picha

MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)

Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik.

MTAMBUE MDUDU MBU ILI UWEZE KUJIKINGA NA UGONJWA WA MALARIA (yajuwe maajabu makubwa ya mdudu mbu)

PAMBANA NA MALARIA KWA KUMTAMBUA MDUDU MBU (MOSQUITO)

 

Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.

 

Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kilo 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimeng’enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.

 

Kabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.

 

Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.

 

Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.

 

Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 2556

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Huduma kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa

Posti hii inahusu zaidi msaada kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa, ni huduma anayopewa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa.

Soma Zaidi...
VIRUSI VYA KORONA AU CORONA (CORONAVIRUS)

Virusi vya korona ni katika aina za virusi ambavyo asili yake ni kutoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu.

Soma Zaidi...
Typhoid husabisha mwili kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na joint za miguu kuchoka

Dalili za typhid zinapasa kuangaliwa kwa umakini. Bila vipimo mtu asitumie dawa za tyohod, kwanu dalili za tyohid hufanana na daliki za maradhi mengi.

Soma Zaidi...
je..! naweza kuambukizwa fangasi kwa kujamiiana na mtu mwenye fangasi?

Je ukifanya mapenz na mtu mweny aina hi ya fangasi na akawa anayo maambukizi ya ukimwi.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa surua kwa watoto.

Surua ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na homa na upele mwekundu, unaotokea utotoni. Wakati mtu aliye na virusi akikohoa au kupiga chafya, matone yaliyoambukizwa huenea angani na kutua kwenye sehemu zilizo karibu. Mtoto anaweza kupata virusi kwa ku

Soma Zaidi...
Fahamu sababu za ugonjwa unanipeleka Kuvimba kwa mishipa ya Damu

posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Kuvimba kwa Mishipa ya Damu hujulikana Kama Behcet amboyo husababisha dalili nyingi ambazo hapo awali zinaweza kuonekana kuwa hazihusiani. Dalili na ish

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa macho

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa macho, ni ugonjwa ambao ushambulia zaidi sehemu za nje za macho ambazo kwa kawaida uitwa conjunctiva na cornea hizi sehemu zikipata maambukizi zisipotibiwa mapema uweza kusababisha upofu kwa mgonjwa.

Soma Zaidi...
Maambukizi kwenye mrija wa mkojo(urethritis )

Posti hii inahusu zaidi maambukizi kwenye mrija wa mkojo, maambukizi haya usababishwa na virusi na bakteria.

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa upele

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa upele, ni dalili au mwonekano wa mgonjwa wa upele.

Soma Zaidi...
Dalilili za Ngozi kuwa kavu

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ngozi kuwa kavu si mbaya, lakini inaweza kusumbua na isipendeze, ikitengeneza mistari laini na Mikunjo.

Soma Zaidi...