Umuhimu wa Kusimamisha Swala
Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.a) tuliyoirejea mwanzoni, kusimamisha swala ni nguzo ya pili ya nguzo za Uislamu. Katika kuonyesha umuhimu wa kusimamisha nguzo hii Mtume (s.a.w) a me sem a:
“Sw ala ndio nguzo kubw a ya Dini (Uislamu) mwenye kusimamisha swala amesimamisha dini (Uislamu) na mwenye kuiacha swala amevunja Dini .” (Uislamu)”
Katika Hadithi nyingine, amesimulia Jabir (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Tofauti yetu sisi (Waislamu) na ukafiri ni kuacha swala”. (Muslim) Pia Mtume (s.a.w) amesema:
“Tofauti iliyopo kati yetu (Waislamu) na wengine (wasiokuw a Waislamu) ni swala ”. (Ahmad, Abu Daud, An-Nasai, Tirmidh)
Kutokana na hadithi hizi, tunajifunza kuwa mtu ambaye hasimamishi swala, hatakama anajiita Muislamu si Muislamu bali ni kafiri kama makafiri wengine. Anakuwa kafiri kwa sababu amekanusha amri ya Allah iliyowazi kama inavyobainika katika aya zifuatazo:
“Waambie waja wangu walioamini, wasimamishe swala. ”(14:31)
“... Basi simamisheni swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyow ekewa nyakati makhsusi.” (4:1 03)
“Na waamrishe watu wako kuswali (kusimamisha swala) na uendelee mwenyewe kwa hayo...” (20:132).
Tukumbuke kuwa hawi Muumini yule anayekuwa na hiari katika kutekeleza amri ya Allah na Mtume wake kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:
“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi”. (33:36)
Umeionaje Makala hii.. ?
Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10
Soma Zaidi...Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali.
Soma Zaidi...- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.
Soma Zaidi...Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...