Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga

Maana ya Swaumu (Funga)



Kilugha; neno 'Swaum' lina maana ya kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa nabii Isa (a.s) alijizuilia (alikuwa katika Swaum ya) kutosema na mtu yoyote juu ya mtoto wake.


'... Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: `Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya Swaum (kufunga), kwa hiyo leo sitasema na mtu' (19:2 6).



Katika Sharia ya Kiislamu kufunga (Swaum) ni kujizuilia kula, kunywa, kujamii, kuingiza kitu chochote katika matundu ya mwili na kujizuilia kumuasi Allah (s.w) kuanzia alfajiri ya kweli mpaka kuingia ma gharibi.


Lengo la Swaumu



Lengo la Swaum katika Uislamu ni kumuwezesha mja awe mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Hivyo, ili lengo hili litimie mfungaji pamoja na kujizuilia kula, kunywa, kujamii, hanabudi pia kujizuilia na kitendo chochote kitakachompelekea kuvunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w). Kwa maana nyingine, ili Swaum ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, mfungaji hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu pamoja na fikra na hisia zake -na matendo aliyoyakataza Allah (s.w.).


Funga ya macho ni kujizuilia kutazama yale yote aliyoyakataza Allah (s.w), funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w), kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana n.k., funga ya masikio ni kujizuilia kusikiliza yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w); funga ya miguu ni kujizuilia kuendea yale yote aliyotukataza Allah (s.w); funga ya fikra na hisia, ni kujizuilia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea mja kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith zifuatazo:


'Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuw a anaacha chakula chake na kinyw aji chake - ( Allah (s.w) hana haja na funga yake). (Bukhari).



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema; Ni wangapi wamefunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu, ni wangapi wanaoswali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).



Hadith hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuilia na maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 349

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo namba 14
12. Soma Zaidi...

Nini maana ya twahara katika uislamu, na ni zipi njia za kujitwharisha
1. Soma Zaidi...

Kujiepusha na maringo na majivuno
Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ndizi
Soma Zaidi...

VIPI VIDONDA VYA TUMBO VINATOKEA
VIPI VIDONDA VYA TUMBO VINATOKEA 1. Soma Zaidi...

FORM ONE CHEMISTRY
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Vocabulary test 003
Soma Zaidi...

Ujumbe wa Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Mfalme Namrudh
Soma Zaidi...

VOCABULARY ANSWERS
1. Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza
Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 35: Msioneane Choyo, Msizidishiane Bei, Msichukiane
Soma Zaidi...