NASAHA ZANGU NNE KWAKO NDUGU YANGU
NASAHA ZANGU 4 KWAKO NDUGU YANGU
Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatu. Shukurani zote zimfikie Allah muumba wa dunia na ulimwengu. Rehema na amani zimuendee kipenzi cha Mtume wa Ummah wa mwisho mtume Muhammad (s.a.w). Ama baada ya hayo, Ewe ndugu yangu nimependa nikufikishie nasaha zangu hizi nne huenda zikakufaa. Zikikufikia nasaha hizi tafadhali shirikisha na wenzio kupata ujumbe huu. Hakuna atulipae kufanya kazi hii isipokuwa Allah.
- KATU USIYATAMANI MAUTI
Utangulizi:
Kifo hutisha sana na ni chenye maumivu makali yasiyoweza kuelezeka. Kwa hakika kifo kinatisha sana kwani utakapokufa katu hutoweza kurudi tena duniani. Ukweli ni kwamba watu wengi wanaogopa kufa, ijapokuwa wapo ambao inafikia hatua hawaogopi kifo kabisa, lakini pia inaweza kufikia hatua kwa baadhi ya watu mpaka wakakiomba kifo. Hii huwenda ni kutokana na shida na taabu walizo nazo. Lakini katika uislamu IMEKATAZWA KATU KUTAMANI KIFO. Makala hii ni darsa la Hadithi linalokwenda kukueleza yale ambayo Mtume (s.a.w) ameyasema kuhusu kutamani kifo, na ikifikia hatua bora mtu afe kwa shida alizo nazo ana kwa namna nyingine nini aseme.
Makala imeandika wa Al-Ustadh Rajabu Athuma na kusambazwa kwako katika tuvuti hii ya bongoclass. Unaweza kushea Elimu hii ya bure, iwe kama sadaka kwako na kuonyesha juudi zako katika kusambaza elimu ya dini. Kabla ya kuendelea na Darsa hii ningependa kukutangazia kwamba, darsa hizi ni za bure na unaweza kupata kitabu cha darsa hizi ukijisajili kwenye maktaba yetu. Pia tembelea tovuti hii kuna darsa nyingi za dini zinakusubiri.
SABABU ZA KUTAMANI MAUTI
Sifa njema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, sala na amani zimfikie kipenzi wa umma Mtume Muhammad (s.a.w). yeye na sahaba zake. Darsa letu hili tutaanzia na hadithi iliyopokewa kutoka kwa Abuu huraira kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Asitamani mmoja wenu Mautu (kifo) ima akiwa ni mwema kwani huenda akazidisha heri ama akiwa ni muovu huenda akatubia.
عنْ أبي هُريرة رضيَ اللَّهُ عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ : » لا يَتَمَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ إِمَا مُحسِناً ، فَلَعَلَّهُ يَزْدادُ ، وَإِمَّا مُسِيئاً فَلَعَلَّهُ يَسْتَعْتِبُ « متفقٌ عليه، وهذا لفظ البخاري
Kutokana na mafunzo ya hadithi hii kwa nza tunapata kujuwa kuwa:-
- Mtume wa Allah ametukataza tusitamani kufa yaani mauti.
- Tusitamani kufa kwa hali zozote tulizo nazo tukiwa ni wachamungu sana ama tukiwa ni waovu sanaa.
- Ukiwa mchamungu uhai wako unaweza kuutumia vyema na ukazidisha uchamungu hivyo ukapandisha daraja yako kwa Allah
- Ukiwa ni muovu unaweza kutumia fursa ya uhai uliyonayo na ukatubu na Allah akakusamehe na ukaweza kuipata pepo. Kwani Allah husamehe madhambi yote pindi mja akitumia toba ya kweli.
- Uhai ni wa thamani pindi tu ukiukosa hutoweza kufanya jambo lolote tena.
Mafunzo ya hadithi hii yapo wazi kabisa. Kwani kwa hakika swala la kutamani mauti sio jambo jema katika dini. Na katika mapokezi mengine hadithi hii imesema kuwa:
لا يَتَمَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ ، وَلا يَدْعُ بِهِ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَأْتِيَهُ ، إِنَّهُ إِذا ماتَ انْقَطَعَ عَمَلُهُ ، وَإِنَّهُ لا يَزيدُ المُؤْمِنَ عُمْرُهُ إِلاَّ خَيرا
Mtume s.a.w amesema “asitamani mmoja wenu mauti na wala asiyaombe mauti kabla hayajamjia kwani hakika pindi atakapokufa, amali zake zote zinakatika, na kwa hakika hautamzidishia muumini umri wake isipokuwa heri”.
Hadithi hii inazidi kutupatia funzo zaidi kuwa tusitamani kufa na si kutamani tu bali hata tusithubutu kufa, kwani kama tutapewa uhai zaidi na tukiwa wema huenda uhai wetu ukawa ni chachu ya sisi kuzidisha wema. Na kama tukiwa ni waovu huenda tukatubu. Hadithi zote mbili hizi zinatujulisha kuwa kifo hakitakiwi kukitamani wala kukiomba.
Kuna kitu kingine hapa kimeelezwa kuwa pindi tu mtu akifa amali zake zote zinakatika. Yaani kama ni muovu na hajatubia madhambi yake kwa Allah basi hatoweza tena kutubia, na kama ni mwema hatoweza kufanya tena mambo mema. Katika hadithi nyingine Mtume wa allah ameeleza kuwa”atakapokufa mwanadamu amali zake zote (matendo) hukatika isipokuwa matendo ya (amali) aina tatu SADAKA YENYE KUENDELEA, ELIMU YENYE KUPATISHA MANUFAA AU MTOTO MWEMA ATAKAYEMUOMBEA DUA”. haya ni katika matendo ambayo yataweza kutupatisha faida pindi tutakapo fariki.
IKIWA HUNABUDI ILA NI KUFA UFANYE NINI
Wakati mwingine mwanadamu anapata taabu na shida kama maradhi. Maradhi kama ya saratani na mengineyo. Inatokea mpaka mwanadamu kwa maumivu ayapatayo na maradhi yake si yenye kutarajiwa kupona basi kwa taabu na shida anaamuwa kuomba bora afe. Hili pia limekatazwa kwenye uislamu. Lakini mtua akiwa a hali kama hii ama hali ambazo zinafanana na hii na akiwa hana budi isipokuwa ni kufa na akawa anatamani bora afe, basi Mtume s.a.w ametufundisha amaneno ambayo tunatakiwa kuyasema:
وعن أنسٍ رضي اللَّه عنه قال : قالَ رسولُ اللَّه صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : لا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ لِضُرٍّ أَصَابَهُ فَإِنْ آانْ لابُدَّ فاعِلاَ ، فَلْيَقُل : اللَّهُمَّ أَحْيِني ما آانَتِ الحَياةُ خَيْراً لي ، وتَوَفَّني إِذا آانَتِ الوفاةُ خَيراً لي « متفقٌ عليه
Katia hadithi iliyopokewa na Anas kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa Amesema Mtume (s.a.w) kuwa “asitamani mmojawenu mauti kutokana na madhara yaliyompata, na ikiwa hanabudi (ila ni kufa ama kutamani mauti ) basi na aseme “ALLAHUMMA AHYINII MAA KANAT ALHAYAAT KHIRAN LII, WATAWAFFANII IDHAA KAANAT ALWAFAAT KHAIRAN LII” (“Ewe Mwenyezi Mungu nipe uhai ikiwa uhai ni bora kwangu na unifishe ikiwa kifo ni bora kwangu”
Hadithi hii inatufundisha maneno ambayo mtu ayaseme kumwambia Allah ikiwa hanabudi isipokuwa ni kuomba kifo. Ukiiangalia vizuri hadithi hii maneno haya yamegawanyika katika vipengele vitatu na kila kipengele kimebeba ujumbe mzito sana. Hebu tuangalie kwa ufupi kabisa hadithi hii vipi tuielewe kwa kupitia vipengele hivi:-
- Hadithi inatukataza kutamani mauti kwa madhara yaliyompata mtu kama maradhi, mabalaa, kufilisika ama kufiwa na mtu wa karibu. Haya yote yakikupata na ukiwa umekata tamaa kabisa badi Mtume anatukataza katu tusitamani kufa. Na ikiwa hakunabudi basi kuna dua yenye maneno ambayo tunatakiwa tuyazungumze kumbia Allah, maneno haya ypo katika sehemu mbili:-
- Kwanza kumwambia Allah akupe uhai, yaani aendelee kukubakisha ukiwa hai, lakini tu kwa sharti kuwa ikiwa uhai una heri zaidi kwako. Hii inamaana unamwambia Allah akuuwe au akupe mauti ikiwa uhai utakuwa na madhara kwako.
- Sehemu ya pili ni kumwambia Allah akufishe yaani akupe mauti ikiwa kufa ni bora zaidi kwako kuliko kuendelea kuwa hai.
KWA NINI IMEKATAZWA KUOMBA MAUTI (KIFO)?
Kama ukiangalia vyema hadithi tajwa hapo juu ni dhahiri kuwa kuomba mauti kumekatazwa kwa sababu kuu zifuatazo:-
- mtu akifa amali zake na matendo yake hukatika hivyo ni bora asiombe kifo ili aendelee kufanya amali.
- Mtu muov akiwa hai huenda akatubu
- Mwenye matatizo na taabu huenda kwa rehma za Allah akaondokewa na matatizo yake pindi akiwa hai
- Mtu mwema huenda akaendelea kufanya heri na kupandisha darja yake pindi akiwa hai
- Shida na taabu ni mitihani ya allah, huenda ukafaulu mitihani hiyo na kupandishwa daraja mwele ya Allah.
- Kukimbia tatizo sio njia njema, kinachotkiwa na kupambana na tatizo na si kuomba kufa ili kulikimbia tatizo.
- Huenda uhai ukawa bora zaidi kwako kuliko kifo.
MWISHO
Kwa kufunga darsa ni kuwa uislamu umekatiaza kuomba umauti, kujiuwa ama kuuwa. Leo hii kuna watu wanazidi kutumia dawa za kuuwa watu wakidai eti wanawapunguzia machungu ya maisha. Kuna madaktari wanathubutu hata kumaliza maisha ya wagonjwa kwa kigezo kuwa mgonjwa hatapona na akiendelea kuishi atakuwa kwenye maumivu tuu. Njia hizi zote haziruhusiwi kwenye uslamu.
Ndugu yangu Muislamu, sisi ni waislamu tuliojitolea kwa ajili ya Allah katika kufikisha ujumbe wa Allah. Hatulipwi na yeyote na katika kufanya kazi hii. Uaweza kutuunga mkono katika kuifanya kazi hii kwa kushea elimu hii, ama kuandika makala kama hizi na kututumia, ama kutusaidia kuediti na kuondoa makosa yote ya kielimu na kitaalamu katika tovuti hii. Kazi hii hutalipwa na mtu yeyote, sote tunajitolea kwa ajili ya Allah.
Unaweza pia kusoma darsa zetu nyingine kama:
- DARSA ZA DUA
- DUA MBALIMBALI ZA KILA SIKU
- DARSA ZA QURAN NA TAJWID
- DARSA ZA FUNGA
- DARSA ZA SIRA
- DARSA ZA FIQH
SUMMERY
Mauti yanaogopesha sana, kwani ni yenye kukatisha raha za dunia kwa wale waliokuwa wakifurahia raha zao. Lakini wapo watu ambao wanafikia hatua mpaka wanatamani kufa na hii ni kutokana na maradhi, shida taabu ama uchamungu walio nao. Haijalishi vyovyote vile lakini Mtume (s.a.w) amekataza kuomba ama kutamani kifo. Iwe uwe na matatizo ama uwe ni mchamungu sana.
Katika mapokezi ya Abuu huraira kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Asitamani mmoja wenu Mautu (kifo) ima akiwa ni mwema kwani huenda akazidisha heri ama akiwa ni muovu huenda akatubia.
عنْ أبي هُريرة رضيَ اللَّهُ عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ : » لا يَتَمَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ إِمَا مُحسِناً ، فَلَعَلَّهُ يَزْدادُ ، وَإِمَّا مُسِيئاً فَلَعَلَّهُ يَسْتَعْتِبُ « متفقٌ عليه، وهذا لفظ البخاري
Hadithi hii inataja baadhi tu ya sababu ambazo zinawafanya watu hata wakatamani mauti. Hadithi hii inatufundisha kuwa
- Mtume amekataza kutamani mauti
- Usitamani mauti hata ukiwa na mwema au muovu
- Uhai unaweza kukupa fursa akatubia madhambi kama ukiwa muovu
- Uhai unaweza kukupa furasa ukaongeza kufanya heri zaidi kama utakuwa mwema.
Lakini inaweza ikatokea kuwa kwa matatizo mtu aliyonayo kama maradhi yasiyotarajiwa kupona na yenye maumivu makali. Mtu akiwa katika hali kama hii bado anatakiwa katu asitamani kufa. Ila kuna maneno ambazo Mtume (s.a.w) ametufundisha kuyasema:
وعن أنسٍ رضي اللَّه عنه قال : قالَ رسولُ اللَّه صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : لا يَتَمَنَّيَنَّ أَحَدُآُمُ المَوْتَ لِضُرٍّ أَصَابَهُ فَإِنْ آانْ لابُدَّ فاعِلاَ ، فَلْيَقُل : اللَّهُمَّ أَحْيِني ما آانَتِ الحَياةُ خَيْراً لي ، وتَوَفَّني إِذا آانَتِ الوفاةُ خَيراً لي « متفقٌ عليه
Katia hadithi iliyopokewa na Anas kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa Amesema Mtume (s.a.w) kuwa “asitamani mmojawenu mauti kutokana na madhara yaliyompata, na ikiwa hanabudi (ila ni kufa ama kutamani mauti ) basi na aseme “ALLAHUMMA AHYINII MAA KANAT ALHAYAAT KHIRAN LII, WATAWAFFANII IDHAA KAANAT ALWAFAAT KHAIRAN LII” (“Ewe Mwenyezi Mungu nipe uhai ikiwa uhai ni bora kwangu na unifishe ikiwa kifo ni bora kwangu”
- NIZIPI FADHILA ZA KUSOMA QURAN?
Quran ni maneno ya Allah yaliyofunuliwa kwa mtume Muhammad (s.a.w) kwa kupitia Malaika jibril. Quran imetufikia sisi kwa hatua. Na duniani imeshuka kwa muda wa miaka 23 vipande vipande, sura kwa sura hata ikatimia yote yenye sura 114, aya 6236, yenye herufi 330,709 maneno 77,449. quran ni kitabu pekee ambacho usahihi wake unaweza kuthibitika kwa kutumia sayansi na teknolojia, ushahidi wa kihistoria juu ya mambo yaliyozungumzwa kuhusu kutokea kwake. Usahihi katika utoaji taarifa wake, muundo wa maneno yake na mengineyo mengi.
Wasomaji wa qurqn wanapata hali flani ya utulivu wa nafsi pindi wanapoisoma kisahihi kwa kuzingatia. Na hili si kwa wasomaji tuu bali hata kwa wasikilizaji wa quran. Kwa hakika kuna gfaida kubwa sana katika kusikiliza na kusoma qurana. Lakini je ni Zipi faida hizo?. makala hii itakwenda kukuletea faida ama fadhila za kusoma quran sambamba na hilo pia tutakwenda kuziona faida za kusikiliza quran inaposomwa.
Makala hii imeandaliwa na Al-Ustadh Rajabu Athuma na kusambazwa katika tovuti hii. Unaweza kutuunga mkono kwa kazi hii kwa kushea na wengine ama kuhariri makala hizi, ama kukosoa makosa ama kuongezea maarifa katika pale palipo pungua. Hatulipwi kwa kazi hii, tunatarajia malipo kwa Allah.
NI ZIPI FADHILA ZA QURAN?
Kama nilivyotangulia kukwambia kuwa kuna ubora mkubwa katika kuzoma quran. Sasa hebu tuzione fadhila hizo bila ya kupoteza muda.
- Katika hadithi iliyopokewa na Abuu Umamah ni kuwa :Mtume Muhammad (s.a.w) amesema kuwa “somenu quran kwani hakika ya hiyo quran italetwa siku ya qiyama kuja kumuombea mtu aliyekuwa akiisoma” (Muslim)
عن أَبي أُمامَةَ رضي اللَّه عنهُ قال : سمِعتُ رسولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : » اقْرَؤُا القُرْآنَ فإِنَّهُ يَأْتي يَوْم القيامةِ شَفِيعاً لأصْحابِهِ « رواه مسلم
Hadithi hii inatueleza mambo yatakayotokea siku ya qiyama. Kwanza tutambuwe kuwa siku ya qiyama hakuna yeyote yule atakayezungumza ila yule atakayepewa idhini na Allah na atazungumza ukweli tupu (quran-surat An-Nabai). na katika aya zingine Allah anatuambia kuwa siku hiyo hatutaweza kuzungumza kwa midomo kwa midomo itakuwa imefungwa, na hivyo viungo kama miguu na mikono ndio vitazungumza uyataja yale tuliokuwa tukiyafanya (quran-sural Yasin). na katika aya nyingine Allah anatueleza kuwa mpaka ngozi zitatowa ushahidi kwa yale tuliokuwa tukiyafanya.
Hivyo katika hali kama hii kuna wengine watakuwa karibu kuingia motoni, wengine watakuwa tayari wamehukumiwa moto, na wengine katika hali tofautitofauti.basi hapo na quran itapewa ruhusa ya kumtetea mtu ambaye alikuwa akiisoma. Hivyo ndo maana Mtume wa Allah ametutaka sana tusome quran (rejea hadithi hapo juu).
- Kwa hakika hali ya siku ya qiyama ni hali ngumu na nzito sana. Siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli cha Arsh ya Allah. Jua litavutwa karibu sana na vichwa vya watu, majasho yatakaribua kufunika watu, katika hali hiyo watu wakiwa wanahukumiwa kwa wema wao, siku hiyo baba hatamsaidia mama, hakutakuwa na wakili wa kukutetea mbele ya hakimu Allah hakimu wa mahakimu (quran-sural At-tiin). basi Allah ataleta baadhi ya sura za quran zije kukutetea mtu aliyekuwa akiisoma quran huku duniani sra hizo ni surat al-Baqarah ikifuatiwa na surat al-’Imran.
عَن النَّوَّاسِ بنِ سَمعانَ رضيَ اللَّه عنهُ قال : سمِعتُ رسول اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : »يُؤْتى يوْمَ القِيامةِ بالْقُرْآنِ وَأَهْلِهِ الذِين آانُوا يعْمَلُونَ بِهِ في الدُّنيَا تَقدُمهُ سورة البقَرَةِ وَآل عِمرَانَ ، تحَاجَّانِ عَنْ صاحِبِهِمَا « رواه مسلم
Imepokewa hadithi kutoka kwa An-Nawwas bin Sam`an (r.a) kuwa amesema nimemsikia Mtume wa Allah akisema: “Italetwa siku ya qiyama quran na mtu wake aliyekuwa akiisoma na kuifanyia kazi (italetwa) surat al-baqarah na surat Al-’Imran (zitakuwa) zikitoa hoja kumtetea mtu wao. (Muslim).
- Katika mapokezi mengine Mtume (s.a.w) kuwa mtu aliye bora ni yule anayejifunza quran kisha akaifanyia kazi.
عن عثمانَ بن عفانَ رضيَ اللَّه عنهُ قال : قالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : » خَيرآُم مَنْ تَعَلَّمَ القُرْآنَ وَعلَّمهُ رواه البخاري
Imepokewa hadithi kutoka kwa ‘Uthman Ibn ‘Afan kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mbora wenu ni yule mweye kujifunza quran kisha akaifanyia kazi” (Bukhari). Hadithi hii inatupa mafunzo kuwa mbora katika watu si tajiri, ama mtoaji sadaka sana ila mbora ni yule aliyejufunza quran na kuifanyia kazi kwa kuisoma na kufuata maamrisho yake na makatazo yake. Na hii ndio uchamungu wenyewe.
- Katika Hadithi nyingine tunajifunza kuwa Allah hupandisha watu darja kwa hii quran. Imepokewa hadith kutoka kwa ‘Umar Ibn Al-Khataab kuwa Mtume (s.a.w) amesema “hakika Allah hupandihs (darja) watu kwa hii quran na kushusha (darja) watu kwa hii quran” (Muslim)
عن عمرَ بن الخطابِ رضي اللَّه عنهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » إِنَّ اللَّه يرفَعُ بِهذَا الكتاب أَقواماً ويضَعُ بِهِ آخَرين « رواه مسلم
- Kwa hakika inafaa kabisa kumuonea wivu yule ambaye anaisoma quran na kuifanyia kazi. Katika hadithi mtume (s.a.w) anazungumza kuhusu husda na kuwa kuna watu aina mbili inafaha kuwaonea husda kwa ajili ya Allah na si kwa ubaya wowote. Miongoni mwa watu hao ni yule aliyeisoma quran na kuifanyia kazi.
عنِ ابن عمر رضي اللَّه عنهما عن النَّبِيِّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » لا حَسَدَ إلاُّ في اثنَتَيْن : رجُلٌ آتَاهُ اللَّه القُرآنَ ، فهوَ يقومُ بِهِ آناءَ اللَّيلِ وآنَاءَ النَّهَارِ ، وَرجُلٌ آتَاهُ اللَّه مالا ، فهُو يُنْفِقهُ آنَاءَ اللَّيْلِ وَآنَاءَ النهارِ « متفقٌ عليه .
«والآناءُ « : السَّاعات
Imepokewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) ambaye anesema: “Hukuna hasadi ila kwa watu aina mbili. Mtu wa kwanza ni yule a,baye Allah amempa quran naye akawa anasimama kuifanyia kazi (kwa kuisoma na kuifata) wakati wa mchana na usiku, na mtu wa pili ni yule ambaye Allah amempa mali naye akawa anasimama kwa kuitoa (kuifanyia kazi kwa ajili ya Allah) mchana na usiku (Bukhari na Muslim).
Husda hii si kwa ajili ya mabaya bali ni kwa ajili ya Allah, yaani ni hali ya kutamani kile ambacho mwenzio anacho. Haya yote yafanyike kwa lengo la kutaka radhi za Allah na si vinginevyo, bila ya kusababisha madhara kwa yeyote.
- Msomaji wa qurqn anapata sakina yaani utulivu. Huu ni utulivu, yaani mtulizano wa nafsi, fikra (akili) na mwili. Utulivu huu humpata pindi anaposoma quran.
عنِ البُراء بنِ عَازِبٍ رضيَ اللَّه عَنهما قال : آَانَ رَجلٌ يَقْرَأُ سورةَ الكَهْفِ ، وَعِنْدَه فَرسٌ مَربوطٌ بِشَطَنَيْنِ فَتَغَشَّته سَحَابَةٌ فَجَعَلَت تَدنو ، وجعلَ فَرسُه ينْفِر مِنها . فَلَمَّا أَصبح أَتَى النَّبِيَّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم .فَذَآَرَ له ذلكَ فقال : » تِلكَ السَّكِينَةُ تَنَزَّلتْ للقُرآنِ « متفقٌ عليه .
«الشَّطَنُ « بفتحِ الشينِ المعجمةِ والطاء المهملة : الْحَبْلُ
Imepokewa hadith kutoka kwa A-bara Ibn ‘Azib (r.a) kuwa alikuwa mtu mmoja (katika masahaba) akisoma quran surat al-kahaf na pembeni yake kulikuwa na farasi akiwa amefungwa kamba. Basi wakati alipokuwa akisoma quran kulikuwa na kiwingu kikishuka karibu yake, kikawa kinaendelea kushuka, na huku farasi akiwa akihangaika huku na huko. Basi mtu yule alipoamka asubuhi akamueleza mtume kuhusu mambo yaliyotokea. Mtume (s.a.w) akamwambia: “hicho (kiwingu) ilikuwa ni sakina (utulivu) hushuka kwa kusoma quran. (Bukhari na Muslim)
- Kwa hakika kuna ubora na fadhila nyingi sana katika kusoma quran. Kwani kila herufi moja ya quran utakayoisoma utapata mema (thawabu) kumi. Kama tulivyoona hapo juu kuwa quran ina herufi 330,709 hivyo atakayesoma quran yote ataweza kupa thawabu 3,307,090 hiki ni kiwango cha chini, lakini Allah analipa zaidi ya hapo mpka kila jambo jema mmara 700.
عن ابن مسعودٍ رضيَ اللَّه عنهُ قالَ : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : منْ قرأَ حرْفاً مِنْ آتاب اللَّهِ فلَهُ حسنَةٌ ، والحسنَةُ بِعشرِ أَمثَالِهَا لا أَقول : الم حَرفٌ ، وَلكِن : أَلِفٌ حرْف،ٌ ولامٌ حرْفٌ ، ومِيَمٌ حرْفٌ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn Mas’ud kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mwenye kusoma herufi moja (katika quran) Allah atampa jema. Na jema mojqa hulipwa mara 10….”
- Waislamu wanatakiwa waisome quran na kuihifadhi katika vifua vyao. Kwa hakika kuna faida kubwa katika kuhifadhi quran. Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya muislamu anayesoma quran na yule asiyesoma quran. Muislamu asiyesoma quran ni sawa na jumba bovu.
عنِ ابنِ عباسٍ رضيَ اللَّه عنهما قال : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : »إنَّ الَّذي لَيس في جَوْفِهِ شَيْءٌ مِنَ القُرآنِ آالبيتِ الخَرِبِ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn ‘Abas (r.a) kuwa amesema: Amesema Mtume (s.a.w) kuwa: “hakika yule ambaye hakuna katika kifua chake (yaani hakuhifadhi) chochote katika quran ni sawa na jumba bovu”. (Tirmidh)
- Kutakuwa na kuachana kukubwa sana kwa darja peponi kati ya waliohifadhi quran na wale ambao hawakuihifadhi. Watakaoingia peponi wataambiwa soma quran, hapo kila atakayesoma aya atakuwa akipanda daraja, atapanda kadiri ya aya atakazozisoma.
عن عبدِ اللَّهِ بنِ عَمْرو بن العاصِ رضي اللَّه عَنهما عنِ النبيِّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » يُقَالُ لِصاحبِ الْقُرَآنِ : اقْرأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ آَما آُنْتَ تُرَتِّلُ في الدُّنْيَا ، فَإنَّ منْزِلَتَكَ عِنْد آخِرِ آيةٍ تَقْرَؤُهَا « رواه أبو داود ، والترْمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa ‘Abdallah Ibn ‘Umar Ibn Al-’Aas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa amesema: “Itaambiwa kwa mtu (msomaji wa quran siku ya qiyama) “soma na na upande (daraja) na uisome (tartila) kama ulivyokuwa ukiisoma duniani. Kwani kwa hakika mafikio (daraja) yako yatakuwa ni mwisho wa aya yako (utakayoisoma mwisho)” (Abuu Daud)
MWISHO
Kwa hakika tunatakiwa kusoma sana qurani na kuihifadhi, na katu kusiiwache ikatitoka. Mtume (s.a.w) amekataza sana vikali kuisahau quran. Darsa lijalo tutakwenda kuangalia makatazo juu ya kuisahau quran baada ya kuihifadhi. Msomaji wa quran anakuwa tofauti na asiyeisoma kwani msomaji anapata faida nyingi kama tulivyoziona.
Ndugu yangu Muislamu, tunakuomba utuunge mkono kwa kazi hii. Kwani ni sadaka yenye kuendelea. Hatufanyi hii kazi kwa kulipwa ni radhi za Allah ndio tunatarajia. Unaweza kutuunga mkono kwa kuongeza maaraifa katika darsa zeu, kurekebisha makosa ya kiuandishi, kushea darsa hizi kwa wengine.
MAKALA NYINGINE ZAIDI
- DARSA ZA FUNGA
- DARSA ZA DUA
- DARASA LA AFYA
- AFYA YA UZAZ
- DARSA ZA SIRA
UFUPISHO WA SOMO
Quran ni kitabu cha Allah kinachotoa mafunzo katika sheria, makatazo na maamrisho na mengineyo mengi. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya kiarabu, hivyo huwafanya watu wajifunze kusoma kiarabu ndipo waweze kusoma quran kiusahihi zaidi. Kitabu hiki pia kinaweza kuhifadhiwa hata kabla ya mtu kuweza kujua kusoma maandishi ya kiarabu.
Changamoto ya wasomaji wengi leo hawajui faida za kusoma quran. Tutakwenda kuona fadhila kuu 9 zinzopatikana katika kusoma quran. Chini hapo nitataja baadh tu ya faida za usomaji wa quran, katika makala hii nitakwenda kukueleza miongoni mwa faida hizo:-
- Quran ni kiombezi siku ya kiyama kuja kumuombea mtu wake aliyeisoma quran duniani;
Mtume Muhammad (s.a.w) amesema kuwa “somenu quran kwani hakika ya hiyo quran italetwa siku ya qiyama kuja kumuombea mtu aliyekuwa akiisoma” (Muslim)
عن أَبي أُمامَةَ رضي اللَّه عنهُ قال : سمِعتُ رسولَ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : » اقْرَؤُا القُرْآنَ فإِنَّهُ يَأْتي يَوْم القيامةِ شَفِيعاً لأصْحابِهِ « رواه مسلم
- Mtu mwenye kusoma quran na kuifanyia kazi ndiye mtu bora
عن عثمانَ بن عفانَ رضيَ اللَّه عنهُ قال : قالَ رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : » خَيرآُم مَنْ تَعَلَّمَ القُرْآنَ وَعلَّمهُ رواه البخاري
Imepokewa hadithi kutoka kwa ‘Uthman Ibn ‘Afan kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mbora wenu ni yule mweye kujifunza quran kisha akaifanyia kazi” (Bukhari).
- Mwenye kusoma quran hupandishwa daraja na Allah huwashusha daraja wasiosoma quran
Mtume (s.a.w) amesema “hakika Allah hupandihs (darja) watu kwa hii quran na kushusha (darja) watu kwa hii quran” (Muslim)
عن عمرَ بن الخطابِ رضي اللَّه عنهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : » إِنَّ اللَّه يرفَعُ بِهذَا الكتاب أَقواماً ويضَعُ بِهِ آخَرين « رواه مسلم
- Allah humlipa msomaji wa quran kwa kila herufi moja atakayoisoma
عن ابن مسعودٍ رضيَ اللَّه عنهُ قالَ : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : منْ قرأَ حرْفاً مِنْ آتاب اللَّهِ فلَهُ حسنَةٌ ، والحسنَةُ بِعشرِ أَمثَالِهَا لا أَقول : الم حَرفٌ ، وَلكِن : أَلِفٌ حرْف،ٌ ولامٌ حرْفٌ ، ومِيَمٌ حرْفٌ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn Mas’ud kuwa Mtume (s.a.w) amesema “mwenye kusoma herufi moja (katika quran) Allah atampa jema. Na jema mojqa hulipwa mara 10….”
- Mtu ambaye hakuhifadhi chochote katika quran kwenye moyo wake ni sawa na jumba bovu
عنِ ابنِ عباسٍ رضيَ اللَّه عنهما قال : قال رسولُ اللَّهِ صَلّى االلهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : »إنَّ الَّذي لَيس في جَوْفِهِ شَيْءٌ مِنَ القُرآنِ آالبيتِ الخَرِبِ « رواه الترمذي وقال : حديث حسن صحيح
Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn ‘Abas (r.a) kuwa amesema: Amesema Mtume (s.a.w) kuwa: “hakika yule ambaye hakuna katika kifua chake (yaani hakuhifadhi) chochote katika quran ni sawa na jumba bovu”. (Tirmidh)
MWISHO
Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwakumbusha nduguzangu waislamu juu ya kuisahau quran baada ya kuihifadhi. Ndugu yangu Muislamu kati usiiwache quran uliyokwisha ihifadhi ikapotea kifuani kwako. Mtume (s.a.w) amekataza vikali sana kuhusu kuisahau quran. Darsa lijalo tutaangalia makatazo hayo.
Tafadhali tuunge mkono kwa kushea makala hii kwa wengine kwa ajili ya Allah.
- MAKATAZO JUU YA KUISAHAU QURAN BAADA YA KUIHIFADHI
Kuifadhi quran ni jambo linalotakiwa sana kwa Muislamu kulifanya. Kwani tusipofanya hivyo tunaweza kukosa faida nyingi. Maulamaa wameweka njia mbalimbali katika kusaidia kuihifadhi quran. Na Mtume pia ametueleza baadhi ya njia hizo ikiwemo kuisoma quran mara kwa mara. Laini leo watu wengi waliohifadhi quran wamesha sahau. Wapo waliohifadhi msahafu mzima na kusahau, na wapo waliohifadhi baadhi tu ya sehemu na kuzisahau.
Mtume (s.a.w) amekataza vikali kuiwachia quran kuisahau baada ya kuihifadhi. Katika makala hii tutakwe
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 596
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Madrasa kiganjani
Post zifazofanana:-
MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...
NAFASI YA SUNNAH KATIKA UISLAMU
Nafasi ya Sunnah katika UislamuMtume Muhammad (s. Soma Zaidi...
Taratibu za kumuona mchumba
Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...
Swala ya kupatwa kwa jua na mwezi na namna ya kuiswali
11. Soma Zaidi...
Swala za tahajud na namna ya kuziswali
4. Soma Zaidi...
ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...
1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
1. Soma Zaidi...
Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)
Soma Zaidi...
Taratibu za kufunga ndoa na kumuinglia mke
Soma Zaidi...
Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo
Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo. Soma Zaidi...
Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa
Soma Zaidi...