image

MUENDELEZO WA HADITHI YA MSHONA NGUO

MUENDELEZO WA HADITHI YA MSHONA NGUO

MUENDELEZO WA HADITHI YA MSHONA NGUO



Mshona nguo akaendelea kusimulia mbele ya sultani kuwa yule muandaaji wa shughuli alipojiridhisha kuwa kinyozi alimtendea ubaya kijana, basi kinyozi ilibidi afungiwe kwenye chumba maalumu kwa uchunguzi zaidi. Mshona nguo anaendelea kusema kuwa baada ya shughuli kuisha kwa salama mimi niliondoka kuelekea nyumbani. Lakini kwa mkewangu mambo hayajakuwa sawa. Mke wangu alikuwa na wivu sana na alitaka kujuwa hasa kilichonichelewesha. Baada ya kumueleza yote akaniambia nimpeleke na yeye akafurahi, kula na kunywa. Sikuwa na jinsi nilimchukuwa mkewangu na kutafuta hoteli nzuri.


Nikiwa na mkewangu tuliendelea kula na kunywa na kufurahi pamoja hadi ilivyofika jioni. Mkewangu akachukuwa samaki mkubwa sana na ndizi kwa lengo la kwenda kupika chakula cha usiku. Nilijuwa kuwa anantaka kunikomowa maana anajuwa fika kama mimi nimeshiba sana. Niliwaza jambo lamda nitafute mtu wa kwenda naye nyumbani ili tule kwa pamoja. Katika pitapita za mitaa nikiwa na mkewangu, ndipo nikakutana na yule kijana aliyekuwa na ugomvi na kinyozi. Kijana alionekana amelewa na mwenye mawazo. Niliamuwa kumchukuwa ili nimsaidia pia nijisaidie mwenyewe maana mke wangu hatakubali nikishindwa kumaliza chakula.


Kijana alikubali na nilikwenda naye. Bahati nzuri mke wangu alionekana kumkubali kijana kwa ucheshi wake. Roho ya wivu ilianza kunijia ila sikuwa na wasi sana maana nilitambuwa kuwa ijana ataondoka kesho yake asubuhi. Tulipofika nyumbani mke wangu aliwa jikoni mimi na kijana tuliendelea kufurahi na kuzungumza mengi sana. Chakula kilivyoiva ndipo tukaanz akula kwa pamoja na kwa furaha ya hali ya juu. Na hapo ndipo tukio la mauwaji haya ulioshuhudia leo limeanzia. Kijana alikabwa na mwiba wa samaki na kupoteza maisha. Tukampleleka kwa tabibi, tabibu akampeleka kwa muuza nyama, muuza nyama akampeleka mtaani, na mtaani akakutana na mlevi. na tukio likaelezwa kwa ufasaha zaidi kama walivyosimulia wenzake waliotangulia.


Baada ya mshona nguo kumaliza masimulizi haya mfalme akatamka kuwa amewasamehe wote waliohusika na mauwaji haya. Maana tukio hili linashangaza sana. Kisha mfalme akaagiza kinyozi aletwe haraka sana. Askari wawili na mshona nguo walikwenda kwa muandaaji wa ile shughuli ya jana kwenda kumchukuwa kinyozi. Punde kinyozi akaletwa mbele ya sultani. Kinyozi hakujuwa kwa lengo gani ameletwa mbele ya sultani. Kinyozi akaelezwa mlolongo wa tukio zima na namna ambavyo anahusika. Kinyozi alishangazwa sana na tukio zima la mauwaji. Kinyozi akatoa mafuta flani kwenye kichupa akamfunua maitina kumuweka kwenye paja lake.


Loo! Loo! Hakika kijana huyu uhai wake bado upo…! watu wote walishangazwa zaidi na maneno ya kinyozi. Kinyozi akampaka mafuta yale kwenye shingo yake, na kuchukuwa mkasi mrefu, kisha akaingiza kwenye koo la kijana. Looo! Kipande cha samaki na mwiba kikatoka. Kijana akapiga chafya na alirudi kuwa mzima. Kwa hakika tukio hili liishangaza zaidi ya maelezo. Sultani akaagiza tukio zima liandikwe vyema kwenye hazina ya Sultani Harun Ar-Rashid na lijifadhiwe vyema kwa vizazi vijavyo vipate kushuhudia.


Baada ya hapo Sultani akaamuru kusamehewa kila muhusika wa tukio. Pia akamteuwa kinyozi, tabibu na mshona nguo wafanye kazi zao ikulu na kuwafanya wawe watu wa karibu naye. Kuanzia siku hiyo Alikuwa akishauriana nao mmbo kadhaa na kuwafanya ni ndugu zake wa karibu. Kijana alitunukiwa mwanamwari mtoto wa Sultani. Tukio huili lilikuwa ni la kushangaza sana.


Baada ya Sheherazade kusimulia hadithi hii kwa Sultani Shahariar, Mdogo wake Dinarzade alionekana kuipenda sana. Kumbuka miezi mingi ilishhapita toka Shehrazade kuolewa na Sultani na kwa ufundi wa masimulizi Sultani hakufikiri tena kumuuwa. Dinarzade alitaka asimuliwe hadithi nyingine. Na hapo ndipo hadithi ya Aladini ikaanza kusimuliwa usiku ule.


#NB kama utakuwa umesahau jinsi mlolongo wa masimulizi haya ulivyoenda tembelea tovuti yetu. Utakuta mlolongo mzima toka hadithi ya kwanza kitabu cha kwanza hadi hapa tulipo.




           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 218


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

Jaribio la kwanza la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Alif lela ulela
Posti hii inakwenda kukusimulia hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hatma ya kijana mchonganishi
Soma Zaidi...

SIRI
Hii ni game ya maandishi bila ya kutumia vioneshi (graphics). Soma Zaidi...

UJUMBE WA SIRI KWENYE KITABU CHA AJABU
Soma Zaidi...

SIRI YA KIFO INAFICHUKA
Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU(A.S.): Ndoto ya nabii Yusufu
Mtume Yusufu(a. Soma Zaidi...

Ugeni wa dhati
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

NJE YA JUMBA LA KIFAHARI JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...