image

Mafundisho ya Mitume

Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.

Mafundisho ya Mitume

Mafundisho ya Mitume


Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.w).Dalili zinazodhihirisha kuwepo Allah (s.w) katika eneo hili ni pamoja na:(a)Umoja wa ujumbe wa mitume(b)Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao(c)Upeo wa elimu waliyokuwa nayo mitume.

Kitu kinachodhihirisha kuwa Mitume ambao baadhi yao ulimwengu mzima una shuhudia historia yao, kama vile historia ya Nabii Ibrahim (a.s), Musa (a.s), Isa (a.s) na Muhammad (s.a.w) kuwa ni wajumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) wenye ujuzi na hekima, ni kule kufanana kwa ujumbe wao.


Kama dhana ya kutokuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) ingelikuwa kweli, ingelikuwa muhali kwa Mitume waliotokea sehemu tofauti nyakati tofauti, kutoa ujumbe unaofanana. Turejee katika Qur-an mifano michache ya mafundisho ya msingi waliyotoa Mitume kwa watu wa o:Tulipompeleka Nuhu kwa watu wake, naye akasema: “Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu.


Nyinyi hamna Mungu ila Yeye.Hakika mimi ninakuhofieni adhabu ya siku (hiyo) iliyo kuu ”. (7:59).Na kwa Adi (tulimpeleka) ndugu yao Hudi, akasema: “Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Basi hamuogopi? (7:65).


Na kwa thamud (tulimpeleka) ndugu yao, Saleh. Akasema “Enyi watu w angu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mola ila Yeye. Hakika umekwisha kukufikieni muujiza ulio dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye na ishara kwenu (ya Utume wangu).


Basi muacheni ale katika ardhi ya Mungu, wala msimtie katika dhara yoyote, isije ikakushikeni adhabu iumizayo. (7:73).


(iv) Shu’ayb (a.s)
Na kwa watu wa Madyan (tulimpeleka) ndugu yao, Shu’ayb, akasema:


‘Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu, hamna Mungu mwingine isipokuwa Yeye. Zimekwisha kufikieni hoja dhahiri kutoka kwa Mola wenu. Basi kamilisheni sawa sawa vipimo (vya vibaba) na mizani (pia) wala msiwapunguzie watu vitu vyao wala msifanye uharibifu katika ardhi badala ya kutengenea kwake. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi mumeamini. (7:85).


Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Mola wenu. Basi muabuduni. Hii ni njia iliyonyooka. (19:36)
(vi) Muhammad (s.a.w)Sema (ewe Muhammad): “Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote; (Mungu) ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi, hakuna aabudiwaye (kwa haki) ila yeye, yeye ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, aliye Nabii Ummiyyi (asiyejua kusoma wala kuandika) ambaye humuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka”. (7:158)


“Na bila shaka tulimpeleka mtume katika kila umma ya kwamba, “Muabuduni Mwenyezi Mungu na mwepukeni twaghuti. Basi wako miongoni mwao ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa na wako miongoni mwao ambao upotofu umethubutu juu yao. Basi tembeeni katika ardhi na mwangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha ”. (16:36)
Ukirejea katika Qur-an utaona kuwa Mitume wote kwa ujumla wamefundisha yafuatayo:-(i)Tawh iid
Wamewafundisha watu juu ya kuwepo Allah (s.w) na upweke wake kwa kuwaonyesha dalili zilizo waziwazi.(ii)Lengo
Waliwafundisha watu kuwa lengo la kuumbwa kwao ni kumuabudu Allah (s.w) na kusimamisha ukhalifa wake hapaulimwenguni na kisha waliwafundisha namna ya kumuabudu Mola wao katika kila kipengele cha maisha.(iii)Kubashiria
Waliwabashiria watu malipo mema ya kudumu ya huko Peponi kwa wale watakaoamini vilivyo na kutenda mema katika maisha yao ya hapa duniani.(iv)Kuhofisha
Waliwahofisha watu juu adhabu kali watakayopata huko Akhera wale watakao mkufuru Allah (s.w) na kumwabudu twaghu ti.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 330


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Nafsi ya mwanaadamu
Soma Zaidi...

(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini
Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini. Soma Zaidi...

MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu). Soma Zaidi...

Maadili na malezi ya jamii
Soma Zaidi...

njia ya maandishi
Soma Zaidi...

Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

Hijabu na kujikinga na zinaa
Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah
Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU
Soma Zaidi...