Kupanga Uzazi katika UislamuKama ilivyo haramishwa kwa jamii, Uislamu umeharamisha pia kudhibiti uzazi kwa mtu binafsi kwa khofu ya kushindwa kuwalisha au visingizio vingine. Hata hivyo Uislamu haujawataka watu wazae kiholela. Kwanza umekataza watu kuzaana nje ya ndoa. Pili, walioona wanatakiwa wazingatie umri baina ya mtoto na mtoto mwingine. Kwa anayetaka kukamilisha muda wa kunyonyesha, basi amnyonyeshe mtoto wake kwa miaka mwili:


Na wanawake waliozaa wawanyonye.she watoto wao miaka miwili kainilz kwa anayetaka lwkamilisha lwnyonyesha..." (2:233)Kunyonyesha humsababisha mama mzazi kuchukua muda mkubwa kabla ya kuingia tena katika siku zake. Iwapo mwanamke atapata siku zake wakati mtoto yungali mchanga (hajafikia umri wa miaka miwili), anatakiwa ajizuie asipate mimba; kwani katika Hadith iliyosimuliwa na Imamu Muslim, Mtume (s.a.w) amesema kuwa mwanamke akipata mimba wakati yungali na mtoto mchanga, afya ya mtoto hudhurika. Njia za kuzuia mimba katika kipindi hiki cha kunyonyesha ni zile ambazo hazina madhara ya kiafya kwa baba wala mama. Katika Hadith iliyopokelewa na Bukhari na Muslim, Jabir (r.a) amesema kuwa wakati wa Mtume (s.a.w) wao walikuwa wanatumia njia ya kuzuia mimba inayoitwa 'azal" (with drawal au coitus interuptus), yaani njia ya kumwaga mbegu za uzazi nje lakini Mtume (s.a.w) hakuikataza.Hapa ifahamike kwamba suala Ia kupanga juu ya muda wa kunyonya mtoto linamhusu baba na mama na si suala Ia kuwekewa sera na taifa; kwani hali za watu zinatafautiana.Ama kwa mama atakayekuwa na matatizo ya kiafya, ikathibiti kuwa akibeba mimba atadhurika au kuhatarisha maisha yake, anaruhusiwa kufunga kizazi hata kutoa mimba ambayo imeshatunga.Hitimisho juu ya Kudhibiti uzazi
Tumeona kuwa kuongezeka kwa watu si tatizo kwani hakuna tatizo Ia riziki kama wale wasiomtegemea Allah (s.w) wanavyodai. Hivyo, kuwapangia watu wazae watoto idadi Fulani ni kinyume kabisa na mafundisho ya Uislamu. Wajibu wa mwanadamu ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, na pia kuweka utaratibu mzuri wa mgao wa rasilimali katika jamii.Uislamu umekemea vikali zinaa na kuweka adhabu kali kwa wazinifu. Sera ya kudhibiti uzazi na Elimu ya ngono (sex education) ni nyenzo "nzuri sana na madhubuti" za kupalilia zinaa katika jamii. Katu waislamu hawatazikaribisha. Huu ndio msimamo wa Uislamu juu ya suala Ia kudhibiti uzazi na waislamu wa kweli daima watakuwa katika msimamo huu kwani:


Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume, hakika amepotea upotofu ulio wazi kabisa. (33:36)