Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka na matibabu yake
PRESHA YA KUSHUKA NA MATIBABU YAKE
Presha ya kushuka mara nyingi haina dalili za kutisha, pia haina shida sana ukilingnisha na presha ya kupanda. Kama unahisi dalili za presha ya kushuka kama kizunguzungu, kichwa kuwa chepesi wakati unaposimama na kuamka, huku mgandamizo wa damu kupunguwa hii hali inatambulika kama postural hypotension.
Kugundua presha ya kushuka daktari atakupima kwa kipimo maalumu. Pia vipo vipimo vngine kama vitahitajika zaidi, kama vile electrocardiogram (ECG), ultrasound pia kipimo cha damu kuangalia kiwango cha sukari kwenye damu na kuangalia kama kuna upungufu wa damu.
Utaratibu wa kuishi ukiwa na presha ya kushuka.Ningependa tu kukujulisha kuwa unaweza kuishi vyema ukiwa na presha ya kushuka, hata bila ya kutumia dawa za mahospitali. Kabla hatujaona dawa za mahospitali sasa nanakwenda kukueleza utaratibu wa lishe kwa mwenye prsha ya kushuka.
1.Kula chakula chenye chumvi zaidi2.Kula vyakula vyenye majimaji mengi kama matunda na mfano wake3.Punguza kunywa vilevi4.Kunywa maji mengi hasa wakati wa joto5.Fanya mazoezi ya mara kwa mara6.Unapolala tumia mto, yaani sehemu ya kichwa chako iwe juu7.Jizuie kubeba vitu vizito8.Washa kukaa maeneo yenye joto sana ma kuoga maji ya moto kwa muda mrefu.9.Acha kusimama wima sehemu moja kwa muda mrefu.
Dawa zinazotumika kutibu presha ya kushuka (hypotension)A.Fludrocortisone, zungumza na daktari kabla ya kutumiadawa hii.B.Midodrine.
Hakikisha dawa hizi humezi kiholela. Kabla ya kutumia dawa yeyote kwanza zungumza na daktari kwanza. Hii ni kwa ajili ya afya yako.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yatokanayo na fangasi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya maradhi yanayosababishwa na hali za maisha
Soma Zaidi...Hapa nitakueleza namna ambavyounaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi ya ini. Kwa njia hizi unaweza kujikina wewe na wengineo na maradhi haya hatari ya ini.
Soma Zaidi...Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi utaziomna hapa. hizi zinaweza kuwa ndio za kwanza kwa ambaye hajapima HIV
Soma Zaidi...Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la Kichwa, Kiharusi, Uvimbe kwenye ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi,
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za vidonda vya tumbo sugu
Soma Zaidi...Post yetu Leo inaenda kuzungumzia Maumivu ya nyuma ni malalamiko ya kawaida. Kwa upande mkali, unaweza kuchukua hatua za kuzuia au kupunguza matukio mengi ya maumivu ya mgongo. Ikiwa kinga itashindikana, matibabu rahisi ya nyumbani na mbinu sahihi za m
Soma Zaidi...Je na wewe unasumbukiwa na kunggoka jwa kucha. Tatizo limekunaza una muda gani nalo?
Soma Zaidi...