7. Kulala MuzdalifaMuzdalifa ni kitongoji kilichoko kati ya Arafa na Mina. Baada ya jua kuchwa Mtume (s.a.w) na Waislamu waliongozana nao katika Hija ya kuaga, waliondoka Arafa na kuelekea Muzdalifa kwa kufuata njia tofauti na ile waliyoijia kutoka Mina.Wakati wa kwenda Muzdalifa, Mtume (s.a.w) amewaamrisha Waislamu waende kimya kimya katika mwendo wa utulivu bila ya makelele na vishindo.Mtume (s.a.w) na Waislamu alioongozana nao waliswali al-Magharibi pamoja na al-Ishai kwa Qasr walipofika Muzdalifa. Mtume (s.a.w) na Waislamu walilala Muzdalifa mpaka Alfajir, bali Mtume (s.a.w) aliwaruhusu watu dhaifu pamoja na wanawake na watoto waondoke kwenda Mina usiku wa manane baada ya mwezi kutua ili waende pole pole na kuepukana na msongamano wa watu wakati wa kutupa mawe. Lakini aliwaamuru wasianze kutupa mawe mpaka jua lichomoze. Baada ya swala ya Al-fajir, Mtume (s.a.w) alipanda ngamia na kuelekea sehemu takatifu iitwayo “Mash-arul-Haram”. Ilivyo ni kwamba bonde lote la Muzdalifa linaitwa kwa jina hili lakini sehemu hasa ambayo Mtume (s.a.w) alisimama katika hija ya Kuaga ni pale ulipo Msikiti wa Muzdalifa hivi sasa. Mtume (s.a.w) alipofika hapa “Mash-arul Haram” alielekea Qibla, akatoa Takbira na kumuomba Allah (s.w).Haya ndio maagizo ya Allah (s.w) kama tunavyosoma:


“.Na mtakaporudi kutoka Arafaat m tajeni Mw enyezi Mungu kw enye Mash-arul Haram. Namkumbukeni kama alivyokuongozeni. Na hakika zamani mlikuw a miongoni mwa waliopotea ” (2:198).Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba si lazima kila Haji asimame sehemu ya Msikiti, bali sehemu yoyote atakayosimama wakati huu wa kumtukuza Allah (s.w) kwa Takbira na kuomba dua, itafaa ili mradi tu aelekee Qibla. Kwani kama tulivyoona katika hadith, Mtume (s.a.w) amesema:“Ninasimama hapa lakini bonde lote la Muz-dalifa ni mahali pakukaa na kusimama ” (Muslim).


Baada ya jua kuchomoza, Mtume (s.a.w) na mahujaji wengine walianza safari ya kuelelekea Mina. Walipofika kwenye bonde la Muhassir (mahali walipouawa watu wenye jeshi la tembo), Mtume (s.a.w) aliwaamuru watu wapite haraka haraka. Wakati wakielekea Mina Mtume (s.a.w) alimtuma Fadhl bin Abbas (r.a) amuokotee vijiwe saba na akawaamuru watu wengine waokote vijiwe saba. Mahali popote pale njiani kuelekea Mina isipokuwa kwenye bonde la Muhassir mtu anaweza kuokota vijiwe saba kwa ajili ya ibada ya kutupa mawe kwenye mnara mkubwa (Jamaratul Aqaba). Mtume (s.a.w) alikuwa akiitikia Labbayka (Talbiya) kuanzia Muzdalifa mpaka alipofika Mina na kuanza kutupa jiwe la kwanza kwenye mnara mkubwa kama tunavyojifunza katika hadith ifu atayo:Ames imulia Ibn Abbas (r.a): Mtume (s.a.w) alimpandisha Al-Fadhl katika kipando chake na akaw a nyuma yake, na Fadhl ameeleza kuw a Mtume (s.a.w) aliendelea mfululizo kuleta Talbiya mpaka alipofanya Ramy katika Jamrat (Jamratul Aqaba). (Bukhari).