i.
i. Dai kuwa Qur’an ni mashairi aliyotunga Muhammad (s.a.w)
- Maquraishi wa Makka walidai kuwa Qur’an ni mashairi aliyotunga
Muhammad kwa ujuzi na ueledi mkubwa wa historia ya Waarabu.
Udhaifu wa dai hili:
- Ujumbe wa Qur’an unatofautiana sana na ule wa mashairi kimvuto na taathira kama mshairi mashuhuri Labiib Ibn Rabiah alikiri hilo.
ii. Dai kuwa Qur’an ni zao la njozi za Mtume (s.a.w) zilizovurugika
- Waandishi kama akina Anderson na Watt walidai kuwa Qur’an ni zao la
mawazo na dhana tu za Muhammad zilizovurugika.
Udhaifu wa dai hili:
- Dhana hizi hazina ukweli wowote kwa sababu haijawahi kutokea katika historia ya mwanaadamu kuuunda kitabu kwa ndoto mithili ya Qur’an. Rejea Qur’an (21:5)
iii. Dai kuwa Qur’an ni zao la mwenye kifafa na aliyepagawa na shetani
- Baadhi ya waandishi wa kikafiri wamedai bila ushahidi wowote kuwa
Mtume Muhammad (s.a.w) alitunga Qur’an akiwa katika hali ya kifafa.
Udhaifu wa dai hili:
- Dai hili halina ukweli wowote kwani haijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu mtu mwenye kifafa kuunda Kitabu chenye wafuasi wengi. Rejea Qur’an (10:38)
iv. Dai kuwa Qur’an ni aya za shetani
- Salman Rushdie alidai kuwa Muhammad hakushukiwa na wahyi wowote
isipokuwa ni mawazo yake akiongozwa na shetani katika kuandika Qur’an.
Udhaifu wa dai hili:
- Qur’an yenyewe inadhihirisha kuwa si aya za shetani, na kama ingelikuwa
ni aya za shetani kwa nini adhhirishe uadui wake kwa wanaadamu?
Rejea Qur’an (81:25), (6:112), (35:6), (17:88), (4:82)
v. Dai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliandika Qur’an kwa msaada wa Mayahudi na Wakristo
- Makafiri wanadai kuwa Mtume (s.a.w) aliandika Qur’an kwa kunakili
mafundisho ya Biblia kutokana na baadhi ya aya kufanana.
- Pia wanadai kuwa alifundishwa na Ujumbe wa Qur’an alipokutana na Padri
Bahirah katika safari yake ya Shamu akiwa na miaka 12.
Udhaifu wa madai haya:
- Mtume Muhammad (s.a.w) hakujua kusoma wala kuandika na alisema
Qur’an inatoka kwa Allah (s.w) vinginevyo ingelikuwa na hitilafu nyingi.
- Nakala ya kwanza ya Agano la Kale iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiarabu ilipatikana miaka 200 baada ya kutawafu (kufa) Mtume (s.a.w).
- Mtume (s.a.w) alikutana na Padri Bahirah akiwa na miaka 12, sio jambo rahisi kufundishwa ujumbe muda huo na aje kuufundisha baada ya miaka
28.
Rejea Qur’an (16:103)
vi. Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur’an ili kuleta umoja na ukombozi wa
Waarabu
- Wako baadhi ya Makafiri wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga
Qur’an ili awaunganishe na kuwakomboa Waarabu.
Udhai wa dai hili:
- Dai hilo sio la kweli kwa sababu hakuna msisitizo wowote ndani ya Qur’an juu ya ukombozi na umoja wa Waarabu na Qur’an inapingana na ukabila.
- Pia Mtume (s.a.w) angelikubali pendekezo la Maquraishi kuwa kiongozi wa
Waarabu ili atumie fursa hiyo kujenga umoja wa Waarabu.
Rejea Qur’an (3:42)
vii. Dai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur’an ili kurekebisha tabia za
Waarabu.
- Wapo Makafiri wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur’an ili
kujenga mwenendo na tabia nzuri za ndugu zake Waarabu.
Udhaifu wa dai hili:
- Kujenga tabia na mwenendo mzuri wa watu ni jambo zuri ambalo halihiajii kutumia udanganyifu au uongo wa aina yeyote.
Rejea Qur’an (6:93), (5:101)
viii. Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur’an ili ajinufaishe kiuchumi.
- Baadhi ya watu wanadai kuwa Muhammad (s.a.w) kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi.
Udhaifu wa dai hili:
- Kama Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur’an kujinufaisha kiuchumi mbona
hali yake kiuchumi ilizidi kuwa duni hata baada ya Utume.
Rejea Qur’an (33:28-29)
ix. Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur’an ili kuwania madaraka na ukubwa
- Makafiri wamedai pia kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur’an ili kujipatia
madaraka na ukubwa kwa Waarabu.
Udhaifu wa dai hili:
- Mtume Muhammad (s.a.w) ni mtu aliyejulikana sana ulimwenguni, hivyo
hakuwa na haja ya kutumia Qur’an kuomba madaraka.
- Mtume (s.a.w) mwenyewe alikataa ofa ya kuwa kiongozi wa Waarabu walipomtaka ili aache kazi ya kulingania Uislamu.
Rejea Qur’an (9:61), (45:9), (28:86), (18:110), (6:50)
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 836
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
TAFSIRI (TARJIMA) YA QURAN KWA LUGHA YA KISWAHILI
Tafsiri ya Quran kwa iswahili iliyotafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-BArwani Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani. Soma Zaidi...
Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)
Soma Zaidi...
Hukumu ya zakat Al-Fitir na namna ya kuitoa zaka ya fitir
Soma Zaidi...
HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...
SIRA (HISTORIA YA ) MTUME MUHHAMAAD (S.A.W) KUZALIWA KWAKE, VITA ALIVYOPIGANA, SUNNAH ZAKE NA MAFUNDISHO YAKE
Soma Zaidi...
Ni nini maana ya ndoa?
Soma Zaidi...
Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo
Soma Zaidi...
Sifa na vigezo vya dini sahihi
1. Soma Zaidi...
ushahidi juu ya Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W)
Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S. Soma Zaidi...