image

HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU

HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU


HADITHI YA ALADINI NA TAA YA MSHUMAA WA AJABU



Hapo zamani katika nchi moja kulikuwepo na mchona ngu yaani fundi cherahani. Fundi huyu alifahamika kwa jina la Mustapha. Mustapha alikuwa na umri 17 toka aanze kati ya kushona. Amekuwa ni fundi maarufu na mwenye kuaminiwa. Mustapha alikuwa na kaka yeke aliyefari zamani pindi alipokwenda nchi za jirani kibiashara na kuvamiwa na mabedui wa jangwani. Huwenda hii ndio ilikuwa sababu ya yeye kujikita kwenye ushonaji na kutofikiria biashara. Siku zote Mustapha aliwaonya watu wa karibu naye waachane na kuwaza biashra za mbali.


Mustapha sasa ana miaka 58 akiwa na mke wake mpezi. Wote walioana wakiwa vijana na sasa wamezeheka wote bila wakiwa na mtoto wao mmoja na wa pekee. Mtoto wao alitambulika kwa jina la Aladin. Aladini alilelewa kwa upendo sana na wa hali ya juu. Huwenda ni kwa sababu kuwa Mustapha hakuwa na mtoto mwingine. Aladini hakujishughulisha na chochote katika uzalishaji wa mali. Alizoea kula na kulala kwa mama na baba. Na baba alikuwa akimsisitiza aladini asiwaze kabisa kufanya biashara. Huwenda ni kwa sababu ya yaliyomkuta kaka yake.


Aladini hakumjuwa ndugu yeyote wa baba yake, na hali hii pia ni kwa mke wa mustapha ambaye hakumjuwa yeyote katika ndugu wa munewe. Ila amefahamu kuwa mumewe alikuwa na ndugu aliyefariki akiwa kwenye biashara. Aladini alikuwa ni mtoto mvivu na asiyefanya kazi. Aladini alikuwa n I mitu na mpenda michezo na ni mkomvi japo hakuwa na nguvu za kujitetea. Mji mzima ulimfahamu aladini kama mtoto mpumbavu na mtukutu. Aladini sikuzote alijivunua kuishi na wazazi wake, na hasa [ale anapohitaji kitu haraka wazazei wake humpatia. Aladini alimpenda sana baba yake na mama yake.


Maisha siku zote yanaendelea hata kama wengine wanadhulumu n kudhulumiwa. Hata ikiwa wengine wana kufa na kufiwa huu haukuwa mwisho wa maisha na dunia. Na hali ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa Aladini, baba yake alifariki ghafla. Wakati huo Aladini akiwa na umri wa Miaka 21. aladini mvivu, mgomvu na mtukutu sasa amefiwa na baba. Aladini ameachiwa ulezi wa kumlea mama yake aliyekuwa ni mzee. Kila akifikiria haya alijuta kuchesea umri wake, alilia sana hata kufikia kukufuru kwa maomboloezo yake. Watu walimfuata kumsi. Mazishi yalifanyika na hakuna hata ndugu wa Mustapha aliyekuja.



Hatimaye siku za matanga zikaisha na watu wakaendelea na shughuli zao. Aladini kila akiangalia mashine ya baba ya kushonea hakuwa na majibu sahihi. Aladini hakuweza chochote. Mama yake alimtaka aladini aanze biashara kwa baba yake amewacha pesa nyigi. Aladini hakuna aliwezalo. Hatimaye mwezi ukaisha na aladini akasahau yote yaliyomkuta. Aladini hakuwacha mambo yake. Mama alifungua kaduka kadogo pale nyumbani. Kaduuka ka kuuza nguo. Mama alijitahidi kumnyoosha Aladini bila mafanikio. Hata akawaza bora angekuwepo ndugu wa Mustapha huenda Aladini angenyooka kwa kusemwa na mwanaume.


Siku moja Aladini akiwa katika pirika zake alikutana na mzee mmoja wa kiafrika. Mzee mrefu na mweui sana. Alikuwa na ndevu nyeupe sna zilizokuwa ndefu. Kijana alimuita Aladinina kumuuliza hivi ni kweli wewe ni mtoto wa Mustapha? Aladini akajibu “naam ni mimi” yule mzee akamkumbatia Aladini na kumbusu kwenye paji la uso. “mimi ni baba yako mdogo, nilipotea baada ya kuvamiwa nikiwa njiani kibiashara” Aladini hakuamini maana sikuzote alitambuwa kuwa baba yake mdogo amefariki. Mzee akamwambia aladini “nenda nyumbani mwambie mama nitakuja jioni” mzee akampatia Aladini pesa kiasi kidogo.


Aladini alikwenda mbia hadi kwa mama yake na kweda kutoa habari. Mama naye hakuamini kuwa mkombozi amekuja. Atakayenyoosha tabia ya aladini sasa kaja. Ijapokuwa hivyo lakini mama alikuwa na mashaka sana. Inakuwaje mtu tuliyejuwa amefariki yapata hata miaka 30 iliyopita na sasa amekuja. Ila jambo hili halikuchukuwa nafasi kwa mama huyu, kwa alikuwa na furaha kwa kupatikana mlezi wa Aladini. Mama aliandaa chakula kiuri na nyama kwa ajili ya mgeni. Vinywaji safi viliandaliwa.


Mheni akawasili mida ya jioni, mama alifurahi sana baada ya kumtambuwa shemeji yake wa pekee. Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa. Baada ya chakula na mazungumzo ya hapa na pele mzee akamuuliza Aladini kuwa anajishughulisha na kitu gani. Aladini hakujibu kitu. Hapo mama akafunguka kuhusu utukutu na tabia ya Aladini. Ukweli ni kuwa mzee alitambuwa kila kitu kuhusu Aladini, na ukweli ni kuwa huyu si baba yake na aladini. Ila ni kuwa mzee ana kamchezo anataka akafanye katika familia hii ya mzee Mustapha. Mzee akamueleza Aladini kuwa atamfungulia duka kubwa na zuri katikati ya mji. Hatimaye usuku ukazidi na mzee akalala, na Aldini pia.


Asubuhi n amepema Mzee alipopata kifungua kinywa alimchukuwa Aladini kuelekea mtaani. Mzee alimnunulia Aladini nguo nzuri na za kisasa. Kisha akaanza kumuonesha maeneo yaliyo mazuri kwa kuanzisha biashara ya duka. Aladini alionekana kuvutiwa sana na mawazo ya baba yake mdogo. Aadini alijiulizwa kwa nini baba asingekuwa na mawazo kama ya huyu. Hapa aladini akapata jibu ni kwa sababu baba huyu ni mgfanyabiashara toka zamani. Aladini na baba yake walirejea nyumbani wakati wa usiku. Mama alifurahi sana kumuona mwanae yupo kwenye mavazi mazeuri ya kupendeza. Mama pia alifurahi kwa mawazo mapya ya kibiashra aliyopata mwanae.



Asubuhi mzeee na Aladini walipopata kifungua kinywa walitoka tena. Walianzi mitaani na kuangalia biashara za mtaani na uanza kufikiria ni biashra gani watauza. Kisha waenelea lutebea ne ya nji. Baba huyu alikuwa na maneno matamu sana. Niani alimsimulia Aladini hadithi nzuri sana na za kupendenza. (utakuja zipata hadithi hizi baada ya hadithi ya Aladini, ili tusirefushe kisa hiki). walikwenda nje ya mji hadi wakafika sehemu moja ya mapango. Aladini alikuwa ameshoka na alimtaka baba yeke warudi. Lakini kila anapotaka kusema huwa anasimuliwa hadith nzuri na kusahau.


Basi walipofika eneo hili mzee akamueleza Aladini kuwa hapa ndio mwish wetu hatutaendelea tena. Mzee akamuagiza aladini alete vikuni ili wawashe moto wachome viazi wapate kula. Aladini akaleta kuni na mzee aliwasha moto kwa kutumia poda flani aliyounyunyiza kwenye kuni baada ya kuzungumza maneno yasiyofahamika.
Aladini alishangaa na kuogopa. Mzee akamsihi Aladini asiogope kwani hayo aliyofnya ni urithi wa familia yao.


Kisha mzee akazungumza tena maneno flani na kuelekeza mkono kwenye majabali. Hapo hapo kukatokea mtetemo wa ardhi. Aladini akataka kukimbia mzee akamtandika kofi la uchogo na kumwambia “Tulia Aladini mwanangu, hupo chini kuna mali, mali hiyo hakuna yeyote anayeweza kuitoa ila wewe”. Aladini alishangaa sana na kufurahi baada ya kutajiwa mali. Mzee akanza kumpatia maelekezo Aladini namna ya kuitoa hiyo mali.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 759


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

FAMILIA MPYA BAADA YA HARUSI
Soma Zaidi...

Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Muendelezo wa hadithi ya mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Ndoa ya siri
NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Soma Zaidi...

Kwanini dirisha moja?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

UGENI WA DHATI
Soma Zaidi...

JARIBU LA PILI LA ALADINI
Soma Zaidi...

Jaribio la pili la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Aladini katika pango la utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Penzi la Mitihani
MTIHANI PENZINI Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Soma Zaidi...

Mshenga wa aladini mbele ya mfalme
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...