Navigation Menu



image

IJUWE MINYOO, SABABU ZAKE, ATHARI ZA MINYOO, MATIBABU YAKE NA KUPAMBANA KWAKE

IJUWE MINYOO, SABABU ZAKE, ATHARI ZA MINYOO, MATIBABU YAKE NA KUPAMBANA KWAKE

MINYOO NA ATHARI ZAO KIAFYA

MINYOO NA HATARI YEKE KWA AFYA

Utangulizi

Karibu tena kwenye makala zetu za afya. Makala hii ni katika mwendelezo wa makala zetu za afya na maradhi. Katika makala hii utakwenda kushuhudia mambo mengi sana kuhusu minyoo. Tumechagua mada hii kwa sababu tatizo la minyoo limekuwa ni tatizo pana sana na linaathiri watu wengi hususan waishio vijijini.


 


Watu wengi hawatambui athari za minyoo kwa mwanadamu ijapokuwa wanaishi na minyoo hata bila ya kugundua. Hatimaye wanashindwa kula kwa kukosa hamu ya kula, wanashindwa kufanya kazi vyema kwa miwasho na ushovu. Wanaingia gharama nyingi kwa kupungukiwa na damu na kutibu maradhi mengine yaliyosababishwa na minyoo.


 


Hivyo usikose kwenye makala hii yenye faida kwa ajili ya afya yako, na afya ya watu wa karibu yako. Ukigundua kuna kosa lolote katika makala hii, wasilianan nasi kwa haraka zaidi ile kupunguza madhara zaidi yatakayosababisha na kukosea kwetu.


 


Mwandishi: Mr.Rajabu Athuman


Mchapishaji: bongoclass


Chanzo:    www.bongoclass.com


Email:     admin@bongoclass.com


 


 


MINYOO NI NINI?

Minyoo ni katika vimelea ama wadudu wanaoishi ndani ya kiumbe aliye hai. Wanaweza kuishi kwenye wanyama kama ngo’ombe, ngurue na mbuzi, pia wanaweza kuishi ndani ya binadamu. Wanajipatia mahitaji humo kama chakula, hewa na kila wanachohitaji. Wakiwa wanaishi ndani ya mwili wa kiumbe hai wanaweza kusababisha madhara makubwa sana katika afya ya mtu. Wadudu hawa kitaalamu wanatambulika kama parasitic worm.


 


Katika makala hii tutakwenda kujifunza, dalili, sababu, matibabu na njia za kupambana na minyoo katika mazingira yetu. Pia tutaona madhara ya kiafya yanayoletwa na kuishi na minyoo mwilini. Endelea kuwa nasi upate faida hii


 


Hatari ya kupata minyoo ni kubwa sana maeneo ya vijijini ama katika maeneo ambayo hali ya usafi sionzuri. Nchi zinazoendelea kama nchi za afrika ni katika maeneo ambayo yanakabil;iwa sana na minyoo kuliko nchi zilizo endelea.


 


Wataalamu wanatueleza kuwa kuna aina zaidi ya 300,000 (laki tatu) za minyoo. Na katika aina hizi kuna aina 300 (mia tatu) za minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu na kumuathiri kwa namna moja ama nyingine.


 


Minyoo wanazaliana kwa kutaga mayai, na mayai yao yanatofautiana ukubwa, kuna ambayo yanaonekana kwa macho na mengine ni madogo zaidi kwa kuonekana kwa macho. Kuna aina za minyoo hutaga mayai bila ya kuhitaji kuwepo kwa dume, kwani kuna minyoo ambayo ina jinsia zote kwa pamoja (hermaphroditc).


 


Minyoo huweza kutaga mayai zaidi ya mara sita kwa siku. Na idadi ya mayai yao ni kati ya mayai 3000, mpaka 700000. na mayai yao yanaweza kudumu kwa miezi mingi biala ya kufa, na yanaweza kuvumialia hali mbalimbali za joto.


AINA ZA MINYOO

Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa. Aina hizi ni Minyoo wanaotambulika kama flatworm, roundworm na thory-headed worm. Majina ya minyoo hawa yanafanana na maumbile yako kama tutakavyoona hapo chini. Wengi katika hawa minyoo wanaweza kuonekana kwa macho


 


  1. Minyoo inayotambulika kama Tapeworm

Hawa ni katika aina za flatworm, minyoo hawa wanaumbo lililo bataa yaani flati. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kunywa maji ambayo yana mayai ya minyoo hawa au lava. Pia unaweza kuwapata. Minyoo hawa kwenye chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuiva vizuri.kama nyama hasa ya ngurue. Karibia nyama za wanyama wote zina wadudu hawa.


 


Minyoo hawa wanaonekana kama pingili zilizoungana na kutengeneza cheni ndefu. Minyoo hawa wanaweza kuwa warefu mpaka kufikia futi 80 na wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu mpaka miaka 30.


 


  1. minyoo inayotambulika kama flukes

Hawa pia ni katika aina za minyoo waitwao flatworm. Mwanadamu anaweza kuwapata minyoo hawa kupitia maji yasiyo salama,kupitia mboga ambazo hukuwa ndani ya maji.pia kwa kula samaki ambaye ana minyoo hawa. Pia inatokea ukaosha mboga, tunda kwa kutumia maji ambayo yana minyoo hawa.


 


Minyoo hawa wanapoingia mwilini wanaelekea kwanye utumbo mdogo na huko ndipo huishi, pia maeneo mengine wanapoishi ni kwenye damu, na tishu za mwili kama ini. Kuna aina nyingi za aina hii ya minyoo, lakini ukubwa wao hawazidi nchi kadhaa.


 


  1. minyoo wanaotambulika kama Hookworm

Hawa ni minyoo aina ya roundworm. Minyoo hawa wanaweza kusambazwa kwa kupitia kinyesina udongo. Hasa kwa wale wanaokula udongo ni rahisi sana kupata aina hii ya minyoo. Njia nyingine nyepesi kwa kupata minyoo hawa ni kwa kutembea miguu peku kwenye udongo ambao una mayai au lava wa aina hii ya minyoo. Malava haya yanaweza kuingia kwenye ngozi yako.


 


Minyoo hawa wanaishi kwenye utumbo mwembamba, na kwa kuwa kichwani kwao kuna kama miimba ilofanana na ndiwano, wanaitumia kujitundika kwenye utumbo mdogo. Ukubwa wao hauzidi nusu nchi.


  1. minyoo wanaotambulika kama pinworms (threadworms)

Hawa ni katika minyoo wadogo sana na maranyingi hawana madhara. Minyoo hawa ni maarufu sana kwa watoto, walezi wa watoto wadogo na maeneo yeye watoto wadogo wengi unweza kuwapata sana hawa. Wana rangi nyeupe na ukubwa wao hauzindi nusu nchi.


 


Minyoo hawa unawapata kwa kuyala mayai yao kutoka kwa mtu mwenye minyoo hii. Mayai ya minyoo hawa hayawezi kuonekana kwa macho. Pindi unapokula mayai haya yanakwenda kukaa kwenye utumbo mdogo mpaka kutotolewa. Wakati wa usiku minyoo wanawake wanakwenye chini kwenye puru na kutaga mayai kwenye mikunjo ya puru. Kama mtu atajikuna sehemu ya puru mayai yale yanabakia mkononi zaidi ya masaa kadhaa.


 


Ikitokea mtu huyu ameshika kitu bila ya kunawa mayai yele yanabaki pale. Kama mtu mwingine akapashika pale na akala kitu bila ya kunawa anaweza akayala mayai yale na kupata minyoo. Pia minyoo hii unaweza kuipata kwa kuvuta hewa yenye mayai ya minyoo hii.


 


Minyoo hii haina athari zaidi kwa afya lakini mwenye minyoo hii atahisi kuwashwa kwenye puru, ama kuzungukia sehemu ya haja kuwa, wakati mwingine maumivu yatumbo. Wakati mwingine ngozi inawasha sana. Minyoo hawa pia kwa wanawake wanaweza kuhama kutoka kwenye puru na kuelekea kwenye uke wa mwanamke na kuingia ndani. Huenda hali hii ikapelekea kupata UTI na matatizo mengine ya kiaya.


 


Kupambana na minyoo hawa hakikisha unaosha mikono unapoamka, unapotaka kula chochote, kuingia kwenye choo safi na usipende kushikshika vitu hasa maeneo ya vyoo vya watu wengi. Minyoo hawa ni rahisi kutibika tofauti na minyoo wengine.


 


  1. minyoo wanaotambulika kama trichinosis worm

Minyoo hawa ni katika minyoo ambao wanapatikana kutoka kwa wanyama. Mtu anaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula nyama ambayo haukuiva vyema, ama kwa kula nyama mbichi. Malava ya minyoo hawa yanakwenda kwenye utumbo mdogo, na huko huweza kuingia kwenye mirija ya damu na kuenda maeneo mengine ya mwili, kwenye misuli na tishu za mwili.


 


NI NINI CHAKULA CHA MINYOO?

Kama tulivyokwisha kuona aina za minyoo, bila shaka umetambua kidogo kuhusu nini wanakifanya wakiwa mwilini. Hivyo basi katika sehemu hii nitakwenda kukueleza chakula cha minyoo ndani ya mwili:-


 


  1. Wanakula chakula tunachokula, katika aina hizi za minyoo wapo minyoo wanaishi kwenye utumbo mdogo. Hii ndiyo sehemu ambayo chakula kinameng’enywa na kuupa mwili nishati na afya yaani kuupatia mwili virutubisho. Lakini minyoo hawa wakati mwingine wanakula chakula alichokula mtu hata kabla ya kumeng’enywa. Hali hii inaweza kusababishia mtu kukosa virutubisho na hatimaye kukonda ama kupoteza usito.
  2. Wanakunywa damu, wapo minyoo wengine wanaishi kwenye mfumo wa damu ama ameneo mengine na kuanza kunyonya damu. Minyoo hawa ni hatari sana kwani wanaweza kusababisha ugonjwa wa anaemia. Ugonjwa huu husababishwa na upungufu wa damu.
  3. Wanakula viungo vya mwili, katika minyoo hawa kwa mfano liverfluke hawa wanaishi kwenye ini ama maeneo ya nyongo. Minyoo hawa wanakula ini, na kulisababishia vidonda. Pia ini linaweza kuvimba hatimaye kuleta madhara makubwa.
  4. Wanakula tishu nyingine, tofauti na hayo tuliyotaja minyoo hawa wanaweza kula tishu nyingine ndani ya mwili. Kama tulivyoona kuna baadhi ya minyoo wanakaa kwenye ngozi, viungio, ini na sehemu nyingine.

VYNZO VYA MINYOO

Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Hapa ninakwenda kukuorodheshea kwa ufupi vyanzo hivi vya minyoo kwa ujumla wao na makundi yao:


  1. kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama. Wakati mwingine kuosha tu haitoshelezi, maana unaweza kuosha kwa maji ambayo yana vimelea vya minyoo, hivyo unajikuta hukufanya kitu. Kwani minyoo wanaishi ardhini, kwenye majani na kwenye maji.
  2. Kunywa maji ambayo si masafi na si salama. Maji machafu yanaweza kuwa na mayai ama lava wa minyoo hii. Maji ambayo yamechanganyika na choo kikubwa yanakuwa na mazalia ya minyoo hii. Ni vyema kuchemsha maji hata yachemke, yapozwe na yahifadhiwe vyema kwa matumizi ya nyumbani na hata biashara.
  3. Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi. Upikaji wa nyama yeyote unatakiwa uwe wa makini sana. Kuhakikisha kuwa nyama imewiva vyema. Kuna baadhi ya nyama zinashauriwa kuwa makini sana katika kuzipika kama nyama ya ngurue na ya punda. Pia kuna aiana za samaki nao wanahitajika kuwapika vyema kama samaki aina ya kaa.
  4. Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo. Minyoo huweza kuishi kwenye udongo, na ikitokea my akatembea bila ya viatu katika eneo hili, minyoo hawa wanaweza kupenya kwenye ngozi yake na kuingia mwilini.
  5. Kula udongo, tunaona sana mara nyingi watu wanakula udongo, ukweli ni kuwa sio kila udongo unakuwa na minyoo. Kama utakuwa umeandaliwa vyema unaweza kuwa hauna minyoo. Lakini kula udongo kunaweza kusababisha minyoo. Pia kuna madhara makubwa sana ya kiafya katika kula udongo.
  6. Kinyesi cha wanyama na binadamu. Hivi ni vyanzo vizuri sana vya minyoo. Kwani minyoo wanaweza kuishi kwenye kinyesi vyema na kwa muda mrefu zaidi kuliko maeneo mengine.

DALILI ZA MINYOO

Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo  wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-


  1. Kichefuchefu
  2. Kukosa hamu ya kula
  3. Maumivu ya tumbo
  4. Kupungua uzito
  5. Uchovu wa viungo
  6. Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
  7. Kuona minyoo kwenye kinyesi.
  8. Kuona damu kwenye kinyesi
  9. Tumbo kujaa

 


Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-


 


  1. minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
  2. Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
  3. Kuwa na alegi
  4. Kuwa na homa
  5. Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa

 


  1. minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
  2. Kuwashwa
  3. Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
  4. Kuwa na uchovu wa hali ya juu.

 


  1. minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
  2. Kupata homa
  3. Kuvimba kwa uso
  4. Maumivu ya misuli na kuchoka
  5. Maumivu ya kichwa
  6. Kutokupenda kupigwa na mwanga
  7. Matatizo katika macho (conjuctivist)

 


ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO

Kukaa na minyoo na kutoitibu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara mengi hususani kwenye ini na maeneo mengine ya mfumo wa kumeng’enya chakula. Kama ulivyoona kwenye dalili za minyoo, hivyo minyoo ikiachwa bila ya kutibia miongoni mwa athari zake ni kuendelea kwa dalili zile na kuwa ni ugunjwa. Miongoni mwa athari hizo ni:-


  1. kupata magonjwa yanayohusiana na ini pamoja na nyongo kama necrosis, gallstone (kuwa na vijiwe kwenye mrija wa nyongo), kuziba kwa mrija wa nyongo, biliar colic, cholecystitis, urticaria
  2. Kutapika na kutapika damu
  3. Maumivu ya tumbo
  4. Kupoteza damu
  5. Mwili kukosa virutubisho kutoka kwenye chakula
  6. Kichefuchefu
  7. Kupunguwa uzito na kukonda
  8. Ukuaji hafifu kwa watoto
  9. Matatizo ya akili
  10. Kuharisha n.k

VIPIMO VYA MINYOO

Haitoshelezi kuwa na dalili pekee ukathibitisha kuwa una minyoo. Itahitajika uende hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi. Kuna aina tano za vipimo vya kupima minyoo kama vile:-


  1. kupima kinyesi kama kina minyoo au mazalia ya minyoo (fecal test)
  2. Kumulika utumbo mkubwa (colonoscopy) hiki ni kifaa chenye kamera ambacho kinaingizwa kwenye njia ya haja kubwa, ili kumulika utumbo mkubwa kama kuna minyoo
  3. Kupima damu (blood test)
  4. Kuchukuwa picha za mwili kwa kutumia vifaa kama X-ray, MRI na CT scan.
  5. Kupima kwa kutumia tep (tape test). unapewa kaji tep (kama kamkanda kadogo) kisha unakaweka kwenye tundu ya haja kubwa na mara nyingi wakati wa asubuhi unapoamka. Kisha katep haka kanawekwa kwenye hadubuni (microscpe) na kuchunguza uwepo wa minyoo aina ya pinworm au mayai yao.

 


 


 


TIBA YA MINYOO

Moja katika sifa za minyoo ni kuwa wanatibika kwa urahisi pindi mgonjwa akipewa dawa husika. Minyoo hawa wanauliwa kwa dawa, kisha wanatolewa nje ya mwili. Ni mara chache sana minyoo hawa wanavamia sehemu nyingine za mwili na hivyo tiba sahihi ni kufanyiwa upasuaji.


 


Tiba ya minyoo hawa pia inategemea ni aina gani ya minyoo ambao mgonjwa anao. Kwani kila aina ya minyoo hawa ina sifa zake na hivyo dawa zao zinaweza kutofautiana. Mgonjwa asikurupuke kwenda duka la madawa kununua dawa za minyoo bila ya kujua aina za minyoo alio nao.


 


Kwa mfano:-


  1. minyoo aina ya tapeworm wanaweza kutibika kwa vidonge kama praziquantel (biltricide)
  2. Minyoo aina ya roundworm wanaweza kutibika kwa mebendazole (vermox, emverm) na albendazole (albenza).

 


Ni vyema mgonjwa kwenda kituo cha afya akaonane na daktari ili aweze kumthibitishia tiba inayofanana na tatizo lake.


 


NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO

Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo. Njia hizo ni kama :-


  1. usile chakula, nyama ana samaki ambaye hajapikwa vyema, ama kula nyama mbichi ama isiyoiva
  2. Epuka kugusagusa nyama unapoandaa chakula chako, tenganisha nyama kivyake na vyakula vingine wakati unapoandaa kupika.
  3. Safisha vyema vyembo ambavyo vimegusa nyama ambayo haikupikwa
  4. Usile mimea ambayo inaishi ndani ya maji yabaridi
  5. Usitembee miguu wazi kwenye maeneo machafu ambayo yana kinyesi
  6. Safisha vyema kinyesi cha wanyama.
  7. Hakikisha unapika vizuri nyama mpaka uhakikishe imewiva vyema,
  8. Wanya kung’ata kucha ama kunyonya vidole
  9. Hakikisha unaosha kila unachokila kwa maji yaliyo safi na salama.
  10. Usafi wa mwili, mavazi na mazingira ni muhimu kwa ajili ya kupambana na minyoo.
  11. Kuwacha kabisa kula udongo

 


MADHARA YA KIAFYA YANAYOHUSIANA NA MINYOO

Tofauti na madhara ambayo tumeyaona huko juu kwenye dalili kama maumivu ya kicha, tumbo na miwasho, kichefuchefu na kutapika. Lakini minyoo ikizidi madhara haya huwenda yakawa makubwa zaidi.


 


  1. mgonjwa anaweza kutapika damu
  2. Miwasho mikali kwenye puru na sehemu za siri kwa wanawake
  3. Inaweza kuathiri ini na tishu nyingine
  4. Inaweza kupelekea kupata ugonjwa wa anaemia
  5. Uchpvu, kupungua uzito na homa

 


FAIDA ZA KIAFYA ZA MINYOO

Wakati mwingine kuwa na aina flani ya minyoo kunaweza kuwa na faida katika afya. Lakini si kila minyoo wana faida hizi. Kribia minyoo wote wanamadhara kiafya kama tulivyoona hapo juu. Sasa hebu kwa ufupi zitambue baadhi tu ya faida za minyoo;-


 


  1. minyoo wanaweza kusaidia kwa wanawake kuchochea kupata ujauzito

Kulingana na tafiti iliyofanya na mwana biolojia anayetambulika kama Aaron Blackwell kutoka chuo kikuu cha (University of California), Santa Barbara. Amefanyia tafiti wanawake 1000 katika kijiji cha Bolvia kwa muda wa miaka tisa.


 


Katika tafiti yake aligundua kuwa wanawake ambao hawakutumia uzazi wa mpango wana wastani wa watoto tisa kwa kila mmoja. Aligundua kuwa wanawake wenye aina ya minyoo inayotambulika kama helmith wanapata ujauzito mapema kuliko wengine.


 


  1. huweza kupunguza alegi (allegy)

Kuna watu wanaaleji na vitu mbalimbali ikiwemo madawa, vinywaji ama vyakula. Mtafiti aliyetambulika kwa jina la John Turton alikuwa ni raia wa Uingereza na alihusika katika baraza la kufanya tafiti za kiafya.


 


Mnamo mwaka 1970 alikuwa na aleji kali sana. Hivyo akajiathiri kwa kujiwekea minyoo aina ya hookworm. Baadaye akajakutoa taarifa kuwa aleji zake zimepungua kwa miaka miwili yote ambayo minyoo ile ilikuwa tumboni mwake.


 


  1. minyoo wanaweza kusaidia katika kupona kwa vidonda.

Minyoo aina ya liver fluke ambao wanaishi kwenye ini wanazalisha homoni inayoitwa granulin. Watu ambao wana minyoo hii wapo hatarini sana katika kupata saratani ya kifuko cha nyongo (bile duct cancer). wakati ambao minyoo hawa wanakula ini kuna vidonda hutokea, hivyo wanavitibu wenyewe vidonda hivi.


 


 


MWISHO

Mwisho tunapenda kusema kuwa unapohisi una minyoo kutokana na dalili ambazo tumezitaja humu, nenda kituo cha afya ukapate ushauri zaidi. Kwani unaweza kutumia dawa lakini za minyoo bila ya kujuwa ni aina gani ya minyoo unapambana nayo.



Download kitabu hiki hapa






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 5748


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Visababishi vya ugonjwa wa Varicose vein
Posti hii inahusu zaidi visababishi mbalimbali vya ugonjwa wa vericose veini, ni visababishi mbalimbali ambavyo utokea kwenye mtindo wa maisha kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Zijue sababu za kushindwa kushuka kwa makende (testicle))
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kushindwa kushuka kwa makende kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye skolatumu(scrotum). Soma Zaidi...

Fahamu Ugonjwa wa misuli kuwa dhaifu.
hali ambayo misuli unayotumia kwa hotuba ni dhaifu au unapata shida kuidhibiti mara nyingi inaonyeshwa na usemi wa kufifia au polepole ambao unaweza kuwa mgumu kuelewa. Sababu za kawaida za Ugonjwa huu ni pamoja na matatizo ya mfumo wa neva (neurolojia Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye mrija wa mkojo(urethritis )
Posti hii inahusu zaidi maambukizi kwenye mrija wa mkojo, maambukizi haya usababishwa na virusi na bakteria. Soma Zaidi...

Dalili za uvumilivu wa pombe
Uvumilivu wa pombe unaweza kusababisha athari za haraka, zisizofurahi baada ya kunywa pombe. Ishara na dalili za kawaida za kutovumilia kwa pombe ni pua iliyojaa na Kuvuta ngozi. Uvumilivu wa pombe husababishwa na hali ya maumbile ambayo mwili hauwezi k Soma Zaidi...

Masharti ya vidonda vya tumbo
Haya ni masharti ya mwenye vidonda vya tumbo. Mgojwa wa vidonda vya hatumbo hatakiwi kufanya yafuatayo Soma Zaidi...

Athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa watoto wadogo.
Posti hii inahusu zaidi athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa watoto wadogo, tunajua kubwa mama kama ana ugonjwa huu anaweza kumwambikiza mtoto na mtoto akazaliwa na Ugonjwa huu. Soma Zaidi...

Dalili za homa ya ini
Kaika post hii utakwenda kujifunz akuhusu dalili za homa ya ini. Dalili hizi sio lazima zitokee zote. Zinaweza zikatokea baadhi tu na ikatosha kuonjesha kuw auna homa ya ini. Soma Zaidi...

VIDONDA VYA TUMBO NA ATHARI ZAKE
Soma Zaidi...

Typhoid husabisha mwili kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na joint za miguu kuchoka
Dalili za typhid zinapasa kuangaliwa kwa umakini. Bila vipimo mtu asitumie dawa za tyohod, kwanu dalili za tyohid hufanana na daliki za maradhi mengi. Soma Zaidi...

Fangasi wa sehemu za Siri
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu fangasi wa sehemu za Siri Soma Zaidi...

Dalili za kifua kikuu (tuberculosis)
Kifua kikuu ni ugonjwa sugu wa kuambukiza na anuwai ya magonjwa ya kiafya yanayosababishwa na Mycobacterium tuberculosis complex. Kwa binadamu sababu ya kawaida ni Mycobacterium tuberculosis. Soma Zaidi...