image

fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

fadhila za sura kwenye quran

imageimage FADHILA ZA BAADHI YA SURA
Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.
1.Surat al-fatiha.
Amesimulia Ibn ‘Abas kuwa “wakati ambao jibril alikuwa amekaa na Mtume akasikia sauti ya mlango uliofunguliwa juu yake akanyanyu kichwa chake kisha akasema “hiyo ni nsauti ya mlango uliopo mbinguni umefunguliwa siku ya leo, na katu haujawahi kufunguliwa ila ni leo tu (ndio mara ya kwanza kufunguliwa). Basi akashuka Malaika kutoka kwenye mlango huu akasema (Jibril) huyu ni malaika ameshuka duniani na hajawahi kushuka kamwe ila ni leo tu akatoa salamu (malaika huyo) kisha akasema (kumwambia mtume) tuo habari za furaha kwa nuru mbili ulizopewa na hakuwahi kupewa mtume yeyote kabla yako kamwe (ambazo ni) surat al-fatiha na aya za mwisho za surat al-baqarah hatusoma herufi yeyote isipokuwa utapewa” (amepokea Muslim). Amesema Mtume “surat al-fatiha ni dawa ya kila gonjwa” amepokea Bayhaqiy)

2.surat al-baqarah
Amesema Mtume “…Mwenye kuisoma katika nyumba yake usiku hatoingia shetani nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu, na mwenye kuisoma mchana hatoingia shetani nyumba hiyo kwa michana mitatu” (amepokea Ibn hiban, tabrany na Bayhaqiy).

3.ayat al-qursiy.
Amesema Mtume “katika surat al-baqarah kuna aya iliyobora kuliko aya zote haitasomwa aya hiyo kwenye nyumba yenye shetani ila atatoka kwenye nyumba hiyo, (aya hiyo ni) ayat al-kursy) (amepokea Al-Haakim na Bayhaqiy)

3.aya za mwisho za surat al-baqarah
Amesema Mtume hakika Allah ameimalizia surat al-baqarah kwa aya zilizo tukufu (zilizotoka) kwenye hazina chini ya ‘arshi basi jifundisheni aya hizo na muwafundishe wake zenu na watoto wenu. Kwani mna ndani ya aya hizo dua, qiraa na dua” (amepokea Al-Haakim kutoka kwa Abuu Dhari).
Pia Amesema mtume “aya mbili za mwisho za surat al-baqarah mwenye kuzisoma usiku zitamtosheleza” (amepokea bukhari,Muslim, Ahmad na Ibn Maajah kutoka kwa ibnmas’ud)

4.surat al-imraan
Amesema Mtume katika mafhumu ya hadithi iliyo sahihi kuwa itakuja qurani siku ya kiyama ikiongozwa na surat al-baqarah na al-imraan katika hali ya makundi mawili na yakawa yanajadiliana juu ya mtu wao yaani msomaji.
Pia amesema Mtume Mtu mwenye kusoma “SHAHIDALLAHU ANNAHU LAA ILAAHA ILLAA HUWA WALMALAAIKATU WA-ULUL-ILMI QAAIMAN BIL-QISTWI LAA ILAAHA ILLAA HUWAL-AZIZL-HAKIIM. INNA DINA ‘IN-DALLAHIL-ISLAM”
Kisha akasema “wa ana ash-hadu bimaa shahidaLLAHU bihi, wa astawdiu LLAHU hadhihi shahadah, wahiya lii indahu wadi’ah”
Basi ataletwa mtu huyu siku ya kiyama na ataambiwa na Allah ewe mja wangu hii ni ahadi yangu niloahidi na mimi nina haki ya kutekeleza ahadi muingizeni mja wangu peponi” (amepokea Abuu Shaykh kutoka kwa Ibn masud).

5.surat israa
Amesema Mtume mwenye kusoma wakati wa asubuhi au jioni “QULID-’ULLAHA AWID-’UR-RAHMANA AYAAMA-TAD-’U FALAHUL-ASMAAU-LHUSNAA” mpaka mwisho wa sura moyo wake hautokufa siku hiyo wala usiku huo. (amepokea Dilamy).

6.Surat Zumar
Amesimulia ‘Aisha kuwa alikuwa Mtume halali mpaka asome surat zumar na surat israa” (amepokea Tirmidh)

7.surat alkahafi
Amesema Mtume “mwenye kusoma surat al-kahafi siku ya ijumaa itampatia mwangaza kati ya ijumaa ile mpaka nyingine.(amepokea Al-haakim na Bihaqi kutoka kwa Abuu musa al-’Ashar).
Amesema Mtume mwenye kuhifadhi aya 10 za mwanzo za surat al-kahafi atalindwa na fitna za Dajali.(mepokea Muslim, Ahmad,na Nisai kutoka kwa Abuu Drdaa).

8.surat yaasin.
Amesimulia Anas kuwa mtume amesema “kila kitu kina moyo, na moyo wa qurani ni surat yaasin. Na mwenye kuisoma huandikiwa kwa kisomo chake thawabu za kusoma qurani mara kumi. (amepokea tirmidh na Dilamy).
Pia amesimulia Ma’aqil ibn yasar kuwa Mtume amesema “moyo wa qurani ni surat yaasin, mwenye kuisoma kwa kutaraji radhi za Allah na mafanikio ya siku ya mwisho atasamehewa madhambi yake.…” (amepokea imam Ahmad na Bayhaqi).

9.surat dukhani
Amesimulia Abuhurairah kuwa Mtume amesema “mwenye kusoma surat dukhani wakati wa usiku ataamka asubuhi na huku malaika sabini elfu wakimtakia msamaha” (amepokea Tirmidh na nisai) na katika mapokeza ya Tabrani Mtume amesema “mwenye kusoma surat dukhani siku ya ijumaa usiku au mchana Allah atamjengea mtu huyo nyumba peponi”

10.surat al-fat-hi
Amesimulia ‘Umar kuwa Mtume amesema “hakika imeshushwa kwangu mimi usiku wa leo sura ambayo ninaipenda kuliko vitu vyote vinavyochomozewa na jua” kisha akasoma INNAA FATAHNAA LAKA FAT-HAN MUBINAA (surat al-fat-hi) (amepokea bukhari).

11.surat al-waaqi’a
Amesimulia ‘Abdullah ibn Mas’ud kuwa Mtume amesema “mwenye kusoma surat al-waaqi’a kila usiku hatopatwa na njaa (kali) katu.

12.surat MUSBIHAT
Hizi ni sura zilizoanzwa na tasbihi yaani sabaha au yusabihu nazo ni tano ambazo ni al-hadid, al-hashri, swafa, al-jum-’a, na taghaabun. Amesimulia ‘Irbaadh ibn Saariya kuwa hakika Mtume alikuwa akisoma musabihat kabla ya kulala na huwa akisema “hakika mna katika sura hizo aya bora kuliko aya elfu moja” (amepokea tirmidh)

13.surat al-mulku
Amesimulia Abuuhurairah kuwa mtume amesema “katika qurani kuna sura ina aya 30. Ni yenye kumuombea mtu mpaka atasamehewa nayo ni “TABAARAKAL-LADHII BIYADIHIL-MULKU”. (amepokea Abuu Dawd na tirmidh)

14.Suratul ikhlas, nasi na falaq
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).


                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 693


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

quran na sayansi
QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIAAsalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Soma Zaidi...

quran na sayansi
2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio. Soma Zaidi...

Nini maana ya Quran
Post hii inakwenda kukuambia maana ya Quran Soma Zaidi...

yaliyomo: HUKUMU YA MIM SAKINA, NUN SAKINA, MADA, WAQFU, QALAQALA, TAFKHIM NA TARQIQ, USOMAJI WA QURAN
DARSA ZA TAJWID YALIYOMOSURA YA 01 . Soma Zaidi...

Makundi ya Id-ghamu katika usomaji wa Quran Tajwid
Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al Quraysh
Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao. Soma Zaidi...

ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN
ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido. Soma Zaidi...

Fadhila za surat al-fatiha na sababu za kushuka kwake
1. Soma Zaidi...

Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia
Soma Zaidi...

Nini maana ya Iqlab katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)
SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...