image

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI



Kaka yangu wa nne alikuwa ni muuza nyama naani bucha. Alikuwa ni maarufu sana katika mji na alipendwa sana na watu. Kaka alikuwa akiuza nyama ya mbuzi na kondoo. Wakati mwingine alikuwa akiuza nyama za ndege kama kanga kwani alikuwa akifuga kanga wengi sana kwake. Kaka alikuwa ni mtu wa heshima na mwenye adabu sana. Naweza kusema badala ya mimi kuwa na heshima katika makaka zangu huyu ndiye nayefata. Bucha la kaka lilikuwa ni kuwa, na lilikuwa likitowa huduma kwa watu wengi na wakubwa katika serikali. Ilifikia wakati kaka alikuwa anapata tenda ya kutowa kitoweo katika masehrehe makubwa. Pia wakati mwingine kitoweo cha mfalme kilikuwa kikinunuliwa kutoka kwake.


Siku moja alikuja mzee mmoja mweusi sana, anayeonekana ni mzee wa makamo na mwenye ndevu ndefu. Akiwa amepakata mkoba wake mkono wa kusoto na mkono wa kulia amebeba kikapu cha rangi ya kahawia. Alikuwa mrefu kama futi tano na robo. Ndevu zake silikuwa ndefu na zilizoshikamana vyema na zilizolingana. Zilikuwa zikipepea kufuatana na uelekeo wa upepo katika hali ya kupendeza. Mzee alikuwa akitembea kwa mwendo wa polepole huku kichwa cheke kikielelea kuelekea chini kana kwamba yupo kwenye mawazo mazito. Alikuwa akitembea miguu yake yote inanyooka kuelekea mbele, na alionekana kuwa na mkono madhubuti na yenye nguvu.


Mzee yule baada ya kutoa salamu alifika dukani kwa kaka na kuchukuwa paja zima la mbuzi. Kisha akatowa vipande 5 vya dhahabu iliyosafi. Kaka alichukuwa dhahabu na kuibusu kucha akaziweka kwenye sanduku la mbao. Wiki ilofata mzee yule kaaja tena na kuchukuwa paja na kuacha vipande vitano vya dhahabu. Kaka naye akaziweka kwenye sanduku la mbao. Mzee yule alifanya vie kwa masiku kadhaa inapata hata ieze mitatu. Kisha kaka akaamuwa sasa atoe zile dhahabu ili apate kununuwa nyumba kubwa katikati ya mji afunguwe tawi lingine.
Kaka kwa mbwembwe na furaha akafunguwa sanduku apate kutowadhahabu zake. Loo!!! alishangaa sana kukutana na makaratasi matupu. Kaka alikuta rundo la makaratasi kwenye sanduku lake la dhahabu. Kaka akaamini kuwa yule mzee amemfanyia mchezo. Alilia sana kaka na watu wakajaa kujuwa nini kinaendelea. Kaka akawaeleza kila kilichotokea. Kitu cha ajabu hakuna aliyemfahamu huyo mzee na hakunaaliyewahi kumuona. Hata watu waliokuwa wakiuza bidhaa zao jirani na kaka walidai kuwa huyo mzee hawamjui na hawajwahi kumuona hata mara moja. Kaka alifadhaika sana na asijuwe nini afanye.


Ilimchukuwa kaka muda wa siku tatu hata kuhudhurisha mawazo yake na kukaa vyema kisaikolojia. Kaka akaamuwa kujifanya kama hakuna kilichotokea lengo ni kumsubiri yule mzee aje tena. Kama kawaida haikupita muda mrefu yule mzee akaja. Kaka kwa jadhba na hasira akamkamata vilivyo yule mzee na kuanza kuita watu. Watu walipokusanyika kaka alaianza kuto wamaneno machafu kumsema yule mzee. Watu wakaanza kumzogoma yule mzee kwa kitendo cha wizi na utapeli alioufanya. Baadhi ya watu wenye busara wakataka mzee apewe fursa ya kuweza kujitete kwanza. Hapo mzee akaanza kufungua mdomo kama ifuatavyo.


Mzee alianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyempa umri mrefu hadi kufikia siku ile. Kisha akaendelea “nashangaa mnanizogoma mimi kwa kuwa eti nimemtapeli huyu kijana. Mimi sikutapeli ina nimetaka kuwalipia nyinyi, kijana huyu hauzi nyama za mbuzi na kondoo bali anauza nyama za watu”. wat waaanza kuzogoma kisha kaka akapewa nafasi aseme neno. Kaka akanena “Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu aliye juu, hakika mzee huyu anazungumza uongo, na kama mimi nauza nyama za watu na ikikutwa nyama ya tu dukani kwangu shibgo yangu itakuwa halali kwenu”.


Pale watu wawili wenye busara wakaongozana na mzee pmamoja na kaka kwenda kuhakiki maneno a mzee. Loo! Walikutana na nyama za watu zimetundikwa. Kaka alitabuwa kuwa uu I uchawi ama mazingaombwe aefanyiwa. Alijitahidi kujitetea lakini wapi. Kaka alichukuliwa na kupelekwa kwa kadhi. Kwa kadhi kaka alipatikaniwa na hatia ya kuuza nyama za watu. Hata hivyo haikuthibitika kama yeye ndiye maeuwa wale watu ama kuna mtu anamletea nyama hizo. Pia hakuna uthibitisho kama wale walikuwa ni watu wa mji ule ama mji ganai. Pia hakujapatikaniwa taarifa za kupotea kwa watu katika hali za utatanishi.


Ijapokuwa kaka alikuwa na hatia ya kuuza nyama za watu lakini hakuwa na hatia ya kuuwa mtu ama watu hivyo akaamriwa apigwe viboko 80 kisha afilisiwe na akamishwe mji. Aka alitandikwa viboko 80. na kwa bahati mbaya kiboo kilimtuwa jichoni na kupasua jicho. Kaka akawa hana jicho moja huku hajiwezi akaenda kutupwa mbali na hakutakiwa kurudi tena mji ule. Nilipozipata habari nilikwenda kwa siri kumchukuwa. Mpaka kufika hapa kinyozi akamaliza hadithi ya kaka yake wa nne. Kisha akaendelea na hadithi ya kaka yae wa tano.







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 241


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI
Soma Zaidi...

Jaribio la pili la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

hatima ya kinyozi
Soma Zaidi...

JARIBIO LA TATU LA A LADINI
Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa tano wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kukatwa mkono na kuurithi utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Nje ya jumba la kifahari la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Hadithi ya kinyozi kaa wa tatu
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa kwanza wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Penzi la Mitihani
MTIHANI PENZINI Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...