MALIPO YA WEMA NI WEMA

Download kitabu Hiki Bofya hapa MALIPO YA WEMA NI WEMA Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi.

MALIPO YA WEMA NI WEMA

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

MALIPO YA WEMA NI WEMA

Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Hapa Zubeida akawa anajiulia kuwa ni nani huyu anakuja? Aua ni yule mchumba wake? Maswali haya hayakupata amjibu. Baada ya muda kupita akatokea binti mmoja mreembi kama mwezi uliokamilika umbo lake. Binti yule akamsogelea Zubeidah na kupiga goti mbele yake na kuukamata mkono wa Zubeidah na kuubusu kisha akamwambia β€œ NI YAPI MALIPO YA WEMA? KWA HAKIKA NI WEMA TU”.

Lilikuwa ni swali ambalo halihitaji majibu kutoka kwa Zubeidah. Kwa malipo ya wema ni wema, Zubeida akamuuliza β€œni nani wewe ni ni nani mimi na nimefuka vipi hapa?. Yule mrembo akaanza kutoa kisa chake. Kuwa yenye ni mtoto wa mkuu mfalme wa majini ambaye alionana naye hapo mwanzo. Alipokiuwa matembezima jana akiwa amejibadili katika umbo la nge alipokuwa nakimbizwa na adui wake aliyekuwa katika umbo la kunguru alimsaidia kwa kumuuwa adui wake kunguru. Hivyo yule nge alikuwa ni huyu mtoto wa mfalme. Kwa ufupo ni kuwa Zubeidah amemuokoa mtoto wa mfalme katika kizingiti za kifo kuuliwa na adui wake na huu ni wema mabao analipwa.

Basi yule mrembo akamwambia Zubeida kuwa ndugu zako walipokutumbukiza baharini nilikuwepo kwenye jahazi lenu kwa nia ya kuku;inda mpaka ufikapo kwenu. Hivyo nilikuokoa kwenuye ajali ile na sikuweza kumuokoa mchumba wako, kwa hilo naomba unisamehe sana. Hata hivyo baba yangu anaweza kukupa chochote utakacho kiseme utapata, na hata ukitaka utaishi hapa na mimi. Ila kuhusu ndugu zako kwa hakika sitaweza kuwasamehe katu. Nitawapa adhabu kubwa sana nai ningewauwa ila kwa kuhofia chozi lako siwezi kufanya hivyo.

Basi Zubeidah akaitwa na mfalem wa majini yule na kuulizwa nini ameamua kati ya yale aloelezwa na binti mafalme. Zubeidah akachagua kurudishwa nyumbani kwao na hakuhitajia chochote. Basi binti mafalme akampa unywele wake na kumwambia ukiwa na shida na mimi choma nywele hii kwa hakika nitakuja hapo kwa haraka zaidi. Basi kufumba na kufumbua Zubeidah akajikuta yupo nyumbani kwake na mlangoni wamekaa mbwa wawili na kuangalia pembeni akakuta bahasha ambayo imewekwa mlangoni. Kufungua bahasha ile akakuta ndani kuna barua iloandika\wa β€œKutoka kwa Binti Mfalme wa majini ya majini na Nchi kavu kwenda kwa Zubeidah mwana wa tajiri mpotea njia mwenye kusalitiwa. Ama baada ya salamu napenda kukutaarifu kuwa hao mbwa unaowaona mlangoni kwako ni ndugu zako na hiyo ndio adhabu niloichagua. Watabaki hivyo kwa muda wa miaka 10 na utakuwa ukiwapiga fimbo za mijeledi 300 kwa kila mmoja na kila siku. Na kama hautafanya hivyo watakufa siku inayofata. Ama kuhusu mali zako zote nimeziokowa na zipo stoo. Hata hivyo baba yangu amekujengea nyumba karibu jirani na mji wa Mfalme mwadilifu Harun Rashidi mfalme wa Baghdah. Huko uende na ukakae na ndugu zako hao. Usisahau kufanya nilichokwambia Zubeidah.”

Hivyo Zubeidah akachukuwa mali zake na kuhamia katika nyumba ile aloambiwa mjini Baghdad na ndugu zake. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mbwa wakawa wanatoa machozi mengi sana na hata mfalme akawa anatoa machozi. Hivyo hii ndi sababu ya mimi kuwaadhibu mbwa hawa kila siku yalikuwa ni maneno ya Zubeidah. Mfalme baada ya kusikiliza hadithi hii akamgeukia Amina aliyekuwa na alama na makovu kwenye mwili wake na mumwambia aeleze hadithi yake, nae akaanza kama ifuatavyo;-


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1256

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Kisiwa cha uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
JINI NA MFANYABIASHARA

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA.

Soma Zaidi...
Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Safari ya nne ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya mke na kasuku

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
SAFARI YA SABA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SABA YA SINBAD Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani

Soma Zaidi...
Safari ya tano ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya samaki wa Rangi nne

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama.

Soma Zaidi...