Jifunze kuhusu Protini, Fati, Wanga na kazi zao mwilini na vyakula vinavyopatikaniwa kwa wingi

Jifunze kuhusu Protini, Fati, Wanga na kazi zao mwilini na vyakula vinavyopatikaniwa kwa wingi

Pritini, Fati,Wanga na Maji

bongoclass-afya

TAMBUA PROTINI, FATI, WANGA NA MAJI

PROTINI, FATI, WANGA NA MAJI



IJUWE PROTINI NA KAZI ZAKE MWILINI
YALIYOMO
Katika makala hii tutakwenda kuona
1.Maana ya protini
2.Vyakula vya protini
3.Faida za protini
4.Upungufu wa protini
5.Ulaji wa protini kupitiliza


MUKTASARI KUHUSU PROTINI.
Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki 'proteios' likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe 'nutrients' ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 18338 na Mkemia kutoka Swedih J'ns Jacob Berzelius.


Pritini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng'enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)


Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes


Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.


VYAKULA VYENYE PROTINI
Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.


Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-
1.Samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini. Ulaji wa samaki umekuwa ni chanzo kizuri cha protini hasa kwa wakazi wa maeneo ya baharini na maeneo ya pwani ama mitoni, mabwawa na maziwa. Tunaposema samaki hapa wanaingia mpaka dagaa, kaa, kaji, kamongo, perege, mikunga, papa na samaki wengine. Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na fati


2.Mayai; mayai ni katika vyanzo vikubwa vya protini. Karibia watu wengi hujipatia protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa limekaangwa, chemshwa ana la kuchoma. Pia unaweza kula yai bichi kama wafanyavyo baadhi ya watu. Ulaji wowote kati ya niliotaja unaweza kukupatia protini. Ila hakikisha kama umelikaanga ama kulichoma halikauki sana likawa kama chapati iliyokauka, upishi huu unaweza kuathiri virutubisho.


3.Maziwa; maziwa ni katika vyanzo vikuu vya protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata ya ng'ombe. Tofauti na kutupatia protini maziwa pia ni chanzo cha vitamini na fati. Maziwa ni katika vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemshha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.


4.Nyama; tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Nyama ni katika vyanzo vizuri vya protini. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe tunaweza kuzipata kwa kula kuku, baadhi ya samaki, kaa. Nyama nyekundu tunaweza kupata kwa kula mbuzi, kondoo na karibia wanyama wengi. Nyama pia ni chanzo kizuri cha fati mwilini. Ulaji wa nyama unaweza kuleta athari za protini kwa muda mchache sana.


4.Mimea aina ya kunde na nafaka; mimea jamii ya kunde hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunnde na maharagwe na mimea jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Watu wenye kipato cha chini mimea hii ni chanzo chao cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo katika aina nyingi yapo ya soya na aina mbalimbali. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.


5.Mboga za majani. Kwa kiwango kilicho kidogo tunaweza kupata protini kwa kula mboga za majani. Mboga za majani oekee hazitoshelezi kutupatia kiwango cha protini kinachohitajika. Kwa wale ambao hawali chama (vegetarian) wapo ambao hawali nyama lakini wanakula mayai na maziwa hawa wanaweza kujipati protini kwenye mayai na maziwa. Lakini kwa wale ambao hawali nyama, maziwa wala mayai watahitajika kupata vyamzo vingine mbadala vya protini yaani watumie protini za kutengeneza japo miongoni mwazo zipia mbazo zinatengenezwa kwa wanyama.


6.Vyanzo vingune: tofauti na vyanzo vya protini nilivyotaja hapo juu lakini pia kuna vyanzo vingine kama ulaji wa senene na kumbikumbi na wanaofanana. Kuna baadhi ya jamii zinakula senene hasa jamii zinazopatikana maeneo ya kagera. Kwao senen ni chanzo kizuri sana cha protini. Kumbikumbi nao hupatikana maeneo mengi na jamii nyingi zinatumia chakula hiki.


KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI
Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini.
Kazi za protini mwilini:-
1.Kujenga mwili;
2.Kupona kwa vidonda na majeraha
3.Kutengeneza antibody (kinga za mwili)
4.Kutengeneza hemoglobin (chembechembe zaseli nyekundu za damu)
5.Kutengeneza enzymes zinatumika katika kumeng;enya chakula
6.Kutengeneza homoni
7.Kuthibiti kichakati na shughuli za ndani ya seli
8.Huhusika katika kutengeneza tishu (nyama na misuli) ndani ya mwili
9.Nywele, kope, nyusi, vinyweleo na kucha hutokana na rotini


1.Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.


2.Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.


3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.


4.Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge'enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng'enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.


5.Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.


6.Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.


UPUNGUFU WA VYAKULA VYA PROTINI
Kama tulizoona faida za protini ndani ya miili yetu basi pia itambulike kuwa kuna hasara kubwa za kiafya endapo mtu atashindwa kupata protini za kutosheleza ndani ya miili yetu. Hapo chini nitakuorodheshea tu baadhi ya madhara ya kukosa protini ya kutosha:
1.Kudumaa na ukuaji hafifu wa mtoto
2.Kypata kiriba tumbo
3.Kupata kwashiakoo
4.Misuli na nyama kustokijazia vya kutosha
5.Kukosa nguvu ya kutoka kufanya kazi
6.Kukonda na kudhoofu


ULAJI WA PROTINI KUPITILIZA
Kwa upande wa pili ulaji wa protini nje ya kiwango unaweza kuleta athari hasi katika afya ya mlaji. Zifuatazo ni madhara ya kula vyakula vya protini kupitiliza
1.Kuongezeka kwa uzito mwilini
2.Kupata tatizo la kukosa chookuharisha
3.Kupungua kwa maji mwilini
4.Kupata matatizo ya moyo
5.Kuathirika kwa fogo
6.Hatari ya kutengengezwa kwa seli za saratani mwilini


VIRUTUBISHO VYA WANGA
Wanga ni moja kati ta virutubisho vikuu vitatu, vingine ni fat na protini. Kazi kuu ya wanga ni kutupatia nishati ama nguvu. Wanga ni katika sukari ambazo zinapatikana kwenye vyakula na ndani ya miili yetu. Tunaweza kupata virutubisho hivi kwenye vyakula na mimea.


Kazi za wanga
1.Kazi kuu ya wanga ni kutupatia nguvu yaani nishati
2.Husaidia katika kuvunjavunja fati mwilini
3.Hupunguza matumizi ya protini kwa ajili ya kuzalisha nishati
4.Hutumika katika kutengenezea bidhaa na madawa


YAKULA VYA WANGA
1.Mahindi
2.Mtama
3.Mihogo
4.Viazi
5.Ngano
6.Mikate
7.Mtama
8.Mchele
9.Keki
10.Krosho
11.Karanga
12.Ndizi
13.Nyama
14.Mayai
15.Maziwa


Upungufu wa wanga
Endapo virutubisho vya wanga vitapungua mwilini athari zitakazotokea ni:-
1.kukosa nguvu ya kutosha
2.Kuwa dhaifu
3.Mwili utashindwa kufany akzi vyema



FATI, MAFUTA NA LIPID
Fati ni moja kati ya virutubisho vikuu vitatu ambavyo ni wanaga an protini. Fati imetengenezwa na chembechembe za kaboni na haidrojen. Fati, mafuta na lipid ni maneno mawili yanayohusiana lakini kuna utofauti kidogo. Tunaposema lipid tunamaanisha fati na mafuta. Tunaposema fat tunamaanisha lipid iliyo katika hali ya yabisi (kitu kigumu) na tunaposema mafuta ni lipid iliyo katika hali ya kimiminika. Lakini mara nyingi tunaposema fati tunajumuisha vyote yaani lipi na mafuta.


Kazi za fati mwilini
1.Husaidia katika utengenezwaji wa nishati mwilini
2.Husaidia katika kuipa joto miili yetu
3.Husaidia katika kulinda sehemu za ndani za miili yetu
4.Husaidia katika utoaji wa taarifa mbalimbali ndani ya mwili
5.Husaidia protini kufanya kazi zake vyema
6.Husaidia katika ukuaji wa kiumbe
7.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
8.Husaidia katika mfumo wa uzalianaji


Vyakula vya fati
1.Mapalachichi
2.Giagi
3.Maziwa
4.Mayai
5.Karanga na jamii za karanga kama korosho
6.Mbegu za chia
7.Samaki
8.Choklet
9.Nazi
10.Nyama
11.Maharagwe ya soya
12.Alizeti



Upungufu wa fati
1.Kukauka kwa ngozi na ukurutu
2.Mupata maambukizi ya mara kwa mara
3.Kupona kwa vidonda kuliko hafifu
4.Kuchelewa kukua cha watoto



MAJI
Maji ni kimiminika kilichotokana na muunganiko wa haidrojen na oksijen. Karibia asilimia 90 ya seli ni maji. Na karibia asilimia 50 - 80 ya mwili wa kiumbe ni maji. Pia anakadiriwa kuwa asilimia 60 ya uzito wa kiumbe ni maji. Kiasi cha maji unayotumia inategemea na mambo mengi kama, hali ya hewa, shughuli unazozifanya, ama hali ya afya.
Faida za maji mwilini
1.Kulainisha viungo
2.Husaidia katika utengenezwaji wa mate na makamasi
3.Husaidia katika usafirishwaji wa oksijeni mwilini
4.Huboresha afya ya ngozi
5.Huboresha afya ya ubongo, ugwe mgongo na milango ya fahamu
6.Husaidia katika kupunguza joto
7.Mfumo wa mmengenyo wa chakula unategemea maji
8.Husaidia katika kuondosha ushafu ndani ya mwili
9.Hutdhibiti shinikizo la damu
10.Huzuia uharibifu wa figo
11.Husaidia katika kupunguza uzito


Upungufu wa maji
Upungufu wa maji unaweza kusababisha mambo yafuatayo:
1.maumivu ya kishwa mara kwa mara
2.Ngozi kukauka
3.Miwasho
4.Homa
5.Mkojo kuwa na harufu kali
6.Maambukizi ya mara kwa mara
7.Uchovu
8.Kiu


Vyakula vyenye maji kwa wingi
1.Tikiti
2.Tango
3.Nanasi
4.Machungwa
5.Madanzi
6.Mapensheni
7.Miwa
8.Mapapai
9.Mastafeli
10.Matunda damu
11.Komamanga



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 184

Post zifazofanana:-

FAIDA ZA MATUNDA MBALIMBALI
1. Soma Zaidi...

MALIPO YA WEMA NI WEMA
Download kitabu Hiki Bofya hapa MALIPO YA WEMA NI WEMA Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Soma Zaidi...

English tenses test 005
Soma Zaidi...

Yunus(a.s) Kulingania Uislamu kwa Watu Wake
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu mapunye
DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo. Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 03
Soma Zaidi...

TONGE LA MWISHO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KWISHA KWA CHAKULA Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa. Soma Zaidi...

Kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni Ushahidi Mwingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w):
(v)Kukosolewa Mtume (s. Soma Zaidi...

HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme. Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri Dhidi ya Qur'an na Udhaifu Wake
i. Soma Zaidi...

Kuibuka kwa kundi la khawarij baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

STANDARD FOUR ENGLISH TEST 17
Soma Zaidi...