picha

dalili za mimba changa na siku ya kupata mimba

Jifunze namna ya kuthibitisha dalili za ujauzito kuwa ni za kweli. Tambuwa namna ya kupima mimba na muda mujarabu wa kupima

dalili za mimba changa na siku ya kupata mimba



JE NITAHAKIKISHA VIPI KAMA NINA UJAUZITO?




Hili ni swali la msingi kabisa, maana unaweza kuwa na dalii za ujauzitio lakini si ujauzito, ama unaweza kuwa ujauzito lakini ukipima huoni kitu. Sasa nini tufanye. Njia pekee ya kuhakiki kama ni ujauzito ama sio ni kupima. Unaweza kutumia kipimo cha mkojo ukiwa nyumbani ama kwenda kupima hospitali.



Kama utatumia kipimo cha mkojo fika duka la dawa na hakikisha unapewa kipimo kilichokuwa hakiku expire. Pata maelekezo kutoka kwa uuzaji kama ni mara yako ya kwanza. Pia maelekezo utaweza kuyakuta kwenye hiko kipimo ila lugha inaweza usielewe. Kipimo hili kinafanya kazi kwa kuangalia uwepo wa kemikali ambazo huzaliwa wakati wa ujauzito. Endapo zitakuwepo kipimo kitaonyesha kuwa ni mjamzito.



Sasa ni muda gani unafaha kupima?
Ni vyema kupia wiki mbili baada ya kukosa hedhi. Endapo utapima wiki moja baada ya kukosa hedhi ama utapima mapema zaidi kuna uwezekano kuwa hutapata majibu kama ni mjamzito. Hivyo inashauriwa sana kusubiri baada ya wiki mbili toka kukosa hedhi ndipo upime. Kama utakwenda kupima hospitali haina shida hata ukiwahi maana zipo njia nyingi wanaweza kutumia.



Nina dalili za uajauzito lakini nikipima sina?
Hili ni katika maswali ambayo wanawake wengi wamekuwa wakiuliza. Inatokea anazo dalili zote za ujauzito lakini akipima hakuna kitu. Kuna sababu nyingi juu ya swala hili. Kabla ya kuendelea na somo hili zaidi, wacha nikufahamishe kuwa, yafuatayo yanaweza kusababisha usione ujauzito kwenye kipimo:-



1.Kama umepima mapema kabisa
2.Kama kipimo ni kibovu
3.Kama umekosea namna ya kupima
4.Kama huna ujauzito
5.Homoni za ujauzito hazipo za kutosha kwenye mkojo.



Hizi ni katika sababu tu zinazotokea hasa wakati wa kupima. Sasa wacha tuingie katika somo hili kitaalamu zaidi. Ni kwa nini unaweza kupata dalili za uajauzitio zilizotaja hapo juu lakini ukipima huna hata ujauzito?. nitaangalia hoja kuu tano za kutokea kwa hali hizi kama ifuatavyo:-



1.Kukosa Hedhi
Kukosa hedhi ni dalili ya ujauzito, lakini haimaanishi kuwa ni lazima utakuwa mjamzito. Kwani mwanamke anaweza kukosa hedhi kwa moja ya sababu zifuatazo:-
A.Uwiyano usiosawa wa homoni (hormene imbalance)
B.Madawa
C.Maradhi katika ovari
D.Magonjwa kama ya PID
E.Misongo ya mawazo
F.Vyakula
G.Njia za uzazi wa mpango



2.Kuuma kujaa na kuvimba kwa matiti. Hii inaweza kuwa ni dalili ya ujauzito.akini pia hali hii inaweza kusababishwa na mambo kadhaa ambayo yanaweza yakakufanya uhisi ni mjamzito.kwa mfano:-
A.Kuwepo kwa uvimbe kwa ndani (breast sore)
B.Kuwepo kwa shida katika tishu za matiti (fibrocystic breast tissue)
C.Kwa wakati mwingine mazoezi makali yanaweza kusababisha hali hii.
D.Uvutaji wa sigara
E.Pia uwiyano mbaya wa homoni (hormone imbalany)



3.Maumivu ya kichwa na kichefuchefu yanaweza kusababishwa pia na sababu nyingine. Ijapokuwa inakadiriwa kuwa asilimia 70 ya kichefuchefu ni ujauzito. Mengine yanayoweza kusababisha ni misongo ya mawazo, vyakula, maradhi na vidonda vya tumbo, sumu katika vyakula na mengineyo.



4.Maumivu ya tumbo na kutokwa na damu kidongo (cramping and spotting). dalili hizi zinawezakufana na sana na mwanzoni mwa hedhi, dalili hizi hazimaanishi moja kwa moja utakuwa na ujauzito. Kwani huwenda pia zikasababishwa na uwiyano mbaya wa homoni (hormone imbalance), matumizi ya baathi ya njia za uzazi wa mpango, matumizi ya madawa, misongo ya mawzo, mashambulizi ya bakteria mwilini (PID) na maradhi yanayojulikana kama uterine fibrinoid.



5.Uchovu, nadhani hapa sina haja ya kuzungumza sana maana kila mtu anafahamu kuwa uchovu unaweza kusbabishwa na mambo mengi sana kama mazoezi, kazi, maradhi mengine.



Hivyo kama unapata dalili za ujauzito na kila ukipima hakuna kitu vyema kufika kituo cha afya kwenda kucheki vyema huwenda kuna kitu haki[o sawa.



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views 5424

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Sababu za kupasuka kwa mfuko wa kizazi

Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.

Soma Zaidi...
Huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja.

Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja, aina hiyo ya mimba kwa kitaalamu huitwa complete abortion.

Soma Zaidi...
Dawa ya chango na dawa maumivu ya tumbo la hedhi

Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango.

Soma Zaidi...
Faida za uzazi wa mpango kwa jamii

Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa jamii, tunapaswa kujua kuwa uzazi wa mpango ukitumiwa vizuri na jamii nayo inapata faida kwa hiyo zifuatazo ni faida za uzazi wa mpango kwa jamii.

Soma Zaidi...
Mabadiliko ya uzito kwa mjamzito

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya uzito kwa mjamzito, hii ni hali ya kubadilika kwa uzito kwa Mama akiwa na Mimba

Soma Zaidi...
Aina mbalimbali za mimba kutoka.

Post hii inahusu zaidi aina mbalimbali za mimba kutoka, hizi ni jinsi mimba inavyoonyesha dalili za kutoka na nyingine zinaweza kuonyesha dalili Ila kwa sababu ya huduma mbalimbali za kwanza hizo mimba zinaweza kudhibiiwa na mtoto akazaliwa.

Soma Zaidi...