katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu vitamini K, kazi zake mwilini, athari za upungufu wake, na vyakula vyenye vitamini K kwa wingi
Vitamini K ni moja ya vitamini ambavyo miili yetu inavihitaji kwa ajili ya shughuli mbalimbali muhimu. Endapo upungufu wa vitamini hii utatokea, madhara makubwa ya kiafya yanaweza kumkumba mtu. Katika makala hii, tutaangalia zaidi kuhusu vitamini K, vyanzo vyake, kazi zake mwilini, athari za upungufu wake, na athari za kuzidi kwa vitamini K mwilini.
Vitamini ni kampaundi za ogania ambazo zinahitajika na mwili kwa ajili ya ukuaji na utendaji wa michakato ya kibaiolojia ndani ya miili yetu (metabolism). Ni virutubisho ambavyo havitengenezwi ndani ya miili yetu. Vitamini vipo katika makundi mawili makuu: fat-soluble (hupatikana kwenye mafuta) na water-soluble (hupatikana kwenye maji).
Vitamini K ni vitamini katika kundi la fat-soluble ambazo zimetokana na kampaundi za naphthoquinone. Vitamini hivi vimeitwa K kutokana na neno la lugha ya Danish "koagulation" ambalo lina maana ya "coagulation" kwa Kiingereza, yaani kuganda. Hii ni kwa sababu vitamini K inahitajika mwilini kusaidia mchakato wa kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.
Kwa mara ya kwanza vitamini K vilianza kuandikwa kwenye maandishi na mwanasayansi wa Danish Henrik Dam mwaka 1929 alipokuwa akifanya tafiti juu ya kazi za cholesterol mwilini. Wataalamu wa lishe wameigawa vitamini K katika makundi mawili: K1 na K2. Vitamini K1, kitaalamu huitwa phytonadione, hupatikana kwenye mboga za majani, na vitamini K2, kitaalamu huitwa menaquinone, hupatikana kwenye nyama, mayai, na maziwa.
Hii ndiyo kazi kuu ya vitamini K. Pindi unapopata jeraha lolote ambalo litapelekea damu kutoka, vitamini K huhakikisha damu inaganda na kusimamisha kutokwa na damu. Vitamini K hutumika katika kutengeneza prothrombin, factors VII, IX, pamoja na X, ambazo zote huitwa clotting factors na husaidia kusimamisha damu isiendelee kutoka kwenye jeraha.
Vitamini K husaidia katika kuboresha afya ya mifupa kwa kudhibiti ujazo na tungamo la mifupa na kuzuia mifupa kuwa midhaifu na kupasuka kwa urahisi (osteoporosis). Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini K ni muhimu katika kulinda mifupa dhidi ya maradhi haya.
Tafiti zinaonyesha kuwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70 ambao wana vitamini K vya kutosha kwenye damu zao wana uwezo mkubwa wa kukumbuka kuliko wale wenye upungufu wa vitamini K.
Vitamini K husaidia kushusha presha ya damu kwa kuzuia kuganda kwa madini ndani ya mishipa ya damu. Hii husaidia moyo kusukuma damu bila matatizo na kupunguza athari za kupata stroke (kupooza).
Baadhi ya waandishi wanaeleza kuwa vitamini K husaidia kulinda mwili dhidi ya vimbe za saratani, lakini bado hakuna ushahidi wa kisayansi wa kutosheleza kuthibitisha madai haya.
Ijapokuwa vitamini K vina faida kubwa ndani ya miili yetu, vikizidi mwilini vinaweza kusababisha madhara ya kiafya kama:
Vitamini K unaweza kuvipata kwa njia ya chakula au kwa kumeza vidonge. Kwa wale ambao wana upungufu wa vitamini K, vidonge vinaweza kununuliwa kwa kufuata maelekezo ya daktari. Ni muhimu kufuatilia makala nyingine za afya ili kupata maarifa zaidi na kudumisha afya bora kwa kutumia vitamini na virutubisho sahihi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowKatika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu maji, faida zake na upungufu wake. Pia utajifunza vyakula vyenye maji kwa wingi
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kijifunza kuhusu faida za kiafya za lula kungumanga
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula tangawizi
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula samaki
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula ukwaju
Soma Zaidi...Katika somohili utakwenda kujifunzafaida za kiafya za kula mbegu za pilipili. Hapa ttunazunumzia pilipili kwaujumla bila kujali ni aina gani ya pilipili.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza Faida za kiafya za kula Mchicha
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula topetope
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula pera
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwedna kujifunz afaida z akiafya zinzopatikana kwneye supu ya pweza.
Soma Zaidi...