FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI

FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI


FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI:



Aladini akiwa mbele ya mfalme alionekana kuwa ni mtoto mtiifu sana na ni wa kipekee anayestahiki kuwa mkwe wa Mfalme. Hali hii ilimfanya mfalme kuridhika sana na chaguo lake na maamuzi. Mfalme alihisi kuwa waziri alikuwa akimpeleka mbali hasa kutaka kumuozesha mwanaye kwa kumchafulia aladini. Japo mfalme alikuwa na mambo anataka kuyafahamu kuhusu Aladini amepata wapi utajiri ule, na ni nani hasa. Mfalme aliamini kuwa ipo siku Aladini atamueleza yeye mwenyewe ama ipo siku atakuja kutambua. Basi kwa bashasha na mapenzi Mfalme akasalimiana na mkwe wake pamoja na mwanaye kipenzi.


Watatu hawa wakakaa kwenye viti hali ya kuangaliana. Viti vilivyopambwa vyema katikati ya bostani la Mfalme ndani ya ikulu. Viti vilikuwa juu ya yasi za kijani sana kwa ubichi, zilipendeza mno. Maua mazuri yenye rangu za kuvutia. Bostani lilijawa na harufu nzuri ya maua na wadudu walioonekana kupendezesha sana wakiwa wanakula nta ya maua. Nyuki wakubwa wa rangi ya njano utadhani ni dhahabu zilizokuwa zikipepea. Nyuki hawa walimkumbusha sana Aladini alipokuwa pangoni. Mfalme alikuwa muda wote mwenye furaha alipomuangalia Aladini mkwe wake. Binti Mfalme alipatwa na wivu kuona sasa mapenzi ya baba yanahamia kwa Aladini. Baba hamuangalii tena mwanaye kwa upendo kama zamani. Ila aliamua kupotezea kwani alianimi Aladini ni mwe tu kwa vyovyote vile.


Wajakazi waliovalia vyema walikuja mbele na kuweka vyakula laini kwa ajili ya kufungulia kinywa. Ukimya ulitawala kwa muda huku Aladini akiangalia kwenye mjengo ulioonekana ni mgeni kwenye mji. Wajakazi walipomaliza kutenge vyakula binti Mfalme akahakikisha kila kitu kipo salama kwa ajili ya Mume wake kipenzi. Mjakazi mkuu wa Mfalme aliyeonekana kuwa na sura nzuri na umbo la kuvutia, naye alikuja kuhakikisha usalama wa chakula cha mfalme. Wote waliwakaribisha mabosi wao na tayari kula.


Wakiwa tayari kula mfalme alivunja ukimya uliotawala kwa muda mrefu. 'aladini mwanangu, karibu sana, na kuwa huru' 'ahsante sana baba, nimefurahi sana, pia ninafuraha zaidi kuwa na mwanao' 'mmh mume wangu, mpkaka unitaje' 'hahaaa mwanangu kutajwa si ndio upendo' 'mmmh Ahsante sana mume wangu kipenzi' 'nafurahi sana kama wanangu mnapendana hivyo 'Ahasante sana baba' yalikuwa ni mazungumzo machache kati ya watatu hawa.


Walianza kuzungumza mazungumzo ya hapa na pale, huku wakiendelea kula, na kukisifia chakula. Binti mfalme alionekana mvivu sana wakula huku akitumia muda mwingi kumuangalia Aladini jinsi anavyokata matonge. Aladini alitambua hilo na alihitaji wamtambue kuwa katika kula hanaga uvivu. Wakiendelea kula Aladini alimueleza Mfalme kuwa jumba Analoliona ni jumba lake hivyo anatarajia leo kuhamia yeye na mkewake kwenye jumba lao.
Mfalme alishikwa na taharuki na mshangao mkubwa, kuona kuwa Aladini si tu ni mtanashati bali pia ni kijana Tajiri. Basi waliendelea kuzungumza kisha Aladini na mkewake wakaondoka waende kujiandaaa kwenda kuona nyumba yao mpya. Mama Aladini alishawai kwenda kuhakikisha kuwa mambo yote yapo safi, mama alikwenda kuhakikisha kuwa vitanda na thamani za ndani vipo sawa. Mama alistaajabishw akuona jumba lote lipo sawa kasoro dirisha moja tu. Mama alijuwa lamda vifaa vya yjenzi vilikwisha. Alichokifanya ni kwenda mjini kutafuta mafundi kwa gharama yeyote kutengeneza dirisha. Lakini Loo! Walishindwa kabisa. Mwishowe mama aladini aliwaruhusu mafundi waondoke na akawalipa kwa uchache kutokana na kazi waliofanya.


Msafara mkubwa wa Aladini na mkewake ukaanza kuondoka. Mfalme aliahidi atakuja siku itakayofata, alimsisitiza binti yake aishi salama na mume wake. Aladini akiwa kwenye gari la kuburuzwa na farasi gari lililopambwa kwa vipambio vilivyo vizuri sana na magodoro malaini. Ndani aladini na mkewake walikuwemo. Farasi waliowapanda wallionekana kuwa wamenona sana na waliopendeza. Walikuwa na viatu vigumu vya rangi sawa. Msafara huu ulifatiwa na kundi la wajakazi wa kiume na kike. Inafikia idadi yao watu 52, wote wakiwa katika mavazi mazuri kama vule wanakwenda kumpokea mgeni wa thamani.


Msafara kila ulipopita mjini watu hawakuwacha kumtaja Aladini huku wakitaja hasa utajiri wake. Aladini alipata kutajwa zaidi hata kuliko mfalme. Mama Aladini alipopata habari kuwa Aladini sasa anakuja alipanga watu wake tayari kuwakaribisha kwenye jumba kubwa la kifahari. Hakika Aladini alikuwa ni tajiri hasa, utajiri usiowezakufananishwa katika historia ya nchi. Utajiri ambao chanzo chake haujulikani ijapokuwa pia mwisho wake upo matatani kwani kila mtu alianza kutafuta siri ya mafanikioa ya Aladini. Sambamba na watu hawa waziri mkuu ndiye aliyekuwa adui mkubwa wa Aladini. Alisafiri hasa kwa lengo la kujuwa undani wa ladini na namna ya kumpindua.


Baada ya mwendo wa muda msafara ukafika kwenye jumba la Aldini. Aladini mwenyewe alistaajabu kwa uzuri wa jumba lake. Ijapokuwa aliona jumba lile kwenye maono lakini hakuamini kama litakuwa zuri kisi hiko. Aladini alikaribishwa na dirisha moja amablo halikuweza kumaliziwa. Aladini alifurahi kweli, maana alitambuwa kuwa alifanya hivi kwa makusudi. Kundi kmubwa lilionekana kustaajabu sana kwani katika mji kusikngeweza kupatikana fundi aliye hodari. Jumba lilikuwa zuri hata kama utaanza kulielezea katu hutamaliza.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 141


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Zijuwe Suna zinazofungamana na swaumu na funga ya ramadhani
Soma Zaidi...

Wanaadamu kushindwa Kuandika Kitabu Mithili ya Qur-an:
Soma Zaidi...

Ijuwe Namna ya Kutawadha ama kutia udhu hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Kujielimisha kwa Ajili ya Allah (s.w).
Elimu ndiyo zana'aliyotunukiwa'mwanadamu'ili aitumie'kutekeleza'majukumu'yake kama Khalifa wa Allah (s. Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa
Soma Zaidi...

Maadili katika surat luqman
Soma Zaidi...

Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...

WAQFU WAL-IBTIDAAI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba
Mtume (s. Soma Zaidi...

Hawa ndio waaasi wakwanza wa Dola ya kiislamu wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...