Navigation Menu



image

Jaribio la pili la aladini

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu

JARIBU LA PILI LA ALADINI

Kifo cha mchawi hakikuwa ndio mwisho wa majaribu ya Aladini. Ijapokuwa kilikuwa ni mwisho wa harakati za waziri mkuu. Maana sasa waziri alianza kujikombkomba kwa aladini na wameanza kuwa marafiki. Waziri hakufikiri tena kumfanyia ubaya Aladini. Lakini saa mchawi yule alikuwa na kaka yake. Huyo kaka yake alikuwa na nguvu sana za kichawi kuliko mchawi wa kwanza. Kama huyu alipogundua kifo cha kaka yake akaanz akufuatilia hasa nini kilitokea. Katika kufuatilia aligundua kuwa kuna pango la ajabu sana. Na hilo pango ndio chanzo cha kila kitu.

 

Jambo la kwanza mchawi alikwenda kwa waziri mkuu kwani alitambuwa ujio wa waziri kwa kaka yake. Alipofika akajitambulisha vyema na kueleza nia yake kuwa ni kuhakikisha kuwa Aladini anapotea kabisa kwenye uso wa dunia na kusibakie hata jina lake kwenye vitabu majarida wala kwenye fahamu za watu. Haya maneno yalikuwa mazito sana maana yalimaanisha kuwa aladini hataweza kukumbukwa tena punde tu baada ya kifo chake ama kupotea kwake. Na wala halitaonekana kaburi lake wala familia yake. Na watu wot ewaliomfahamu watalisahau jina lake, na karatasi zote zilizoandikwa jina lake zitatoweka. Pango ambalo ndio kila kitu litatoweka pia.

 

Mchawi huyu akaanza kumfahamisha waziri kipolepole na kwa ufasaha zaidi. Mwanzoni waziri alionyesha kutokukubaliana lakini baadaye alikubali. Basi siku ilofata mchawi na waziri walitoka kuelekea pangoni waende wakaharibu kila kitu. Kitu kimoja walihitaji kule pangoni, nacho ni kitabu cha historia ya lile pango, nani hasa ndiye mmiliki, na vipi kulisambaratisha pango lile. Wakatiwao wakiwa na mawazo ya kuharibu kila kitu Aladini akajiwa na jini wa Mshumaa kwa haraka. Hhakika haikuwa kawaida kwa jini wa mshumaa kuja bila ya kuitwa, lakini leo amekuja mwenyewe. Aladini alishangaa sana.

 

“Aladini unatakiwa uondoke sasa hivi uende pangoni, ukakichukuwe kitabu cha kale, utakikuta kwenye kabati. Ni ruhusa kukisoma kitabu upendavyo lakini hakikisha haukusudii mabaya kuhusu mango na historia yake, kumbuka aladini hutaruhusiwa kuchukuwa chochote kutoka kwenye pango zaidi ya kitabu tu.” haya yalikuwa ni maneno machache ya jini wa Mshumaa. Aladini bila kuchelewa alitoka mapema sana Alfajiri na kwenda pangoni. Kwa kutumia pete ya kichwawi aliweza kufungua mlango wa pango. Hakukuwa na mabadiliko sana toka siku ile aliyokuja kwa mara ya mwisho. Karibia vitu vyote vilikuwa sawa. Ila mara hii chanzo cha mwangaza wa ndani kilikuwa ni mzinga wa nyuki. Hii ni tofauti na mwanzo ambapo chanzo cha mwangaza kilikuwa ni mshumaa wa kichawi.

 

Aladini hakufanya makosa aliendelea moja kwa moja mpaka kwenye likabati kubwa. Kabati lilikuwa ni la dhahabu lote lililowekwa vioo vya Almasi. Hakikuwa kikionyesha ndani kioo hiki. Miguu ya kabati ilikuwa ni ya mbao zilizo ngumu nyekundu sana. Aladini alishangaa kukuta kuwa kabati halikuwa na kufuli. Mwanga hafifu wa rangi zenye kubadilishana zilikuwa zikitoka ndani ya kabati katika sehemu ya chini. Aladini bila ya kupoteza muda aliingiza mkono wake na kukinyakuwa kitabu. Aladini hata hakutaka kuchunguza mambo mengi zaidi. Aliamini huenda yakamshinda.

 

Aladini wakati anataka kurudi aliona ule mwangaza unaongezeka. Aladini roho ilimsukuma kurudi tena. Aladini akaanza kuchungulia, Loo! Ilikuwa na vijiwe viwili vya duara. Vijiwe vilikuwa na rangi nzuuri sana. Hakika viliweza kuvutia vyema kwenye macho ya mtazamaji. Aladini alifikiri mwanga wa vijiwe hivi ungetosheleza kungarisha nyumba yake yote. Aladini tamaa zikaanza umshinda akatamani kuviiba vijiwe vile. Akakusudia haza kuvichukuwa, Aladini aliponyoosha mkono kuvishika vijiwe, alihisi kama shoti ikimpiga na hapo kauli ya jini wa mshumaa ikajirudia “kumbuka aladini hauruhusiwi kutoka na kitu chohote” Aladini alitambuwa hili ni jaribio amepewa, na asipokuwa makini atafeli.

 

Haraka sana alitoka nje ya pango huku moyo ukaenda mbio. Aladini akatumia nguvu za jini wa pete na kumwambia kuwa afunge pango ili asiweze kuingia mtu yeyote. Kisha Aladini akapotea zake kwenda nyumbani. Nyuma ya kuondoka kwa Aladini mchawi na waziri waliwasili. Mchawi alijitahidi sana kuingia kwenye pango lakini alifeli. Hatimaye kwa kutumia nguvu zake alitambuwa kuwa Aladini alishakuwepo kwenye pango na kitabu walichokitaka tayari amekichukuwa. Waziri alikuwa na hamu ya kujuwa ni nini hasa kimeandikwa kwenye kitabu kile?. hata mchawi alikuwa na mawazo haya ijapokuwa alikuwa na ufahamu kidogo kwa ujumla kitamu kilimuhusu nanai na ni kwa nini






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1215


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Sababu ya kukatwa vidole gumba
KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA? Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaka wa pili
Soma Zaidi...

Historia ya zamani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Kukatwa mkono na kuurithi utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA TANO WA KINYOZI
Soma Zaidi...

BINTI MZURI ASIYETAMBULIKA
BINTI HUYU NI NANI? Soma Zaidi...

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

MUENDELEZO WA HADITHI YA MSHONA NGUO
Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

HISTORIA YA PANGO, ALADINI NA KITABU
Soma Zaidi...

JARIBIO LA TATU LA A LADINI
Soma Zaidi...