikisha Allah (s.w) na mungu yeyote na kuwa ataishi kwa kufuata sunnah ya Mtume Muhammad (s.a.w).



(viii)Kuwa imara katika ushahidi au katika kusimamia haki. Muumini wa kweli ni yule asiyehofu chochote katika kusimamia haki.