Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 1: Hadithi ya jini na mfanya biashara.

Hadithi hii ya jina na mfanya biashara imetoka katika kitabu cha kwanza cha simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tusikilize simulizi nzuri na zakusisimua

Jini na mfanya biashara.

 

Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara aliyejulukana kwa utajiri mkubwa sana wa mali na watoto. Alifahamika nchi nzima na aliishi maisha ya upendo na familia yake. Alitoka sikumoja katika safari zake za kibiashara. Alikuwa amepanda farasi akiwa na mfuko uiojaa tende na maji. Alifanya biashara kwa raha na amani na kuanza kurejea baada ya miezi miwili.

 

Siku ya nne baada ya kuanza safari ya kurudi alpita katika jangwa lililofahamika kwa jina la uwanja wa ujinini. Jina hili lilitumika miaka mingi iliyopita na huenda sasa limesahaulika. Mfanyabiashara huyu alipopita eneo hili akaona kuna mti wenye kivuli, hivyo akaamua kuketi ili apate kula chakula. Hivyo akawa anakula tende na kutupa punde pembeni. Alifanya hivi mpaka alipo maliza kula. Karibia na mti ule kulikiwa na kijieneo chenye maji hivyo alipomaliza kula tende zake akanawa mikono na akaswali swala zake.

 

Wakati yupo pale ghafla kulitokea upepo mkali sana na kimbunga, vumbi lilitanda eneo lile. Upepo uliambatana na moshi kisha kukatokea jini kubwa sana. “NITAKUUWA KAMA ULIVYOMUUWA MWANAGU” ni maneno ya jini yaliyosikika yakimwambia mfanya biashara. Nimefanya nini mpaka ninastahili kuuwawa?” mfanyabiashara akimwambia jini. Jini likaendelea “chagua nikuuwe namna gani.… Wakati ulipokuwa unakula tende zako ukawa unatupa punje na mwanangu alipita eneo lile ukampiga na punje yako akafa papo hapo. Hivyo lazima nikuuwe kama ulivyomuuwa mwanagu”

 

Mfanyabiashra akaendelea kumuomba jini msamaha “nisamehe mkuu, sikukusudia kumuuwa mwanao” jini kwa hasira likawa linajibu, “hakuna msamaha wala huruma hapa nitakuuwa kama ulivyomuuwa mwanangu”. Jini likatowa upanga wake kuuweka tajari kwa ajili ya kumuuwa mfanya biashara.

 

Mpaka kufika hapa Schehra-zade aligunduwa kuwa asubuhi imefika tayari na sultani anatakiwa akaswali na akahudhurie kikao cha baraza. “…. Mmmh ni hadithi nzuri sana dada nimeipenda kweli, hivi mwisho wake utakuweje?, mfanyabiashara atauliwa, au jini litamsamehe?” ni maswali aliyokuwa Dinar-zade akimuuliza dad yake Schehra-zade. “mmh ni nzuri kweli na bado huko mbele ni nzuri zaidi kama sultani ataniruhusu niishi ili kesho nikusimulie muendelezo wa hadithi hii” Schehra-zade alikuwa akimjibu mdogo wake. Sultani akamruhusu asiuliwe ali aje kuimalizia hadithi yake nzuri.

 

Siku ile sultani alitoka akiwa na tabashahsa na hata waziri wake alishangaa kuona sultani ametoka akiwa na tabasamu bla ya kutowa amri ya kumuuwa Schehra-zade kama ilivyo kawaida yake. Sultani alifanya kazi zake za kawaida huku akiwa na shauku la kutaka kujuwa mwendelezo wa kisa cha jini.

 

Usiku uliingia na ilipokaribia alfajiri, sultani hakusubiri akamwambia Schehra-zade “maliza mwendelezo wa hadithi yako, ninashauku la kuta kujuwa mwisho wake”. Basi Schehra-zade akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-

 

Basi yule mfanya biashara alivyoona jini anakaribia kumkata upanga akapiga magoti na kumwambia jini “tafadhali mkuu nina neno naomba unisikilize, nina familia mkuu na nina madeni naomba unipe muda angalau nikaiage familia yangu na kulipa madeni yangu”. “Unataka nikuachie ili ukimbie?” ni jini akimjibu mfanya biashara. “hapana na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitarejea hapa hapa, naweka ahadi mbele ya Mwenyezi Mungu” haya maneno aliyasema mfanya biashara.

 

Baada ya kufikiri jini likamuuliza “haya ni muda wa siku ngapi nikupe” naomba unipe mwaka mmoja” akamjibu. Basi jini lile likakubali kichukuwa ahadi ile na likamwacha mfanya biashara papepale na likotoweka. Mfanya biashara akaondoka akiwa na mjonzi makubwa. Alipofika kwake akaieleza familia yake yote yaliyompata.

 

Hakuwa na muda wa kupoteza akalipa madeni yake na kuweka akiba ya kuweza kutumiwa na familia yake pindi atakapo ondoka. Mwaka haukuwa mrefu hatimaye miezi 12 ikawadia. Mfanya biashara kwa majonzi na masikitiko akaaga familia na akaondoka kwenda kutekeleza ahadi yake. Alifika eneo la tukio na kumsubiri jini aje.

 

Katika hali kama hivyo akiwa amekaa kumsubiri jini katokea mzee mmoja akiwa na mbuzi wake. Alistaajabu mzee yule kuona mtu eneo lile hatari. Akmuuliza hasa yaliyomkuta kukaa eneo lile, akampa kisa kizima. Kiasha yule mzee kamwambia “nitakaa hapa hapa na mimi nishuhudie kitakacho tokea”. Punde akatokea mzee mwingine akiwa na mbwa wawili weusi. Naye akataka habari ya kilichowakuta wenzie wale mpaka wakakaa pale. Akasimuliwa kisa kizima, na yeye akabaki pale ili ashuhudie kitakacho endelea. Akaja mzee wa tatu akiwa na mbwa wake mwekundu na akapewa habari na akakaa ili aone kitakacho endelea.

 

Punde wakaona moshi uliofatana na upepo na likatokea jini kubwa lililoshika upanga mkononi mwake. Jini lile haliku msemesha yeyoye likamfuata mfanya biashara na kumwambia “simama ili nikuuwe kama ulivyo muuwa kijana wangu sasa hivi sina huruma leo”.

 

Pale yule mzee mwenye mbuzi akajitupa miguuni mwa jini kisha kwa hisia kubwa kamwambia “ewe mkuu wa majini wa eneo hili, naomba usikiklize hadithi yangu na huyu mbuzi nilyekuwa naye hapa. Kama utaiona inastaajabisha kuliko tukio hadithi ya mwanao na mfanya biashara huyu, iwe kama fidia ya kupunguzia adhabu:. Jini lifafikiri kwa muda na kisha likasema “vizuri sana ebu tuangalie hadithi yako”. Basi mzee yule akaanza kusimulia hadithi yake kama ifuatavyo;-






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-09 12:45:13 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 128


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 4: Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu.
Hadithi za HALIF LELA U LELA hii ni moja wapo imetoka katika kitabu cha kwanza imaelezea kisa cha mzee wa tatu.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 3: Aladini akiwa na binti wa mfalme
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 15: Mji uliogeuzwa mawe
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 7: Hadithi ya safari ya majibu juu ya maswali mawili
Wapendwa wasomaji na wasikilizaji wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tuendelee kusikiliza hadithi zetu mzuri na za kusisimua.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 20: Kinyozi maishani mwangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 5: Bonde la uokozi
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4  Part 13: Simulizi ya nyani kibadilika kuwa chongo
Mwendelezo wa hadithi zetu nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 13: Jaribio kwa Aladini kwa mara ya kwanza
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 8 Part 1: Hadithi ya tunda
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 14: Hadithi ya kifo cha kujionea
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Muendelezo wa safari ya Sinbad Soma Zaidi...