KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)
Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika.
KWA NINI MBU HAWEZI KUAMBUKIZA HIV (UKIMWI)
Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika. Na mradhi mengine kama malaria na homa ya bonde la ufa. Lakini kuna jambo linaumiza sana fikra za wasomaji. “kama mbu wanaweza kuambukiza maradhi hayo ya virusi, sasa ni kwa nini mbu hawezi kuambukiza HIV?”
Kwa hakika swali hili linasumbua fikra za watu wengi sana. Tafiti nyingi za kisayansi zimefanywa ili kuthibitisha majibu sahihi na kuwaridhisha waulizaji. Ukweli ni kuwa mbu katu hawezi kueneza HIV. Na huu ni ukweli ambao haupingiki katu, lakini sasa ni kivipi?. katika makala hii nitakueleza jibu la swali hili katika namna tatu:-
- Mdomo wa mbu una sehemu kuu 6, katika hizo 6 nne hutumika kutoboa ngozi ya mwili wa kiumbe anachotaka kunyonya damu. Na sehemu 2 zilizobakia ni kwa ajili ya kunyonya damu. Katika sehemu 2 hizo mojawapo ni kunyonya damu na nyingine ni kupeleka mate kutoka kwenye mwili wa mbu na kuelekea kwenye mwili wa kiumbe kinachonyonywa damu. Mate haya hutumika kwa kuifanya damu isigande.
Hivyo basi kitu ambacho kinatoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu ni mate ya mbu tu, na si damu, kwani damu haiwezi kutoka kutoka kwa mbu kwenda kwa kiumbe kinachonyonywa. Tafiti zinaonesha kuwa mate kati hayawezi kuambukiza ukimwi, hata yawe ya mtu. Hivyo basi hata kama mate ya mbu yataingia kwa mbu kati hayawezi kuambukiza ukimwi kkama amebeba virusi.
- Virusi vya HIV vikifika mwilini mwa mbu vinaliwa na kupotea kabisa. Virusi vya HIV ili viendelee kuzaliana vinahitaji kupata T seli (T cell), lakini mbu hana seli aina hii. Hivyo virusi vinapofika kwa mbu, vinaliwa pamoja na damu na kupotea kabisa. Kwa sababu hii hakuna uwezekano wa virusi vya HIV kuingia kwenye mate ya mbu ambayo ndio huenda kwa kiumbe kinachonyonywa damu. Hii inaonyesha kuwa katu HIV haiwezi kusambazwa kwa mbu.
- hata kama virusi vya HIV vitaweza kuingia kutoka kwa mbu kwenda kwa kiume kinachonyonywa damu (japo jambo hili haliwezekani) hakua uwezekano wa kuambukiza HIV. Tafititi zinaonyesha kuwa ili damu ama mate ya mbu yasambaze HIV inahitajika ang’ate si chini ya mara milioni 10. Jambo hili kisayansi haliwezekani. Pia kummeza mbu aliyebeba HIV HAIWEZEKANI KUSAMBAZA HIV. Haka akipasukia kwenye jeraha la mtu katu damu yake haiwezi kuambukiza HIV.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 kitabu cha Simulizi ๐2 Bongolite - Game zone - Play free game ๐3 Madrasa kiganjani ๐4 Simulizi za Hadithi Audio ๐5 Dua za Mitume na Manabii ๐6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Faida za kiafya za kufunga
Simulizi yetu ya leo tutajifunza kuhusu faida za kiafya za kufunga kwa mtazamo wa kitabibu, kama anavyoeleza daktari. Tutaangalia namna kufunga kunavyoathiri na kusaidia viungo na mifumo mbalimbali ya mwili. Somo letu la leo litahusuโฆ faida za kiafya za kufunga katika figo, moyo, ini, mfumo wa kinga, kisukari, presha ya damu na mmengโenyo wa chakula.
Soma Zaidi...Kitabu Cha Darsa za Afya
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Ijue timu ya upasuaji
Posti hii inahusu timu ya upasuaji hii ni timu ambayo inahusika katika chumba cha upasuaji, kwa sababu ya kutunza usafi na usalama chumba hiki kinapaswa juwa na timu ya watu wanne na walio na elimu kuhusu kazi hiyo.
Soma Zaidi...