Hadithi ya mwenye kutabiriwa mtoto wa tajiri

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI

Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Kwa sasa nina umri w miaka 15 na baba yangu aliponizaa alinichagulia jina la Agib. Nimewekwa hapa kwenye handaki si kama nimetelekezwa hapana. Hii ni njia pekee iliyoonekana kuwa nitakuwa salama. Bla shaka unataka kujuwa hasa nini kilinitokea, mambo yalikuwa hivi;-

 

Baba yangu kabla hajanizaa kwa muda wa mwaka mmoja alipata ndoto ya ajabu sana. Aliwatafuta watu maarufu na wenye elimu ya kutambuwa maana za ndoto na wakamwambia kuwa mke wake yaani mama yangu atapata ujauzito wa mtoto wa kiume. Na mtoto huyo ataishi kwa furaha na amani kwa muda wa miaka 15. na kama akifika miaka 15 bila ya kitu chochote kumpata Jabir mwana wa mfalme katika mlima wa sumaku, mtoto huy ataishi salama mpaka uzeeni. Vinginevyo kama akifika miaka 15 na mwana wa mfalme Jabir akipatwa na ajali katika mlima wa sumaku basi uhesabu siku 40 tu za umri wa mtto wako zitakazokuwa zimebaki toka utakapopata hiz habari.

 

Hivyo mambo yakawa kama hivyo mimi nikazaliwa na mpaka sasa nina miak 15 sijawahi kuumwa wala kupata majonzi makubwa. Lakini ni siku 5 zilizopita baba alipata habari kuwa Mlima wa sumaku umesababisha ajali ya watu na huenda huyo Jabir mwana wa malme akawemo humo. Hivyo baba akaamuwa kunificha huku ili nisiweze kukutana na jabir. Kwa sasa nina matumaini kidogo lakini huwezijua hatima ya mwanadamu. Hii ndio stori yangu ewe ndugu yangu.

 

Basi niliposikia stori ya kijana yule nilipatwa na majnzi kuona kumbe ni mimi nitakayemuuwa. Sikuamini mawazo haya na kikaapa kuakaa pale ili nimlinde huenda akawa ni mtu mwingine atakayekuja kumuuwa. Basi niliaua kumdanganya jina langu na kumwambia naitwa Habir ni mvuvi niliyepatwa na ajali majini. Nikampatia mapera niliyochuma kule nje na aliyependa sana. Basi nikamwambia nitaishi na wewe hapa na nitakulinda na huyo anayetarajiwa Jabir kama akija.

 

Kijana alikubali na alifurahi pia, kwani alitaka hata apate mtu wa kuweza kuzungumza naye pale ndani, maana wazazi wake walimuahidi kuwa watakuja siku ya 40. basi mimi nikawa ndiye mfanyaji kazi pale ndani, napika na kufanya mambo kmengine kama kutandika kitanda na kufagia. Kwakweli tuliishi kwa furaha sana wawili sisi pale ndani. Nilikuwa nikijaribu kumfurahisha kila wakati kwa namna yoyote ile.

 

Basi mabo yakawa kama hivyo, tuliishi kwa upendo na furaha kubwa kwa muda wa siku 39 zote pale handakini. Siku ya 40 hatimaye ikafika na kila mmoja katika sisi alifikiri mambo yale yamekwisha hivyo kijana yupo salama. Siku hii kijana alivaa nguo zake nzuri na niliandaa chakula kizuri sana. Ilifika muda wa wa kukaribia mchana kijana akaend kualala. Basi mimi nikaendelea kuandaa chakula na vinywaji. Lakini nilipotaka kumenya matunda sikukiona kisu.

 

Nikaenda kukitafuta kisu nimenye matunda bila ya mafanikio. Ghafla nikakumbuka kuwa kijana alikuwa akimenyea embe jana kitandani kwake. Basi nikaelekea kwenda kukichukua kisu. Nikakikuta amekitundika kwenye mjiti wa kitanda kunapochomekewa pazia la kitanda. Basi kwa utaratibu nikapanda pale kwenye kitanda bila ya kumuamsha na nikawa nakichomoa. Kwakuwa mikono yangu ilikuwa ikiteleza kisu kiliniponyoka na kufikia kwenye kifua cha kijana na kuumaliza uhai wake kupitia moyo.

 

Nilipatwa na woga sana, sikiamini9 kama mimi niliyetaka kumlinda ndiye nimemuua. Nililia sana, ila ghafla nikakumbuka leo wazazi wake watakuja hivyo nikatoka pale ndani kwa haraka. Nilipomaliza tu kutoka nje na kuukaribia mpera nikaona kundila watu linakuja. Basi kwa woga wangu nikaificha pale kwenye mpera.

 

Wale watu wakaingia ndani mule na kwa muda usiopungua masaa 3 wakatoka na mwili wa kijana huku wengine wanalia sana. Wakauzika mwili ule pale pembeni na kisha wakaondoka. Nilikaa pale kwa muda mrefu hata ilipokaribia jioni nikatoka pale na kutembea tembea katika eneo lile. Nikakuta kanhia kanakoelekea milimani nikakafuata. Huko nikakutana na watu 10 wote ni machongo wa jicho la kulia.

 

Watu wale nikawaelezea kuwa mimi nimepata ajali baharini na sina ninaemjua eneo hili hivyo nikawaomba wanihifadhi. Ijapokuwa kati yao baadhi walikuwa wakikataa lakini mkubwa wao akazungumza “tutakukubalia kukaa nasi ila kwa sharti moja naloni KUTOKUULIZA CHOCHOTE KATIKA MAMBO YATAKAYOFANYIKA USIKU”. kuna mwengine akaongezea kwa kusema “na sharti hili ni kwa ajili ya usalama wako tu” basi nikatoa ishara ya kukubaliana na sharti lile.

 

Kwahakika niliishi bila ya shaka nyumbani kwao wale machongo. Lakini jambo moja tu lilikuwa likinisumbua ni kuwa kila ifikapo usiku wanachukuwa mijeledi na kuanza kujitandika mgongoni viboko 100. nilikaa hivi bila ya kuuliza kwa muda wa siku kadhaa. Siku moja nikaamuwa kuwauliza na lolote litakalotokea na litokee ila lazima nijuwe ni kwa nini wanajitandika mikwaju ile na ni kwa nini wote ni machongo wa jicho la kulia?.

 

Basi mambo yakawa kama hivi, siku ile mchana nikawauliza maswali yale mawili. Basi walishangaa sana kuona ninakiuka masharti ya kuishi ndani pale. Mkubwa wao akanieleza “kijana sharti hili tuliweka kwa ajili ya usalama wako, lakini sasa inaonekana hata haujali nini kitakupata”. kaka mimi naomba kupata majibu ya maswali haya na sijali kwa lolote litakalonipata. Akanijibu “sisi hatutakueleza chochote katika hayo ila utajionea mwenyewe, kama ukotayari tutafanya maandalizi kesho” nikamjibu kuwa nipo tayari.

 

Basi siku ile ilofata asubuhi wakamchinja kondoo nakuniambia “tutakushonea kwenye ngozi ya kondoo huyu na tutakupa kisu. Tuatkuweka juu ya mlima na hapo atakuja roki (ndege) atakubeba akidhani ni kondoo. Pindi akikutuwa tumia kisu na uchane ngozi yeye atakimbia. Utakapotoka upande wa mashariki ya mlima kwa chini utaona njia ndogo. Ifate njia hiyo na utakuba nymba. Humo usimuulize mtu yeyote juu ya mambo haya. Ukifanikiwa kurudi hapa ndani ya sikua 100 na ukawa haukupata majibu ya maswali yako nitakujibu mwenyewe

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-08     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 591

Post zifazofanana:-

Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sita
Post hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya sehemu ya sita.sehemu hii inaonyesha jinsi bibi alivyo ndumila kuwili na hapendi kuonekana mbaya. Soma Zaidi...

Nyanja sita za afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu nyanja sita za afya Soma Zaidi...

Unakuta siku imefka ya hedhi kabla haijaanza kutoka hedhi yanatoka maji meupe clean kabisa hii Ina naamisha nini?
Kutoka na majimaji ka uchache kwa mwanamke sio jambo lakishangaa sana. Damu hii inawezapiabkikbatana damu na maumivu makali. Soma Zaidi...

Walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu
Post hii inahusu Zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu, pamoja na kuwepo Kwa sababu zinazopekekea kupata tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu ila Kuna watu wenye hali Fulani wako kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu kama Soma Zaidi...

Mbinu za kupunguza Kichefuchefu
Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu. Soma Zaidi...

Utaratibu wa lishe kwa wajawazito na wanaonyonyeaha
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wajawazito na wanaonyonyesha Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa uchovu sugu.
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa uchovu sugu ni ugonjwa tata unaoonyeshwa na uchovu mwingi ambao hauwezi kuelezewa na hali yoyote ya matibabu. Uchovu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa shughuli za kimwili au kiakili, lakini haiboresha kwa kupumzika Soma Zaidi...

Namna ya kuchoma chanjo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa. Soma Zaidi...

Sababu za kuwepo kwa saratani ya inni.
Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za kuwepo kwa saratani ya ini, saratani hii imekuwa tishio kwa wengi ila ni vizuri kujua baadhi ya sababu ambazo uchangia sana kuwepo kwa tatizo hili la saratani ya inni. Soma Zaidi...

Ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu -multiple sclerosis
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dadili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu ambao kitaalamu hujulikana Kama multiple sclerosis. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Bawasili
Posti hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa Bawasili, ni ugonjwa unaotokea kwenye njia ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa uvimbe au nyama ambazo uonekana hadi nje, kwa lugha ya kitaalamu ujulikana kama haemorrhoid au pokea. Soma Zaidi...

Ukuaji wa mmea
Je wajua kwa nini mmea kama nyasi na miti hukua? Posti hii inahusu' zaidi ukuaji wa mimea katika mazingira yetu kwa sababu watu hawatambui kwamba mimea .ni chanzo cha mahitaji kwa binadamu. Soma Zaidi...