Suratul – Bayyinah (98): Imetereshwa Madinah; Ina Aya 8
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1. Wale waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina (walitoa ahadi kuwa) hawataacha (waliyonayo) mpaka iwajie hoja (iliyodhahiri ya kuonesha upotofu wa dini yao).
2. (Naye ni) Mtume aliyetoka kwa Allah anayewasomea kurasa zenye kutakaswa.
3. Ndani yake humo zimo sharia madhubuti.
4. Wala hawakufarikiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia hoja hiyo
(waliokuwa wakiitaka).
5. Wala hawakuamrishwa ila kumuabudu Allah kwa kumtakasia dini na waache dini za upotofu (upotevu), na wasimamishe Swala na watoe Zakat. Hiyo ndiyo dini iliyo sawa (nao wameikataa).
6. Bila shaka wale waliokufuru miongoni mwa watu waliopewa Kitabu na washirikina wataingia katika moto wa Jahannam; wakae humo milele; hao ni waovu wa viumbe.
7. Hakika walioamini na kutenda mema, basi hao ndio wema wa viumbe.
8. Malipo yao kwa Mola wao ni pepo ya daima ambayo mbele yake inapita mito, watakaa humo milele; Allah amewaridhia, nao wameridhika (na malipo). Hayo ni kwa yule anayemuogopa Mola wake.
Mafunzo ya sura hii kwa ufupi:
1. Katika zama zetu hizi muongozo pekee wa kumuongoza mwanaadamu ni Qur’an
kama alivyokuja nayo Mtume (s.a.w).
2. Mayahudi, Wakristo na Washirikina wengine wamehiari kuendelea kuwepo katika upotofu kwa jeuri licha ya kuwajia Mtume (s.a.w) na uongofu wa haki.
3. Wana adhabu kali wale waliokufuru na kufuata dini na njia za upotofu (upotevu)
baada ya kuwajia na kuijua haki.
4. Wenye kufanya amali njema watakuwa na malipo mazuri ya pepo ya kudumu na milele kwa Mola wao.
5. Kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo ni pamoja na kumtakasia dini yake kwa kusimamisha swala na kutoa zakat.
Suratut – Tiyn (95): Imeteremshwa Makkah; Ina Aya 8
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1. Naapa kwa tini na Zaituni (chini ya miti hiiamepata Utume Nabii Ibrahim na Nabii
Nuhu).
2. (Na) kwa mlima Sinai (amepata Kitabu hapo Nabii Musa).
3. Na kwa mji huu wenye amani (wa Makka alipopelekewa Utume Nabii
Muhammad).
4. Bila shaka tumemuumba mwanaadamu kwa umbo lililo bora kabisa.
5. Halafu tukamrejesha chini kuliko walio chini.
6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, watakuwa na ujira usiokwisha
(unaoendelea kwa Mola wao).
7. Basi lipi likupalo kukadhibisha (kukanusha) malipo baada (ya kuona hayo)?
8. Je, Mwenyezi Mungu si Hakimu muadilifu kuliko Mahakimu wote?
Mafunzo ya sura hii kwa ufupi:
1. Allah (s.w) pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuapia kiumbe chake chochote na mwanaadamu anaruhusiwa kuapa kwa jina la Allah (s.w) pekee.
2. Umbile la mwanadamu ni katika dalili za kuonesha kuwepo na uwezo wa Allah
(s.w).
3. Ubora wa mwanadamu hupatikana kutokana na imani sahihi ikiambatanishwa na vitendo vizuri pia.
4. Ni lazima iwepo siku ya hukumu ili waumini waliotenda wema walipwe wema wao na waliotenda uovu walipwe uovu wao mbele ya Hakimu muadilifu (Allah (s.w)).
Suratun – Nash-rah (94): Imetereshwa Makka; Ina aya 8
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1. Je, hatukukupanulia kifua chako?
2. Na tukakuondolea mzigo wako (mambo mazito mazito)?
3. Uliovunja mgongo wako?
4. Na tukakutukuza utajo wako (unapotajwa)?
5. Basi kwa hakika baada ya dhiki (huja) faraja
6. Hakika baada ya dhiki huja faraja.
7. Basi ukishamaliza (kulingania) shughulika kwa ibada
8. Na jipendekeze kwa Mola wako.
Mafunzo ya sura hii kwa ufupi:
1. Mitume huteuliwa na kuandaliwa na Allah (s.w) mwenyewe hata kabla ya kupewa
Utume (Mitume huzaliwa wakiwa mitume).
2. Mwenyezi Mungu (s.w) humuongoza mtu aelekeaye kwake kwa kutaka kuongoka.
3. Mafanikio yoyote hupatikana baada ya juhudi za kibinaadamu kufanyika kisha kumtegemea Allah (s.w).
4. Ni wajibu kwa Waislamu kutumia rasilimali ya muda na wakati vilivyo katika kufanya ibada.
5. Subira na uvumilifu ni katika nyenzo muhimu sana katika kulingania na kusimamisha Uislamu katika maisha ya jamii.
Suratu Dhuhaa (93): Imeteremshwa Makka; Ina Aya 11.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1. Naapa kwa mchana
2. Na kwa usiku unapotanda
3. Hakukuacha Mola wako wala hakukukasirikia (wewe Muhammad)
4. Na bila shaka (kila) wakati ujao (utakuwa) ni bora kwako kuliko uliotangulia
5. Na Mola wako atakupa mpaka uridhike
6. Je, Hakukukuta yatima akakupa makazi (mazuri ya kukaa)?
7. Na akakukuta hujui kuongoza njia, akakuongoza?
8. Na akakukuta fakiri, akakutajirisha?
9. Basi usimuonee yatima
10. Wala usimkaripie aulizaye
11. Na neema ya Mola wako isimulie (kwa kushukuru na kwa kufanya amali njema)
Mafunzo ya sura hii kwa ufupi:
1. Mwenyezi Mungu (s.w) kama Muumba na Mmiliki wa kila kitu ana uwezo wa kuapia kitu chochote.
2. Nusura na msaada wa Mwenyezi Mungu hupatikana baada ya Waislamu kufanya jitihada za kibinadamu
3. Harakati za kusimamisha Uislamu hutegemea juhudi na mikakati ya waislamu kwa wakati husika.
4. Binadamu anatakiwa awachunge na kuwaangalia wale walioko chini yake
5. Mwenyezi Mungu (s.w) pekee ndiye mdhibiti wa mafanikio au shida zote za wanadamu.
6. Tunawajibu wa kushukuru neema za Allah (s.w) na njia bora za kushukuru ni kutekeleza maamrisho yake.
Suratul A’laa (97): Imetereshwa Makka; Ina Aya 19
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
1. Litukuze jina la Mola wako aliyemtukufu
2. Aliyeumba (kila kitu na) akakitengeneza
3. Na akakadiria (kila kitu) na akakiongoza
4. Na aliyeotesha ndisha (malisho)
5. Kisha akayafanya makavu yenye kupiga weusi
6. Tutakusomesha (ewe Muhammad na) wala hutasahau
7. Ila akipenda Mola wako Mwenyezi Mungu, Yeye anayajua yaliyodhahiri na yaliyofichikana.
8. Nasi tutakusahilishia (kuitangaza) dini (kwa njia) iliyo nyepesi.
9. Basi kumbusha, ikiwa kutafaa kitu (ukumbuso huo)
10. Bila shaka atakumbuka mwenye kumuogopa (Mwenyezi Mungu).
11. Na atajitenga na ukumbusho huo aliyemuovu
12. Ambaye ataungia moto mkubwa.
13. Kisha humo hatakufa wala hatakuwa hai
14. Hakika amekwisha faulu aliyejitakasa (na mabaya)
15. Akakumbuka jina la Mola wake na akaswali
16. Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya dunia
17. Hali ya kuwa Akhera ni bora (zaidi kabisa) na yenye kubaki (kudumu)
18. Hakika haya (mnayoambiwa humo katika Qur’an) yamo katika vitabu vilivyotangulia.
19. Vitabu vya (Nabii) Ibrahim na Musa.
Mafunzo ya sura hii kwa ufupi:
1. Mwenyezi Mungu (s.w) pekee ndiye anayestahiki kutukuzwa na kusifiwa.
2. Kila kilichoumbwa kitakufa (kina mwisho wake isipokuwa vile apendavyo Allah)
3. Qur’an imehifadhiwa na Mwenyezi Mungu (s.w), hata hivyo juhudi kubwa inatakiwa ifanywe katika kuijua na kuifundisha vilivyo kwa lengo lake.
4. Kuwaonya na kuwakumbusha watu juu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu (s.w) ni lazima.
5. Kila anayepuuza ukumbusho wa Allah (s.w) na kuendelea kufanya mauovu atapata adhabu iumizayo.
6. Hatuna budi kuyapenda na kuyapupia zaidi maisha ya Akhera kwani ni bora kuliko ya dunia na ni yenye kudumu.
7. Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wanaadamu wote ni moja tu ambayo ni
Uislamu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 476
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...
Zijuwe suna (sunnah) za Udhu ama Kutawadha
Soma Zaidi...
Vituo vya kunuia ibada ya hija
Soma Zaidi...
Ndoa ya mke zaidi ya mmoja na taratibu zake
Soma Zaidi...
Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo
Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...
MAFUNZO YA QURAN: QURAN NA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Soma Zaidi...
Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa
Soma Zaidi...
Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee
1. Soma Zaidi...
swala za tahiyatu al masjid, qabliya na baadiya
Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid. Soma Zaidi...
Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...
Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii
1. Soma Zaidi...