Pera ni tunda bora lakini pia ni dawa, tambua umuhimu wa tunda hili kiafya
Pera ni katika matunda yanayopatikana maeneo mengi duniani. Tunda hili ni katika matunda yenye kutia afya zaidi katika miili yetu hasa kwa wale wenye maradhi sugu. Tunda hili hutumika mapaka majani yeke na kuleta faida nyingi sana. Hata wazee wetu wa zamani walikuwa wakitumia mmea huu kwa ajili ya tiba asili. Sasa hebu tuanze kuziona faida hizo:-
Katika tafiti iliyofanyiwa watu 19 imethibitisha kuwa kunywa majimaji yatokanayo na majani ya mpera husaidia katika kushusha kiwango cha sukari na athari hii huweza kuendelea mpaka masaa mawili. Tafiti nyingine aliyofanyiwa watu 20 wenye aina ya kisukari type 2 diabetes waliligundulika kuwa kunywa majani ya mpera kumeshusha sukari kwa asilimia 10%.
Pia kiwango cha madini ya potassium (chumvi) iliyomo kwenye pera pamoja na kambakamba zilizomo kwenye pera husaidia katika kuimarisha afya ya moyo. Pia ulaji wa mapera unaweza kuondoa cholesterol zilizo mbaya (LDL cholesterol) na kuongeza cholesterol nzuri). Hivyo hupunguza nafasi ya kupata maradhi ya shinikizo la damu la juu yaani presha ya kupanda na kupata kiharusi yaani kupalalaizi. (stroke).
Tafiti iliyofanyiwa wanawake 197 ambao huwa wanapata maumivu wakati wa kupata sikuzao, tafiti imeonesha kuwa unywaji wa miligram 6 za maji ya majani ya mpera husaidia kupunguza maumivu haya. Pia utafiti zaidi umeonesha kuwa majani ya mpera husaidi kupunguza maumivu haya mara dufu tofauti na kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia tafiti zinaonesha kuwa majani ya mpera hupunguza maumivu wakati wa kukojoa kwa wale wanaopata maumivu haya.
Pia majani ya pera yakitengenezwa majimaji yake husaidia katika kuboresha afya ya mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula. Kwa wale wenye tatizo la kuharisha majani ya mpera ni mujarabu sana katika kuondoa ama kupunguza tatizo. Pia kuna tafiti nyingi zinaonesha kuwa pera husaidia katika kuuwa vijidudu vibaya ndani ya matumbo yetu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Nyanya ni katika viungio vya mboga, kuna faida kubwa za kiafya katika nyanya
Soma Zaidi...Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya vyakula na vinywaji vilivyo salama kwa mtu mwenye kisukari, na ni vyakula vipi ni hatari kwa mwenye kisukari. Pia utajifunza njia za kujilinda na kupata kisukari.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula salama kwa mwenye kisukari
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida anazozipata mtu anayekula mayai hasa wakati wa kifua kinywa, tunajua wazi kuwa mayai yana kiwango kikubwa cha protini pamoja na hayo kuna faida nyingi za kutumia mayai hasa wakati wa asubuhi kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin E
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...