Simulizi hii inatoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadidhi za HALIF LELA U LELA.
Kiapo cha Sultan
Hapo zamani sana katika nchi za Uajemi , china na hindi kulitokea sultani aliyefahamika kwa kuwa na upendo kwa watu wake na nguvu pia ya kijeshi na kuitawala. Watu wake walimpenda sana na yeye aliwapenda. Sultani huyu alikuwa na watoto wawili ambao ni Shahriyar ambaye ndiye mkubwa na mwingine ni Shahzanam ambaye ndiye mdogo.
Watoto hawa pia walitambulika kwa ushujaa walio nao na uhodari katika mambo mbalimbali, hususan katika fani ya kupanda farasi. Sultani huyu alipofariki utawala wake akamwachia mwanaye mkubwa ashike madaraka yake. Na mwanae mdogo akabakia anatawala maeneo mengine katika utawala wa baba yake. Huyu mdogo akaelekea maeneo ya Samarkand na huyu mkubwa akabaki palepale.
Sultan Shahriyar alikuwa na mke wake aliyempenda sana kwa muda mrefu. Hakuwahi kuamini kama itaweza kutokea sikumoja akamsaliti. Ilitokea sikumoja akamkuta mkewake anazini na mtumwa wake. Kitendo hiki kilimuuma sana na akamuuwa mkewe na yule mtumwa. Kutokea hapo akaapa kutokumwamini mwanamke yeyote duniani. Na kitendo hiki kilimfanya ajiwekee utataratibu mpya wa maisha nao ni kuoa kila siku mke mpya na kisha humuuwa ifikapo asubuhi.
Hivyo mambo yakawa kama hivi kila siku jioni bibi harusi mpya mwanamwari huolewa na na ikifika asubuhi huuliwa. Kitendo hiki kiliendelea kwa muda mpaka watu wakawa wanaogopa. Ikiwa nyumba moja watu wanalia kwa kufiwa na bint yoa nyumba nyingine hufanyika harusi. Sultani alikuwa na waziri wake maalum ambaye alikuwa amepewa kazi hii ya kumletea mfalme wanawari na kutekeleza amri ya kuwauwa kila ifikapo asubuhi.
Waziri huyu aliyepewa kazi hii alikuwa na watoto wawili aliyewapenda sana, mmoja aliitwa Schehra-zade ambaye ndiye mkubwa na Dinar-zade ambaye ndiye mdogo. Schehra-zade alipata upendo mkubwa kutoka kwa baba yake. Alipewa taaluma mbalimbali za matibabu, sanaa, kuandika, masimulizi , kazi za mikono na nyingine nyingi. Ukiacha mbali na taaluma hizi pia alijulikana kwa uzuri wake ulioaminika kuwashinda wanawake wote katika nchi hiyo. Mabinti wawili hawa walipendana zaidi kila mmoja.
Ilitokea siku moja katika mazungunzo waziri mkuu akiwa na mabinti zake wanaongea Schehra-zade alitowa ombi kutoka kwa baba yake ambalo lilionekana kumshangaza sana. “baba ninaombi ila niahudi kwanza kuwa utanitekelezea” alizungumza Schehra-zade kumwambia baba yake. “naahidi nitalitekeleza kama lipochini ya uwezo wangu” alisikika waziri mkuu akimjibu binti yake.
“ninataka kukomesha tabia ya kikatili ya sultani kuuwa mabint” mmmmhhh mwanangu kipenzi, vip utaweza kumaliza tabia hii ya sultani wetu? Ni maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kati ya waziri na mwanae. “baba ninataka unipeleke mimi kwa sultani niwe mkewe” alizungumza Schehra-zade. Mwanangu unafahamu fika kuwa ukuolewa punde tu ifikapo asubuhi nitaamriwa nikuuwe” alizungunza waziri kwa masikitiko makubwa.
Schehra-zade aliendelea kusisitiza ombi lake la kutaka kuolewa na sultani ili akamalize tabia yake ya kuuwa mabinti. Waziri nae hauacha kumsihi mwanae asithubutu kijiingiza kwenye matatizo haya makubwa. Wazii akawa anamwambia mwanae “ hivi mwanangu unataka nikufanye kitugani mpaka uachane na msimamo wako huo? Au unataka yakupate yalompata mke wa mfugaji?” kwa shauku Schehra-zade akauliza “kwani baba ni kitu gani kilimpata mke wa mfugaji” mmmmhh.. Ni habari kubwa lakini nitatakusimulia hadithi yake” alizingumza waziri na kuanza kusimulia hadithi hii. Mwisho wa simulizi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-09 12:37:45 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 206
Sponsored links
š1
Simulizi za Hadithi Audio
š2
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
š3
Madrasa kiganjani
š4
Kitau cha Fiqh
š5
kitabu cha Simulizi
š6
Kitabu cha Afya
Simulizi za HadithiĀ EP 7 Part 12:Ā Dirisha moja kwanini????
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 9 Part :Ā Taharuki kwa mfalme
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 9 Part :Ā Nurdini na Barua ya mfalme wa baghadad
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 6 Part 12:Ā Tabibu asimulia hadithi
Hii ni hadithi iliyopo ndan ya kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 5 Part 8:Ā Hadithi ya kisiwa cha uokozi
Simulizi hii ipo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 6 Part 15:Ā Baba tajiri na kifo chake
Muendelezo....... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 9 Part :Ā Nudhini na mtumwa
Muendelezo....... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 6 Part 21:Ā Kinyozi mwenyewe
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 4 Part 15:Ā Mji uliogeuzwa mawe
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za HadithiĀ EP 4 Part 14:Ā Simulizi ya binti wa kwanza na mbwa
Tuendeleee kuburudika na simulizii zetu nzuri kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...