(a) UgirikiTunajifunza katika historia ya Ulimwengu kuwa jamii ya Wagiriki ilikuwa miongoni mwa jamii zilizoanza kustarabika.
(a) Ugiriki
Tunajifunza katika historia ya Ulimwengu kuwa jamii ya Wagiriki ilikuwa miongoni mwa jamii zilizoanza kustarabika. Lakini utakuta kuwa hadhi ya mwanamke katika jamii hiyo ilikuwa chini sana. Bwana E.A. Allen katika kitabu chake "History of Civilization Vol. 3" anasema mwanamke wa Kigiriki alilazimishwa kuolewa pasina idhini yake. Mumewe huyo alihesabiwa kuwa Bwana (Lord) wake. Mwanamke alihesabiwa kuwa ni kama mtoto na kwahiyo alitakiwa kumtii mumewe bila kuhoji. Wanawake huko Ugiriki waligawanyika katika makundi matatu:
(i)Makahaba (Malaya) ambao kazi yao ilikuwa ni kuwastarehesha wanaume tu.
(ii)Watumishi ambao kazi yao ilikuwa kuangalia na kutunza siha za mabwana zao.
(iii)Wake amabo kazi yao ni kuzaa na kulea watoto.
Mke alitakiwa awe mwadilifu na achunge murua wake lakini haikuwa vibaya kwa mwanamume kujamii nje ya ndoa. Matokeo ya utaratibu huu ni kuwa wanawake makahaba wakawavutia watu wa ngazi zote - wanafalsafa, washairi, wanahistoria, wanafasihi na wasanii. Picha na sanamu za wanawake walio uchi zikazidi kuchochea zinaa na ufasiki. Ndoa ikaja kuonekana kuwa kero na zinaa ikawa jambo takatifu. Kuzama katika uzinifu kuliwapeleka Wagiriki kuchonga na kuabudu Aphrodite - mungu wa kike wa urembo na mahaba.
Kwa mujibu wa mafundisho ya Wagiriki ni kuwa huyo "Aphrodite" anasemekana kuwa alikuwa ni mungu wa kike aliyeolewa na mungu mwingine. Lakini hakutosheka na mume huyo mmoja. Akaanza kuzini na miungu wengine watatu na akawa pia anazini na binaadamu mmoja. Mungu huyo alipofanya jimai na binaadamu, wakazaa mungu wa kiume aliyeitwa Cupid yaani mungu wa mapenzi. Uzinifu wa "Aphrodite" na kuabudiwa kwake na Wagiriki ni kielelezo cha namna jamii hii iliwatukuza makahaba na kuupa uzinzi hadhi kubwa.
Kutokana na haya tunajifunza kuwa mwanzoni mwanamke katika jamii ya Ugiriki alidunishwa sana. Baadaye jamii ilipopiga hatua mbele katika maendeleo ya kiuchumi, hadhi duni ya mwanamke ilibadilishwa sura. Mwanamke aligeuzwa kuwa chombo cha kuwastarehesha wanaume jambo ambalo lililzidi kumdunisha na kumdhalilisha.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inakwendabkukujiulisha maana ya twahara na jinsi ya kujitwaharisha.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu.
Soma Zaidi...Taratibu za Kutaliki KiislamuKama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu,kutoa zakat na sadaqat (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh.
Soma Zaidi...Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria.
Soma Zaidi...