image

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU


KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU


Nafasi ya akili katika kumtambua Allah (s.w)Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) itathibitika moyoni baada ya kumjua vyema Allah (s.w) na sifa zake zote tukufu. Allah (s.w) hatumuoni kwa macho bali tunamfahamu kwa akili zetu katika kuchunguza dalili mbali mbali zilizotuzunguka.


Tunavyojifunza katika Qur-an, matumizi ya kwanza ya akili tulizotunukiwa ni kuyakinisha kuwepo kwa Allah (s.w) na sifa zake. Msisitizo wa matumizi ya akili na fikra zetu katika kazi hii ya kumjua Allah (s.w) na sifa zake tukufu unabainishwa katika aya zifuatazo:“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ziko hoja (za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu - Allah) kwa wenye akili”. (3:190).


“Na katika ishara zake, (za kuthibitisha kuwepo kwake na uweza wake) ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kutoka kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofa hamu” (30:21)“Na katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi”. (30:22).


“Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.” (30:23)


“Na katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamu” (30:24)
Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo:“Je! Huoni kwamba Mw enyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kw ayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.(35:27)


Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu.” (35:28)
Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za “dini” bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists). Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:1 79)


“Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)” (8:22).


Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu.


Je! Huoni ya kw amba Mw enyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nu ru (31:20)


Na katika w atu w ako w anaojadiliana juu ya Mw enyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8).
Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni:
Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake
Nafsi ya mwanaadamu
Historia ya mwanaadamu
Maisha ya Mitume
Mafundisho ya Mitume


“Na katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi”. (30:22). “Na katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.” (30:23) “Na katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamu” (30:24) Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo: “Je! Huoni kwamba Mw enyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kw ayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.(35:27) Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu.” (35:28) Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za “dini” bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists). Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an: “Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:1 79) “Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)” (8:22). Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu. Je! Huoni ya kw amba Mw enyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nu ru (31:20) Na katika w atu w ako w anaojadiliana juu ya Mw enyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8). Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni: Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake Nafsi ya mwanaadamu Historia ya mwanaadamu Maisha ya Mitume Mafundisho ya Mitume


                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 344


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu. Soma Zaidi...

Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Soma Zaidi...

Maswali juu ya mtazamo wa uislamu kuhusu dini
Mtazamo wa uislamu kuhusu dini (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Athari za vita vya Uhud
Vita vya uhudi viliweza kuleta athari nyingi. Post hii itakuletea athari baadhi za vita hivyo. Soma Zaidi...

Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Soma Zaidi...

Kujiepusha na Shirk
Shirki ni kitendo chochote cha kukipa kiumbe nafasi ya Allah (s. Soma Zaidi...

Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Himizo la kuwasamehe waliotukosea
“Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Soma Zaidi...

Makatazo ya kujiepusha nayo
Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMAN
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

elimu yenye manufaa
Soma Zaidi...