Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari?Hapana kiwango maalum cha mahari kilichowekwa na Sheria ya Kiislamu. Mahari ni haki ya mwanamke mwenye kuolewa na ndiye pekee mwenye uhuru kamili wa kutaja kiasi cha mahari anachokitaka. Akipenda anaweza kudai mrundi wa dhahabu na fedha (Qur-an: 4:20), au akitaka anaweza kupokea kiasi kidogo sana cha mali kama vile shilingi 1/- au chini zaidi kuliko hivyo au akitaka anaweza akasamehe asitake kitu chochote ila kauli nzuri tu.Lakini tunashauriwa katika Qur-an kuwa mtoaji mahari na mpokeaji mahari waangaliane hali. Kama hali ya mtoaji ni nzuri, ni vyema azidishe mahari kuliko kile kiasi kilichotajwa iwapo ana uwezo huo. Na mpokeaji wa mahari, endapo ataona hali ya mtoaji si nzuri kiuchumi, basi ampunguzie mahari na apokee kiasi kidogo zaidi ya kile alichokitaja mwanzoni. Huku kuangaliana hali kunazidisha mapenzi na huruma baina ya mume na mke.Pamoja na kuwa mahari hayana kiwango maalum kilichowekwa, inashauriwa yasiwe ya juu sana kiasi cha kuifanya ndoa kuwa jambo gumu na kurahisisha uzinifu katika jamii. Hebu tuusikilize ushauri wa Umar bin Khattab (r.a) (Khalifa wa Pili wa Mtume (s.a.w) ambaye amesema:


"Kuweni waangalfu msfanye mahari ghali. Ingelikuwa kufanya hivyo ni jambo zuri la kumpelekea mtu kwenye ucha-Mungu, Mtume (s.a.w) angelikuwa wa kwanza katikajambo hilo. Sikumbuki kumuona Mtume (s.a.w) katika lwmuoa yeyote katika wake zake au katika lwwaoza yeyote katika binti zake kwa zaidi ya Wakia 12.5 (lwmi na mbili na nusu) ambazo ni sawa na Dirham 500".Pia katika hadithi iliyosimuliwa na Jabir (r.a) Mtume (s.a.w) amesema: Atakayetoa viganja viwili vya tende au shairi kama mahari ya mkewe (naye akaridhia) atakuwa ameufanya uchi wa mkewe uwe halali kwake. (Abu Daud).