MWANZO WA USALITI

Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani.

MWANZO WA USALITI

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

USALITI UNANZA HAPA

Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Ndugu zake na Zubeidah kumbwe hawakupendezwa na mafanikio ya ndugu yao. Hali hii iliwafanya kuwa na wifu na kijicho. Basi zubeidah akaongea na ndugu zake na kuwapa mali zile zote na kuwambia mimi shida yangu ni kufika salama na huyu kijana ambaye kwa sasa ni mchumba wangu na tutaoana punde tu tufikapo nyumbani. Mali zile wakagawana ndugu wawili hawa.

Hili pia halikutosha wakataka na wawaue kabisa, na kawafanya hivyo katika majira ya usiku. Waliwachukuwa wawili hawa na kuwatia baharini. Anakuja kushituka zubeida yupo baharini anakunywa maji ya chumvi na hatimaye kupoteza fahamu na asijue nini kiliendelea. Basi kwa furaha ndugu wale wakaanza kugawana tena mali zile.

Kwa upande wa Zubeidah alopokuja kupata fahamu ilikuwa ni wakati wa jioni na akajikuta amezungukwa na kundi la wananwke wenye sura nzuri za kuvutia waliojipamba vizuri sana. Mbele yake kuna kiti kirefu sana kilichopamba na magodoro yaliyochovywa kwenye dhahabu nyekundu. Miguu ya kiti hicho ni meno ya tembo yaliyopambwa vizuri. Kwa hakika kiti hicho kilikuwa na kila aina ya mapambo mazuri. Aliponyanyua kichwa akaona amekaa juu ya kiti hicho mzee wa heshima mwenye ndevu ndefu zilizo kaa vyema.

Zubeida kwa mshangao alionekana kufurahia mazingira yale na asijuwe nini kinaendelea. Alikuja msichana wa makamo hivi aliyependeza sana na akampaka maji ya marashi yaliyochanganywa na misk na kutiwa manukato mazuri sana. Zubeidah akarudisha kumbulkumnbu zake zote na akajuwa kwa mara ya mwisho alitumbukia kwenye maji sasa akawa anajiulia yupo wapi?. Yule mzee akamwambia β€œmwanangu furahia uwepo wako hapa kwa hakika hupo peponi wala kuzimu, hapa upo chini ya bahari na mbele yako ni mfalme mkuu wa majini yaendayo baharini na nchi kavu. Mzee yule akaagiza kuwa Zubeidah afanyiwe kila kinachostahiki kufanyiwa kisaha akatoweka.



Kwa shauku Zubeida alikuwa na maswali mengi sana, wakaja mabinti watatu waliokuwa na sura nzuri sana hata Zubeidah akajiona yeye si lolote wala si chochote, wakamchukuwa na kwenda nae bafunu. Huko maji yaliyo na umoto kwa mbali yalikwisha andaliwa. Kwa mara ya kwanza Zubeidaha anakwenda kuoga maji yaliyotiwa marashi pamoja na misk nyekundu, manukato mablimbali yenye kuvutia. Zubeidah alijihisi yupo ulimwengu wa raha. Kwa maringo na madaha wakamvua ngu Zubeidah na kumtumbukiza kwenye bafu lile na kuanza kumsuguwa.

Wakaendelea kumsuguwa kwa visugulio vyenye rangi ya silva vilivyochovywa kwenye marjani. Kwakweli utasema mwili wa Zubeidah umekuwa lulu iliyohifadhiwa vizuri. Uchafu wote mwilini mwa Zubeidah uliondoka hata akawa kama akawa kama aliyofanyiwa scrub na kumbakisha kama mtoto alozaliwa. Ngozi laini na nyusi za kupendeza. Hawakuishia hapo wakaendelea kumpmba na kumpaka manukato. Nguo safi za hariri zenye mapindo yalochovywa kwenye dhahabu, hakika siwezi kuelezea zaidi urembo walomchagulia.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1765

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

SAFARI YA SITA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SITA YA SINBAD.

Soma Zaidi...
Safari ya pili ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.

Soma Zaidi...
Kuelekea bonde la uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama.

Soma Zaidi...
Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME.

Soma Zaidi...
Safari saba za sinbad

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Kisiwa cha uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Safari ya tatu ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...